Kusoma Masters tofauti na degree ni kupoteza muda.
Kuruhusiwa unaweza kabisa.
Ngoja Nikupe mifano miwili ya watu niwajuao.
1. Huyu Alisoma BAED with IT, kwahiyo aliajiriwa kama mwalimu Ila alipambana akahamishiwa bomani kuwa IT.
Akiwa bomani amesoma Dip ya IT na na mwaka huu ameomba ruhusa akasoma Bach. Ya IT.
Na taarifa chini ya kapeti ni kwamba barua yake imetoka, unasubiriwa muda muafaka wapewe barua zao waliomba. Na jina lake lipo..!!
2. Huyu Alisoma BAED, alipambana akaingia bomani, Ila yeye ndoto zake ni kuwa Muhasibu.
Hivi navyoandika hapa kamaliza semester ya kwanza open ya Accounts.
Kusoma masters tofauti na bachelor yako sio ushauri mzuri.
Hata waziri mkuu (Majaliwa) alishawahi kulisema hili.
Na alishauri watumishi wasome masters za bachelor zao.
Simshauri kabisaa asome masters isiyo ya bachelor yake Wala diploma.
Chakusoma ni hiyo Bach ya IT.
Na si lazima aende full time (huenda ana michongo yake, then akienda chuo itafeli), asome tu open.
Maana changamoto ya kwenda chuo mtumishi wa Umma, kama unategemea posho kutoka ofisini ina maana utazikosa zotee.
#YNWA