Nahitaji msaada wa haraka, hasira zitaniumbua mimi

Asante kaka . Nakupenda pia
 
Aisee, mnatakiwa mfanyie kazi anger management. Siku huzi kuna wataalamu wa kila fani. Pale MNH kuna wataalamu wazuri sana wa saikolojia na afya ya akili. Jaribuni kiwatembelea, wao wana njia nyingi za kufahamu shida iko wapi na jinsi ya kuwasaidia.
Dah...my ex kanitisha sana...
 
Dear...mbona nakuogopa ghafla??

Sasa si utanichakaza sura jamani?
 
ITAKUWA NI STRESS TU,KWANI UMEOLEWA? ILI TUANZE TIBA SASA
 
toa basi kaushauri kidogo kabla sijakutafuta naomba
Una matatizo ya kisaikolojia,kuna mambo ukiwa mdogo hayakwenda sawa,usiogope ni matatzo ya kawaida,wataalam wa tiba hii wapo wachache nchi yetu ila ungebahatika umpate jamaa mmoja hivi ni psychologist wa International School of Tanganyika,anawahudumia watoto wapale,yuko poa sana kuna dada mmoja alimuhudumia vizur sana,au nipe muda kuna kituo kimoja hivi ntawauliza maana wana deal na psychotherapy,kama unaweza kuuliza sehem yoyote wana deal na masuala ya Psycho therapy,
 
Chakwanza unapokasirika km ulikuwa umesisima basi kaa chini hasira zitapungua pombe sio suruhu ya hasira pole kwa hali hiyo dada
 
Mwanamke hata uwe na hasira vipi_ wewe endelea tu maake hauna madhara...hata ukirusha ngumi haina madhara....mm mwanamke hata akinichoma na kisu huwa siumii..
Ushauri wangu...wewe endelea tu na hasira zako maake hazina madhara_ungekuwa na madhara...hapo sawa.!
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] unaripuka kama bom. Unapiga mateke, na kunywa mbege.

Pole sana
 
Pole sana kwanza acha pombe dia mtoto wa kike na pombe sio vizuri .pili una marafiki wa kike aina gani? Jaribu kuwa na urafiki na watu ambao sio watumia pombe.

Pale unapokuwa moodless nenda kwa huyo rafiki na ukifika fanyeni vitu vya kukurudisha kwenye mood mnaweza kuangalia movie etc. Acha pombe dia . pole sana
 
Pole sana dada yangu, Mimi pekee ndo nina dawa ya hasira zako. Hata hivyo hatua ya kwanza kuwa karibu na Mungu kwa kusikiliza kwaya. Acha kuangalia tamthilia na Movie za kutisha, pendelea kuangalia Comedy na kusikiliza mziki wa Kufurahisha sio hii Miziki ya kuumizwa.

Tembelea marafiki, Achana na Pombe, na vileo vyote. Ukipata nafasi uwe unaenda kutembelea beach. Jitahidi kutojibizana na mtu. Jifunze kuwa Mvumilivu. Safiri kubadilisha mazingira. Kuwa mbali na watu wanaokutia hasira.

Uwe unanitumia PM nikupe ushauri nasaha zaidi.

Pole tena ndugu yangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…