Naibu Waziri wa Afya, Dr. Mollel amjibu Fr. Kitima kuhusu Corona. Amkosoa na kumuelimisha maana ya UKWELI

Hii Wizara kweli imepatikana. Hao mabosi wawili ni burdan tosha kuwaangalia tu. Huhitaji kusikia wanachosema; bila shaka walishasahau taaluma zao siku nyingi. Na sasa inabidi wawe na tahadhari. Masuala ya corona ni nyeti sana. Yamezingirwa na landmines.
Hawa Madaktari wawili Dr Gwajima na Dr Mollel HAWAMFAI Rais SSH, kwa kuwa ni WANAFIKI wa hali ya juu. WAJIUDHURU
 
Hawa Madaktari wawili Dr Gwajima na Dr Mollel HAWAMFAI Rais SSH, kwa kuwa ni WANAFIKI wa hali ya juu. WAJIUDHURU
Hawawezi kujiuzulu kwa sababu ya njaa
IMG-20210518-WA0036.jpg
Screenshot_20210518-142559.jpg
 
Hii inaonyesha jinsi madaraka yakikutana na mtu asiesahihi yanaua
 
Mjadala uko mubashara kupitia kipindi cha Ajenda kinachoongozwa na mtangazaji Aloyce Nyanda Star tv.

Naibu waziri wa afya Dr Mollel anajibu hoja zilizotolewa na Katibu mkuu wa Baraza la maaskofu wa Kanisa Katoliki Padre Dr Charles Kitima.

Dr Mollel anasema utabibu siyo sawa na fani ya sheria kwa sababu katika utabibu Ukweli unapatikana Maabara na siyo kwingineko.

Karibu.

=======

Dr Mollel anasema ni kawaida kwa kipindi cha November hadi March kila mwaka wagonjwa wenye matatizo ya kupumua, pumu na nimonia kuongezeka hata wananchi wakiangalia takwimu watagundua hilo.

Mollel anadai Dr Kitima ameongea kama mwanasheria ndio maana hoja zake zimejaa kasoro nyingi sana lakini yeye anajaribu kumuelimisha kama mwanasayansi.

Mollel anasema takwimu za Fr Kitima za vifo vya mapadre 25 na watawa 60 havina uthibitisho wa kisayansi kwamba vilitokana na Corona. Mollel anadai hata vifo vya mwaka jana vingi vilitokana na maradhi mengine kama vile magonjwa ya moyo na waathirika kuogopa kwenda hospitali wakihofia Corona.

Mwisho waziri Mollel amewataka wananchi waendelee kujifukiza kwani dawa kama mkaratusi ni tiba nzuri.

Dr Mollel ameulizwa maswali mengi lakini mengine ameyajibu kisayansi, mengine kisiasa na wengine kibiblia.

Kwa mfano Dr Mollel amesema Mungu alipomuumba binadamu alimuwekea dawa zote (mitishamba) katika bustani ya Eden na baadae akampa mwanadamu sayansi kwa ajili ya kuitawala dunia.

Chanzo: Star tv

Maendeleo hayana vyama
Mualikeni Tena Mollel Star TV halafu mumuulize tena swali hilohilo muone majibu yake.
 
Hatukuwa na uchaguzi Oktoba 2020 ndiyo sababu wakapatikana viongozi mataahira wengi nchini. Wengi wao walizaliwa bila vichwa wakaishia kupachikwa vifuu vya nazi ili wafanane na binadamu wa kuchora. Mollel ni mfano hai, ndiyo maana akiambiwa nchini Tanzania jua linatokea magharibi na kuzama mashariki ataimba wimbo huo kwa juhudi zote ili asisahau bosi wake amemwamuru aseme nini. Dkt. Charles Kitima, Mungu akujalie utulivu na amani ya kweli itokayo kwa Baba yetu ailye juu, ukiwasamehe hao kwa kuwa hawajui wasemalo.
Hakika wewe ni nabii! Uliona mbali sana! Leo hii hawa hawa akina Mollel na kundi lake bila aibu wanatulazimisha tukachanje!
 
Back
Top Bottom