Nahitaji kubadilisha fani ya uwalimu

Sikia huu USHUHUDA labda UTAWEZA kukusaidia..

Niliajiriwa Idara x katika halmashauri z, nilikua na diploma.

Ila kiukweli Mimi nilipenda sanaa fani y.

Baada ya miaka 2 nika apply chuo course y na kuomba ruhusa ya masomo.

Nikaenda kusoma masomo ya fani y.

Nikaunga na masters kabisaa ya fani y.

Nilivyorudi kutoka masomoni nikahamishiwa bomani kutoka kijijini nilipokuwa naitumikia fani x, nikawa mfanyakazi wa Idara y bomani.

Nikakuta mkuu wa Idara y amepata shavu la kwenda kusoma phD ulaya, hivyo nikawa na kaimu huku jamaa ananifundisha kazi.

Nasubiri mwezi wa 7 kufanyiwa RECATEGORIZATION ili niwe mkuu wa Idara kamili wa y.

Then na wewe.....

Nenda chuo kasome bachelor ya IT then maliza.
peleka Cheti kwa utumishi wako subiri RECATEGORIZATION.

Huku unasubiri kubadilishiwa muundo.

Ukimaliza unaweza kuwa unatafuta Kazi kwengine kupitia ajira.go.tz au wizara ya utumishi huwa wanapost nafasi kibao za kufanyia Kazi UN na AU na kwengine huko (int. Org) kwa watumishi wa umma..

Chukua hatua....

Mimi nilichukua hatua, sikutaka ndoto zangu zife.

Sikuipenda Kazi x, umasikini wa nyumbani ulinifanya nikaisomee na kuajiriwa serikalini ili tu nitoke kwenye mikono ya kulelewa na ndugu.

Sikuacha ndoto zangu za kuwa y KUFA.


#YNWA
Mkuu ngoja nije PM nipate ujanja
 
Mkuu ngoja nije PM nipate ujanja
Ujue unanafasi nzuri kuhama Kwa kuwa Upo kwenye mfumo.

Kwa mfano. Ukitaka kuhamia anywhere lazima uwe na sifa. IT- uwe na bachelor of computer science au bachelor of ict.

Afisa mipango-mchumi..uwe na bachelor of economics
 
Nashukuru kwa kunikosoa ila hili ni zao la mbegu tuliyoipanda kwenye Elimu yetu na vyuo vyetu nimejitaidi kufikisha ujumbe kwenye jukwaa na nadhani wengine watanielewa
Big no. Hili Ni tatiy la kwako binafsi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom