Mwl Solomon
Member
- Oct 25, 2010
- 24
- 14
Malumbano ya hoja yasiyo na uvumilivu na yaliyojikita katika kuenguana hayawezi kukisaidia CDM.
Watakao iua CHADEMA ni wanachadema wenyewe kwa kuwashinikiza viongozi wetu kujenga moyo wa kufukuzana na kusemana hovyo hovyo. Leo utasikia Shibuda, kesho Zitto, baada ya muda Mh Godbless hatumwelewi!!
Mara zote hauwezi kujenga amani na umoja eti kwa msingi wa kufukuzana na kusemama hovyo.
Kwa mfano, issue ya Shibuda: Kwanza lazima tuelewe mtu mnayesema ni mamruki, Shibuda. Huyu ndg move yake ya kuhamia CDM imetokana na kuenguliwa ktk kura za maoni za CCM 2010. Na sababu kubwa ni kwamba alikuwa ni mtu wa kwanza kabisa kujitokeza hadharani kutangaza nia ya kumpatia JK changamoto ktk kura za maoni ndani ya CCM kwa post ya URAIS . Ndiye aliyeonekana katika TV ya Mlimani akihojiwa na ndg Damu-Mbaya kwa lengo la kutangaza nia. Baada ya kufanya hivyo, Makamba aliweka wazi kwamba CCM itamsimamisha JK, anayetaka kugombea urais atafute chama kingine lkn kwa CCM NO!
Kwa hiyo, si kweli kwamba huyu ndg ni mamluki. Wana CCM nao walimng'oa baada ya kuona kwamba anataka kuleta mvutano usiokuwa wa lazima ndani ya chama kwa habari ya mtu wa kumsimamisha kugombea kiti cha URAIS. CCM nayo haimtaki!
Nini kifanyike kwa Shibuda: Ninachokiona kwa shibuda ni dalili za frustrations, ambazo zinatokana na kushindwa kuelewa hatima yake iko wapi kisiasa! Ikiwa CDM mtamfukuza mjue atahamia chama kingine cha upinzani na wala si kurudi CCM. Hata ikiwa atarejea CCM hana jipya zaidi ya kukalia benchi. All in ALL kuna mambo mengi mazuri ambayo CDM inaweza kujipatia kutoka kwa Shibuda, moja kubwa likiwa ni moyo wa ujasiri wa kudiriki kufanya au kusema kile anachokiamini. Pengine, anahitaji msaada wa kisaikolojia tu kuweza kumfanya kuwa na mfumo wa ku-consult wakubwa wake kabla hajatoa contradicting statements, hasusani msimamo wa chama unapohitajika. Nadhani kumfukuza si jambo la kujenga.
Kutupiana maneno makali yasiyokuwa na ukweli wowote pia kwaweza kuwa ni mwiba mwingine unaoinyemelea CDM. Mwiba huo utakapojikita katika mbavu za CDM bila shaka kichomi kitakuwa ni pelekeo la anguko lake!. Mh Zitto amekuwa ni miongoni mwa wanaoandamwa na wakati fulani kuitwa wasiliti wa CDM, au Mamruki! Akiwepo kwenye msafara wa JK anaitwa mamruki etc. Sasa, ninalojiuliza ambalo pengine wengine hujiuliza pia ni kwamba, tafsiri ya mwanachama wa chama cha upinzani na ushiriki wake ktk shughuli za kitaifa ni upi? Je! Ni mtu yule amwonaye kiongozi wake wa kitaifa kama adui na kwamba hawezi kushirikiana naye? Je! Ni yule ambaye hawezi kutoa maoni na mtazamo wake pale ambapo anaona wenzake wengi wanamtazamo wa watofauti na alionao? Je! Mwanachama na kiongozi wa chama cha upinzani ni yule ambaye hawezi kujikwaa katika ulimi wake? Ikiwa aweza kujikwaa katika ulimi wake kama wengine, Je! hana fursa ya kusamehewa na kuheshimiwa utu wake?
Serikali inahitaji uwepo wa wapinzani makini, lakini kwa mwelekeo wa CDM wa kurushiana maneno kila uchwao, umakini huo upo hatarini na huenda kufikia 2015 mzozo baina ya viongozi na wanachama ukawa umefikia hatua yakuwa ni mchongoma.
Bila shaka serikali yoyote iliyo makini inahitaji vyama makini vya upinzani vinavyoweza kuongeza tija katika kuikosoa na kutoa mawazo yake. Lakini chama chochote kilichoandamwa na malumbano ndani yake, kamwe hakiwezi kujiwekea heshima bora ya kuikosoa serikali inayotawala. Hivyo basi, badala ya CDM kufikiria kufukuzana na kushutumiana kila iitwapo leo, wajikite kutafuta chanzo cha mashutumu hayo, na kuyatatua.
Nawasilisha