Malumbano ya hoja yasiyo na uvumilivu na yaliyojikita katika kuenguana hayawezi kukisaidia CDM.
Watakao iua CHADEMA ni wanachadema wenyewe kwa kuwashinikiza viongozi wetu kujenga moyo wa kufukuzana na kusemana hovyo hovyo. Leo utasikia Shibuda, kesho Zitto, baada ya muda Mh Godbless hatumwelewi!!
Mara zote hauwezi kujenga amani na umoja eti kwa msingi wa kufukuzana na kusemama hovyo.
Kwa mfano, issue ya Shibuda: Kwanza lazima tuelewe mtu mnayesema ni mamruki, Shibuda. Huyu ndg move yake ya kuhamia CDM imetokana na kuenguliwa ktk kura za maoni za CCM 2010. Na sababu kubwa ni kwamba alikuwa ni mtu wa kwanza kabisa kujitokeza hadharani kutangaza nia ya kumpatia JK changamoto ktk kura za maoni ndani ya CCM kwa post ya URAIS . Ndiye aliyeonekana katika TV ya Mlimani akihojiwa na ndg Damu-Mbaya kwa lengo la kutangaza nia. Baada ya kufanya hivyo, Makamba aliweka wazi kwamba CCM itamsimamisha JK, anayetaka kugombea urais atafute chama kingine lkn kwa CCM NO!
Kwa hiyo, si kweli kwamba huyu ndg ni mamluki. Wana CCM nao walimng'oa baada ya kuona kwamba anataka kuleta mvutano usiokuwa wa lazima ndani ya chama kwa habari ya mtu wa kumsimamisha kugombea kiti cha URAIS. CCM nayo haimtaki!
Nini kifanyike kwa Shibuda: Ninachokiona kwa shibuda ni dalili za frustrations, ambazo zinatokana na kushindwa kuelewa hatima yake iko wapi kisiasa! Ikiwa CDM mtamfukuza mjue atahamia chama kingine cha upinzani na wala si kurudi CCM. Hata ikiwa atarejea CCM hana jipya zaidi ya kukalia benchi. All in ALL kuna mambo mengi mazuri ambayo CDM inaweza kujipatia kutoka kwa Shibuda, moja kubwa likiwa ni moyo wa ujasiri wa kudiriki kufanya au kusema kile anachokiamini. Pengine, anahitaji msaada wa kisaikolojia tu kuweza kumfanya kuwa na mfumo wa ku-consult wakubwa wake kabla hajatoa contradicting statements, hasusani msimamo wa chama unapohitajika. Nadhani kumfukuza si jambo la kujenga.