Naihurumia CHADEMA kwa malumbano..... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naihurumia CHADEMA kwa malumbano.....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwl Solomon, Jul 14, 2011.

 1. Mwl Solomon

  Mwl Solomon Member

  #1
  Jul 14, 2011
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Malumbano ya hoja yasiyo na uvumilivu na yaliyojikita katika kuenguana hayawezi kukisaidia CDM.

  Watakao iua CHADEMA ni wanachadema wenyewe kwa kuwashinikiza viongozi wetu kujenga moyo wa kufukuzana na kusemana hovyo hovyo. Leo utasikia Shibuda, kesho Zitto, baada ya muda Mh Godbless hatumwelewi!!

  Mara zote hauwezi kujenga amani na umoja eti kwa msingi wa kufukuzana na kusemama hovyo.

  Kwa mfano, issue ya Shibuda: Kwanza lazima tuelewe mtu mnayesema ni mamruki, Shibuda. Huyu ndg move yake ya kuhamia CDM imetokana na kuenguliwa ktk kura za maoni za CCM 2010. Na sababu kubwa ni kwamba alikuwa ni mtu wa kwanza kabisa kujitokeza hadharani kutangaza nia ya kumpatia JK changamoto ktk kura za maoni ndani ya CCM kwa post ya URAIS . Ndiye aliyeonekana katika TV ya Mlimani akihojiwa na ndg Damu-Mbaya kwa lengo la kutangaza nia. Baada ya kufanya hivyo, Makamba aliweka wazi kwamba CCM itamsimamisha JK, anayetaka kugombea urais atafute chama kingine lkn kwa CCM NO!

  Kwa hiyo, si kweli kwamba huyu ndg ni mamluki. Wana CCM nao walimng'oa baada ya kuona kwamba anataka kuleta mvutano usiokuwa wa lazima ndani ya chama kwa habari ya mtu wa kumsimamisha kugombea kiti cha URAIS. CCM nayo haimtaki!

  Nini kifanyike kwa Shibuda: Ninachokiona kwa shibuda ni dalili za frustrations, ambazo zinatokana na kushindwa kuelewa hatima yake iko wapi kisiasa! Ikiwa CDM mtamfukuza mjue atahamia chama kingine cha upinzani na wala si kurudi CCM. Hata ikiwa atarejea CCM hana jipya zaidi ya kukalia benchi. All in ALL kuna mambo mengi mazuri ambayo CDM inaweza kujipatia kutoka kwa Shibuda, moja kubwa likiwa ni moyo wa ujasiri wa kudiriki kufanya au kusema kile anachokiamini. Pengine, anahitaji msaada wa kisaikolojia tu kuweza kumfanya kuwa na mfumo wa ku-consult wakubwa wake kabla hajatoa contradicting statements, hasusani msimamo wa chama unapohitajika. Nadhani kumfukuza si jambo la kujenga.

  Kutupiana maneno makali yasiyokuwa na ukweli wowote pia kwaweza kuwa ni mwiba mwingine unaoinyemelea CDM. Mwiba huo utakapojikita katika mbavu za CDM bila shaka kichomi kitakuwa ni pelekeo la anguko lake!. Mh Zitto amekuwa ni miongoni mwa wanaoandamwa na wakati fulani kuitwa wasiliti wa CDM, au Mamruki! Akiwepo kwenye msafara wa JK anaitwa mamruki etc. Sasa, ninalojiuliza ambalo pengine wengine hujiuliza pia ni kwamba, tafsiri ya mwanachama wa chama cha upinzani na ushiriki wake ktk shughuli za kitaifa ni upi? Je! Ni mtu yule amwonaye kiongozi wake wa kitaifa kama adui na kwamba hawezi kushirikiana naye? Je! Ni yule ambaye hawezi kutoa maoni na mtazamo wake pale ambapo anaona wenzake wengi wanamtazamo wa watofauti na alionao? Je! Mwanachama na kiongozi wa chama cha upinzani ni yule ambaye hawezi kujikwaa katika ulimi wake? Ikiwa aweza kujikwaa katika ulimi wake kama wengine, Je! hana fursa ya kusamehewa na kuheshimiwa utu wake?

  Serikali inahitaji uwepo wa wapinzani makini, lakini kwa mwelekeo wa CDM wa kurushiana maneno kila uchwao, umakini huo upo hatarini na huenda kufikia 2015 mzozo baina ya viongozi na wanachama ukawa umefikia hatua yakuwa ni mchongoma.

  Bila shaka serikali yoyote iliyo makini inahitaji vyama makini vya upinzani vinavyoweza kuongeza tija katika kuikosoa na kutoa mawazo yake. Lakini chama chochote kilichoandamwa na malumbano ndani yake, kamwe hakiwezi kujiwekea heshima bora ya kuikosoa serikali inayotawala. Hivyo basi, badala ya CDM kufikiria kufukuzana na kushutumiana kila iitwapo leo, wajikite kutafuta chanzo cha mashutumu hayo, na kuyatatua.

  Nawasilisha
   
 2. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #2
  Jul 14, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Naamini Chadema watasikia utetezi wa Shibuda .Nao watakuwa wameona maoni yako na nadhani hawatakurupuka .Malumbano penye wengi ni kawaida .Ondoa wasi wasi mwisho wa siku Chama ni kimoja na wataendelea na mapambano .
   
 3. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #3
  Jul 14, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,004
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  tabia za kuleana ndo zimezaa matunda ya kuchelea kujivua gamba kwa CCM tena kwa kuogopana, hakuna kulala, kila anayevurunda timulia mbali, shibuda ni nani hata asitumiliwe kwa makosa?? najua ww ni mtu wa magamba na hizi ni propaganda, km umefuatiliana kikao chenu wanamagamba kule dodoma ilikuwa kila mtu anaogopa kutaja jina la anayetajwa kuwa ni fisadi, hata mwenyekiti JK anauliza, ''ni nani hao? watajenio'' hembu ona unafiki huo, hatutaki kufika huko, kila anayekiuka sera za CDM timulia mbali hata akiwa Dr.Slaa. hakuna kuoneana haya. tunataka kuijenga nchi yetu upya.
   
 4. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #4
  Jul 14, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,004
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  haya nakujibu kwa kufuata bold ya kila sentesi.
  kwako wewe shibuda kuleta mvutano usiokuwa wa lazima ndani ya cdm ni bora zaidi?

  frustrations? are you serious?

  not from Shibuda

  yaani kukiuka sera za chama??????????


  cdm ni chama cha umma sio chuo kufundisha watu km shibuda saikolojia

  hapa sijakuelewa, kwako wewe maneno yenye ukweli ni yepi?
   
 5. SILENT WHISPER

  SILENT WHISPER JF-Expert Member

  #5
  Jul 14, 2011
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 2,231
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  shibuda ni hatari...ATIMULIWE..! chama kwa sasa kina makamanda hodari ...tukilea wajinga kama shibuda chama chafa!
   
 6. Mwl Solomon

  Mwl Solomon Member

  #6
  Jul 14, 2011
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndg Zembemkuu, katika kila ngazi na eneo la maisha hauwezi kuondoa huduma ya Saikolojia. Dr Slaa na wanazuoni wengine wanaweza kuelewa hili. Unaweza kuishia kumtimua mtu ambaye tatizo lake laweza kuisha kwa counselling tu.
  Siwezi kukushangaa kwa sababu inategemea unaliangalia suala hili katika nafasi ipi. Kwa kiongozi ambaye ni Transactional Leader, atachukua mtazamo kama wako ambao unataka kufanya kila kitu bora liende, mwishowe hugonga pua kwenye jiwe. Lakini kwa Transformational Leader ataelewa ninachokizungumza hapa. Transformational Leader hutafuta kumfanya mtu awe bora kwa kuainisha mapungufu aliyonayo na kutafuta namna ya kumsaidia. Viongozi wengi wa kisiasa wanahitaji kusaidiwa na professional counselors/ Psychologists ili wawe wazuri zaidi.

  Dr Slaa ni psychologist na anaweza kuwasaidia watu wa staili kama ya Shibuda na Zitto ambao wengi wamekuwa wakiwarushia maneno. Naamini kwamba wanayonia thabiti ya kuwatumikia wananchi wakiwa katika CDM, lakini kukiwa na transactional leaders wengi wanaoangalia masuala kwa urefu wa pua inapoishia, hakuna awezaye kujenga chama chochote kile kwa ubora unaotakiwa!
   
 7. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #7
  Jul 14, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,694
  Trophy Points: 280
  Mwl Solomon,

  haya uliyosema ndiyo yanayomfanya Julius Malema Mwenyekiti wa vijana wa ANC South Africa Asifukuzwe,badala yake anakuwa shaped kuwa better,haya ndiyo yaliyomfanya Hon.patrick wa PDP ya Nigeria asifukuzwe hadi alipohama mwenyewe kuingia chama cha Action Congress.

  Haya uliyosema ndiyo yaliyomfanya Colin Powel aendelee kuwa mwanachama wa chama cha Republican kule United States.Chadema ni chama makini hakitafanya uamuzi kwa kukurupuka lakini tukubali tu kwamba Demokrasia yetu kama Taifa ina changamoto kubwa.Ndiyo maana huwa mara nyingi najiuliza,is democracy universally beneficial to nations ?
   
 8. k

  kiloni JF-Expert Member

  #8
  Jul 14, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 575
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  FIDEL CASTRO Aliamuru rafiki yake kipenzi aliyepigania naye UHURU auawe kwa sababu alikutwa na tuhuma za madawa ya kulevya.
  Uongozi ni dhamana ya wananchi siyo ya kulindana
   
 9. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #9
  Jul 14, 2011
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  CDM,watakuwa wamekusoma na labda wamekuelewa,na imani watachukua maamuzi yenye busara na hekima kwa ajili ya chama,ili kisijepoteza mvuto uliojijengea kwa wananchi.Ila kuhusu Shibuda,nahisi km hafai,inaonekana anataka madaraka ya harakahara ndani ya chama wakati bado ni kinda ktk cdm
   
 10. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #10
  Jul 14, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,004
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  kwa kuendelea kumuacha shibuda eti kwa sababu hizi mkuu, hilo sikubaliani nalo, unaweza ukalinganisha siasa za hao uliowataja hapo juu na uzito wa kile shibuda anachokifanya, ni tofauti kabisa, inawezekana na ni vyema km hilo linafanyika (mm ni architect, sijui taaaluma ya siasa) au labda kwa sababu ya ushabiki wangu tu.
   
 11. Mwl Solomon

  Mwl Solomon Member

  #11
  Jul 14, 2011
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndg yangu ninakushukuru. Nami ninachomaanisha siyo kufuga wezi na watu wasiowaadilifu wenye lengo la kuhatarisha ustawi wa chama, na kwa lugha nyingine kuhatarisha ustawi wa taifa. Ninasema haya kwasababu, ustawi na uimara wa CDM na vyama vingine vya siasa hauwezi kuishia kuwanufaisha wanachama wa CDM pekee, bali utalinufaisha taifa zima. Ndiyo, maana kama umempata Ben amechangia kuonyesha kwamba hekima na uangalifu makini unahitajika tunapokuwa tumefikia kushughulikia masuala ya viongozi ndani ya vyama vyetu wanaoonekana kuwa aidha wamekosa au kupotoka!

  Mimi binafsi si mwanachama wa CDM lakini kazi zifanywazo na CDM nazikubali na maoni yangu hayamaanishi ninaionea gele CDM! Ustawi wa CDM kama chama unanihusu kwasababu utaleta ustawi wa taifa ambalo mimi ni sehemu yake.
   
 12. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #12
  Jul 14, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,004
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  hekima ipo CDM ndo maana tangu kuanzishwa kwake kimeendelea kukua siku hadi siku, na kingine bwana mwl, heading ya thread hii imekaa ndivyo sivyo, na pengine sijui unakusudia nini. hadi sasa tunanufaika na CDM ila tunataka kunufaika zaidi, kujivua gamba kwa CCM ni moja ya faida tunazoziona, pia nakukumbusha kuwa USHABIKI WA CHAMA KWENYE SIASA SIO USHABIKI WA CLUB YA TIMU YA MPIRA MKUU. mm ni mshabiki wa simba damu damu, huwezi hata siku moja kunishawishi nihamie Yanga, ila kwenye siasa lolote laweza kutokea, karibu sana CDM mwl.
   
 13. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #13
  Jul 14, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  ni kweli lazima shibuda apewe nafasi ya kujitetea lakini jamani wote tulimsikia mwanasiasa huyu mkongwe akikiuka kwa MAKUSUDI sera za chama chake bungeni huku akipigiwa makofi na wabunge wa chama tawala.

  in other words ni sawa na kuwasengenya wazazi wako mbele ya kadamnasi ya watu bila kujua athari zitakazotokea kifamilia. Huyu mzee kwa makusudi kabisa aliamua kukijeruhi chama.

  Mbunge mwakilishi wa watu anapingana na sera zake MAKUSUDI tena Bungeni mbele ya wabunge wenzake wa upinnzani, mbele ya kiongozi wake wa upinzani, mbele ya mwenyekiti wake ni dharau kubwa sana.

  Mimi sishabikii Shibuda afukuzwe laa hasha, bali nataka haki itendeke, kwa kweli ulikuwa USALITI mkubwa lazima chama kichukue hatua kali.

  Napendekeza apewe adhabu inayostahili kosa lake, kama si kufukuzwa basi akae chini ya uangalizi maalum wa kimaadili wa chama kwa miezi isiyopungua sita. otherwise kufuga kipele basi utatibu donda ndugu.

  Lazima CHADEMA ijitue baadhi ya mizigo isiyobebeka mapema - Kumbukeni wananchi wako radhi kuwapa ridhaa ya kuongoza nchi hii 2015 - sasa watu wa type kama hii ndiyo ni mizingo yenyewe hii ninayoongelea.

   
 14. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #14
  Jul 14, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,694
  Trophy Points: 280
  Zumbemkuu,
  I dont condone the culture of impunity. Sasa kwa mfano Julius malema alifikia hatua ya Kuimba wimbo uliopigwa marufuku wa 'kill the boers'.huu ni wimbo uliokatazwa baada ya harakati za kupinga ubaguzi Afrika kusini kufika mwisho,sasa Julius malema kama kiongozi wa juu wa kisiasa kuimba wimbo huu na wafuasi wake ilikuwa against the spirit of reconcilliation,agaiunst the spirit of healing the social fabrications.Huo ni Wimbo ambao uli-cross the values of ANC kama chama kinachoongoza serikali inayo-struggle kuponya makovu ya ubaguzi na kutishia uhai wa Taifa zima la South Africa

  Colin Powel alimuunga mkono waziwazi mgombea wa Democrats Barack obama badala ya yule wa chama chake Senator John Maccain(Republican).Hebu niambie kwa hali kama hii ingekuwa ni wanachama wa chama cha siasa Tanzania hii angepona kweli?Je kosa kama hili ni dogo?

  Ni lazima tujikomaze kidemokrasia na kutafuta values and lines based on ideologies ambazo ni uncompromised.Kwa mfano hii trend ya wanasiasa kufanya cross carpeting kuingia kwenye vyama vingine kipindi cha uchaguzi ni symptoms za Ombwe la kiitikadi kwenye demokrasia ya vyama vingi kitu ambacho kinawafanya wanasiasa hao kushindwa ku-adopt political culture and environment of their new political parties.Tukishagundua hilo basi ni lazima tutafute another mechanism to solve these problems amicably at the same time keeping in mind that human beings are social animals,conflicts are necessary because being a social animal your interests will be self centered contrary to the group interests hence conflict of intersts.Kwa hiyo pia ni lazima suala la conflict management liwe na mechanisms ambazo hazitasababisha more conflict.But all in all conflict is very very necessary.

  Kwa kuangalia mapungufu ya kidemokrasia,kiitikadi na katika values chama kinaweza kuaamua njia sahihi ya kumuwajibisha au kum-shape kwa kupata maoni ya wakazi wa jimbo lake,kwa kumpa onyo,kumpa nafasi ya kujutia au kumfukuza kutokana na mazingira kwa kuweka balancing ya yote niliyosema hapo juu.Hata hivyo naona CHADEMA ndicho chama kilichoko in a better position to solve such kind of problems than any other Political party in Tanzania.Tukipe ushauri wa heri kwa wala wanaokitakia mema,tukikosoe kwa kujenga na tukipe sapoti.Hili ndilo tumaini jipya kwa Mtanzania,Chadema ndiyo nchini ya kweli kwenye treni hii ya ukombozi wa pili Tanzani.The future of tanzania depends on the survival and sustainability of CHADEMA as awaiting Government ! ! !
   
 15. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #15
  Jul 14, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Shibuda ni mzee wetu, ni mwanasiasa wa miaka mingi sana, kitendo alichokifanya si cha bahati mbaya ila alikusudia kukisema chama chake mbele ya viongozi wake waandamizi tena ndani ya Bunge, anajua fika kama kuna jambo haafikiani nalo basi kuna vikao vya chama, je huyu mzee hajui utaratibu wa kutatua matatizo yanayojitokeza hasa haya ya ki sera?

  Angekuwa mwanasiasa kijana ni rahisi kumsaidia, sasa mzee wa miaka 60 na ushee unamsaidia vipi ndugu zangu? ndo maana tunasema chadema iwe makini sana na jambo hili mapema.

  Mnaomtetea hamkitakii mema chadema. anyway kwangu mimi huyu mzee ni mzigo.

  Demokrasia ya Tanzania bado changa kulinganisha na za wenzetu, sisi kauli kama hii ya huyu mzee inaweza kukiumiza chama vibaya sana kukilinganisha na kauli kama hii kama endapo ingetolewa na wabunge wa huko ughaibuni Mr Ben.


   
 16. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #16
  Jul 14, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,004
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  labda! ngoja tusubiri tuone mwisho wa hii sinema. ndo maana taaluma zinatofautiana, ningekuwa mm kwenye position ya uhakimu wa kumhukumu shibuda angekiona cha mtema kuni, looh!
   
 17. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #17
  Jul 14, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  mzee wa miaka 60 na ushee unaanzia wapi kum-shape? tunashape wanaisasa vijana.
   
 18. Mwl Solomon

  Mwl Solomon Member

  #18
  Jul 14, 2011
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ben, I support your constructive ideas. Tunahitaji watu wenye kuainisha chimbuko la matatizo tuliyonayo katika uongozi ndani ya taifa hili na si watu wanaotaka kuziba viraka pasipokujua chanzo cha kutoboka kwa nguo inayohitaji viraka. Kimsingi migongano ni mizuri ikiwa itawezakuwa managed vyema kwa vile hupelekea aliyekubwa na migongano (conflicts) kupata kujifunza namna ya kwenda mbele.
   
 19. Mwl Solomon

  Mwl Solomon Member

  #19
  Jul 14, 2011
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama hawezi kuiacha tabia yake ndipo tutajua na hapo, anafukuziwa mbali kama nzi.
   
 20. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #20
  Jul 14, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Timueni tu.
  Hapakosi watu wa kuokota mbao za vipande vya CHADEMA iliyovunjika vunjikia baharini
   
Loading...