Naibu Waziri wa Afya, Dr. Mollel amjibu Fr. Kitima kuhusu Corona. Amkosoa na kumuelimisha maana ya UKWELI

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
82,745
139,520
Mjadala uko mubashara kupitia kipindi cha Ajenda kinachoongozwa na mtangazaji Aloyce Nyanda Star tv.

Naibu waziri wa afya Dr Mollel anajibu hoja zilizotolewa na Katibu mkuu wa Baraza la maaskofu wa Kanisa Katoliki Padre Dr Charles Kitima.

Dr Mollel anasema utabibu siyo sawa na fani ya sheria kwa sababu katika utabibu Ukweli unapatikana Maabara na siyo kwingineko.

Karibu.

=======

Dr Mollel anasema ni kawaida kwa kipindi cha November hadi March kila mwaka wagonjwa wenye matatizo ya kupumua, pumu na nimonia kuongezeka hata wananchi wakiangalia takwimu watagundua hilo.

Mollel anadai Dr Kitima ameongea kama mwanasheria ndio maana hoja zake zimejaa kasoro nyingi sana lakini yeye anajaribu kumuelimisha kama mwanasayansi.

Mollel anasema takwimu za Fr Kitima za vifo vya mapadre 25 na watawa 60 havina uthibitisho wa kisayansi kwamba vilitokana na Corona. Mollel anadai hata vifo vya mwaka jana vingi vilitokana na maradhi mengine kama vile magonjwa ya moyo na waathirika kuogopa kwenda hospitali wakihofia Corona.

Mwisho waziri Mollel amewataka wananchi waendelee kujifukiza kwani dawa kama mkaratusi ni tiba nzuri.

Dr Mollel ameulizwa maswali mengi lakini mengine ameyajibu kisayansi, mengine kisiasa na wengine kibiblia.

Kwa mfano Dr Mollel amesema Mungu alipomuumba binadamu alimuwekea dawa zote (mitishamba) katika bustani ya Eden na baadae akampa mwanadamu sayansi kwa ajili ya kuitawala dunia.

Chanzo: Star tv

Maendeleo hayana vyama
 
Mjadala uko mubashara kupitia kipindi cha Ajenda kinachoongozwa na mtangazaji Aloyce Nyanda Star tv.

Naibu waziri wa afya Dr Mollel anajibu hoja zilizotolewa na Katibu mkuu wa Baraza la maaskofu wa Kanisa Katoliki Padre Dr Charles Kitima.

Dr Mollel anasema utabibu siyo sawa na fani ya sheria kwa sababu katika utabibu Ukweli unapatikana Maabara na siyo kwingineko.

Karibu.

Updates;
Very uncalled for
 
Kumuuliza Mollel(sijaandika Dr. kwasababu wamekana taaluma zao) atoe takwimu za Covid ni sawa na kutafuta bikira kwenye wodi ya Wazazi waliojifungua bila operesheni.
😅😂😂🤣

Nimecheekaaaah daaah JF burudani!

Everyday is Saturday................................:cool:
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom