Jitahidi kuchagua mti mzuri wa mbao unapokwenda kuchagua mbao za kupaulia nyumba Yako.
Sokoni zipo aina 3 common za mbao:-
1. Ukichagua mti WA MLINGOTI,
Jitahidi ununue ambazo hazijakauka Sana na saiti zisikae Sana bila kupauliwa, Huwa zinatabia ya kupinda zikipigwa jua.
Pia hazifai Kwa nyumba yenye Kuta dhaifu, inasababisha nyufa sababu ya paa kua zito Sana..
Uzuri wake: Zinahimili Sana mchwa Hata kama umenunua ambazo hazijatibiwa.
2. Ukichagua mti WA Cyprus,
Jitahidi upate ambazo zimetibiwa, hizi zinaliwa na mchwa Balaa.
Ikishindikana, zipakae oil chafu, inasaidia zidumu MDA mrefu.
Uzuri wa hizi
-hazipindi hovyo Hata zikipigwa na jua
-paa linakua jepesi, Hata kama Kuta ni dhaifu. (Zinafaa kwenye maghorofa,nyumba zenye misingi dhaifu, nyumba zilizojengwa kwenye udongo mfinyanzi)
3. Ukichagua mti wa msufi,
Jitahidi upate za msufi pori uliokomaa vzur, mbao changa inamung'unyika kama biskuti na Ni rahisi Sana kupekechwa na mchwa kuliko ata Cyprus.
Changamoto yake ni, hautaki maji, kitobo kimoja TU cha msumari unaovuja kinaweza sababisha mbao yote ikakatika katikati.
Hakikisha nyumba Yako haivuji Hata kitobo kimoja baada ya kupauliwa.
4. Ukipata mbao ya mnazi uliokomaa, vizuri utaenjoy, ni miaka buku, hamna mchwa wala kupinda.
5. Jitahidi usije kuuziwa mbao ya mwembe, hasa kama haujatibiwa.Utajuta.
Mti Bora sana Kwa kupaua Kama huna ela ya mawazo ni MVULE😊👍