Naibu Waziri wa Afya, Dr. Mollel amjibu Fr. Kitima kuhusu Corona. Amkosoa na kumuelimisha maana ya UKWELI

Kwa jinsi loyce nyanda (mtozi) alivyokua akimbana naibu waziri Kwa maswali,
nikajua muheshimiwa atakasirika na kumwambia "unajua unaongea na nani" alafu aache kipindi na kuondoka badala yake alikua ana punch maswali kisomi uku anaiba muda ili kipindi kiishe bila nyanda kujijua.

Hadi mwisho wa mchezo mtozi hakupata alichotaka kiende Kwa hadhira, anatazama saa yake dakika tisini za mchezo zimemalizike daktari 3 mtozi 0.
Game ilikua tamu sana
 
Mjadala uko mubashara kupitia kipindi cha Ajenda kinachoongozwa na mtangazaji Aloyce Nyanda Star tv.

Naibu waziri wa afya Dr Mollel anajibu hoja zilizotolewa na Katibu mkuu wa Baraza la maaskofu wa Kanisa Katoliki Padre Dr Charles Kitima.

Dr Mollel anasema utabibu siyo sawa na fani ya sheria kwa sababu katika utabibu Ukweli unapatikana Maabara na siyo kwingineko.

Karibu.

Dr Mollel anasema ni kawaida kwa kipindi cha November hadi March kila mwaka wagonjwa wenye matatizo ya kupumua, pumu na nimonia kuongezeka hata wananchi wakiangalia takwimu watagundua hilo.

Mollel anadai Dr Kitima ameongea kama mwanasheria ndio maana hoja zake zimejaa kasoro nyingi sana lakini yeye anajaribu kumuelimisha kama mwanasayansi.

Mollel anasema takwimu za Fr Kitima za vifo vya mapadre 25 na watawa 60 havina uthibitisho wa kisayansi kwamba vilitokana na Corona. Mollel anadai hata vifo vya mwaka jana vingi vilitokana na maradhi mengine kama vile magonjwa ya moyo na waathirika kuogopa kwenda hospitali wakihofia Corona.

Mwisho waziri Mollel amewataka wananchi waendelee kujifukiza kwani dawa kama mkaratusi ni tiba nzuri.

Dr Mollel ameulizwa maswali mengi lakini mengine ameyajibu kisayansi, mengine kisiasa na wengine kiblia.

Kwa mfano Dr Mollel amesema Mungu alipomuumba binadamu alimuwekea dawa zote ( mitishamba) katika bustanu ya Eden.
Na baadae akampa mwanadamu sayansi kwa ajili ya kuitawala dunia.

Source Star tv

Maendeleo hayana vyama
Pumbu
 
Kwa jinsi loyce nyanda (mtozi) alivyokua akimbana naibu waziri Kwa maswali,
nikajua muheshimiwa atakasirika na kumwambia "unajua unaongea na nani" alafu aache kipindi na kuondoka badala yake alikua ana punch maswali kisomi uku anaiba muda ili kipindi kiishe bila nyanda kujijua.

Hadi mwisho wa mchezo mtozi hakupata alichotaka kiende Kwa hadhira, anatazama saa yake dakika tisini za mchezo zimemalizike daktari 3 mtozi 0.
Game ilikua tamu sana
Swala siyo Mtozi bali je hoja za Fr Kitima zimejibiwa?

Au Fr Kitima alikuwa hana hoja?
 
Mwisho waziri Mollel amewataka wananchi waendelee kujifukiza kwani dawa kama mkaratusi ni tiba nzuri.
Yule aliyekuwa Waziri wa Afya nadhani alikuwa Mbunge wa Kigamboni akaondlewa uwaziri kwakuwa alikanusha kuwa kujivukiza hakujathibitika kisayansi kuwa kunatibu corona, huyu waziri wa leo anaikana sayansi
 
Ukweli ndiyo huo na itatuweka huru. Hongereni sana Kanisa Katoliki.

Hivi ni mjinga na mpumbavu gani hawezi kutofautisha Pneumonia ya kawaida na ya COVID 19?

Natafakari picha ya Mwanasesere a.k.a mdoli na binadamu mwenye akili.

So sad. Sad indeed.
 
Kamanda acha hizo, huyo ni kamanda mwenzetu kabisa ccm tumewaazimisha kwa muda kwa kuwa sisi chama chetu kimezorota 😂. Au umesahau kuwa alikuwa mmoja wa wapambanaji wetu mashuhuri?

Uliwahi kuona wapi akisifiwa? Huyo alikuja na mafuriko ya fisadi Lowassa.
 
Mollel anadai Dr Kitima ameongea kama mwanasheria ndio maana hoja zake zimejaa kasoro nyingi sana lakini yeye anajaribu kumuelimisha kama mwanasayansi.
Bogus doctors.

Sayansi ni kupima hao wanaokufa kujua ni nini kinawaua. Wamepima wakaona sio corona?
Mollel anasema takwimu za Fr Kitima za vifo vya mapadre 25 na watawa 60 havina uthibitisho wa kisayansi kwamba vilitokana na Corona.
Ni nani mwenye wajibu wa kupima, Fr Kitima, au serikali?

Serikali imekataa kutimiza wajibu wake kwa sababu wanazozijua wao, sasa kwa nini alaumu mtu asiyehusika kabisa?
Mwisho waziri Mollel amewataka wananchi waendelee kujifukiza kwani dawa kama mkaratusi ni tiba nzuri.
Utafiti wa hii (sayansi) ulifanyika lini, wapi na nani?

Ni mamlaka gani iliipitisha hiyo dawa kuwa inatibu huo ugonjwa. Hivi huyu anaelewe hata taratibu za kufanya utafiti kabla dawa haijathibitishwa kuwa inatibu ugonjwa?

Hawa jamaa sasa wamekuwa zaidi ya matapeli. WaTanzania inabidi tuwastukie kwa utapeli wao.
 
Back
Top Bottom