saigilomagema
JF-Expert Member
- Jun 5, 2015
- 4,173
- 6,156
we ndio mzembe wenzako wametajirika na hayo madini we unakuja kubwabwaja huku matandaoni utapata faida gani. Nenda kachimbe wewe acha uzembe.Nsikuchoshe na Usinchoshe, tusichoshane.
Huwezi kuniambia niendelee kuusifu Uafrika wakati kuna mambo ya kutumia tu akili ndogo tumeshindwa kuyafanya.
Mfano.
Taifa la Tanzania ni moja ya nchi inayopatikana kwenye hili bara la Afrika (BARA LILILOJAA NEEMA).Moja ya Rasilimali tulizonazo kama Taifa ni pamoja na Madini (DHAHABU, ALMASI, TANZANITE, MAKAA YA MAWE n.k)
Shule zetu (Msingi & Sekondari) hadi leo hakuna mtaala unaohusu madini, namna ya kuyatunza na namna ya kuyachimba. Ajabu ni kwamba Nchi zisizo kuwa na Madini ndizo ambazo zinawapatia watoto wao elimu inayohusu madini kisha wanakuja kuyachimba, kuyaandaa na kuyasafirisha ili wakatajirike.
Watoto wetu wakimaliza shule hasa Form 4 na form 6 wanaingia kuwa machinga, kuendesha bajaji na Bodaboda huku wakiwa hawana kabisa ufahamu kuhusu rasilimali zao za madini waliyobarikiwa na Mungu.
Kwakuwa sisi ni washamba kwenye rasilimali zetu, ndiyo maana wakati fulani walitokea waafrika wajinga wakawa wanapasua chupa na kuzifunga vizuri na kuingia mjini kisha kuwahadaa waafrika wenzao kwamba zile zilikuwa ni Almasi na kiukweli wajinga wale walijipatia sana fedha miaka hiyo.
Madini tumebaki kuyatazama huko YouTube na kwenye television.
Pamoja na Madini kuwa ni mali yetu sisi Waafrika lakini wanaonufaika nayo ni watu weupe.
Wao wanachimba (Sisi hatuwezi kuchimba kwasababu kuna wajaa laana huwa wanasema hatuna mitambo,sasa sijafahamu hiyo mitambo inauzwaga kiasi gani cha fedha ambacho hatuna uwezo wa kununua)
Wao wanayafanyia processes (Sisi hatuwezi kufanya processes kwakuwa wajaa laana huwa wanasema hatuna mitambo,Hiyo mitambo inauzwaje kama Taifa tushindwe?)
Wao wanasafirisha (Hapa wajaa laana huwa wanasema tukifanya sisi tutakosa masoko, watazira!)
Haya ndiyo tuyafanyayo ngozi nyeusi.
Kazi tunazoweza ni kusomesha watoto na wakimaliza waingie mitaani kuwa wachuuzi wa bidhaa(Machinga) au kuendesha Boda na Bajaji halafu tuwaminye ki kweli kweli walipe kodi wakati huo huo huku kwenye Madini ambayo tumepewa Neema na Mungu Kodi inayokatwa haiendani na kile tulichonacho na wakati mwingine hao wachimbaji wanakwambia "HATUJAPATA FAIDA, HIVYO HATUWEZI KULIPA KODI".
Kama Ndivyo!?
Kwanini nikisema AFRIKA INA NEEMA ILA WAAFRIKA WANA LAANA mnachukia na kufuta nyuzi zangu?
Hayo niliyoyaainisha ni machache sana miongoni mwa meeeeengi mnooooo ambayo ngozi nyeusi inayafanya,sasa sijui mnataka nitumie lugha gani!.
NIPINGENI KWA HOJA, KWANINI NISISEME NGOZI NYEUSI INA LAANA?
NAHITAJI KUELEWESHWA ILI NIWE NA MTAZAMO CHANYA KUHUSU NGOZI NYEUSI.