Pole sana mkuu kwa changamoto unazopata kutoka kwa wadau.
Naomba nikutaarifu kuwa kwa ngazi uliyonayo sasa( degree) ndio ngazi kubwa ya elimu inayotambuliwa na serikali. Ni ngumu sana hata kupata ruhusa kwa mwajiri wako kwenda kuchukua degree nyingine. Yaani akupe ruhusa ya miaka mitatu au minne? Ni ngumu.! Ruhusa unayoweza kupata wew ni ruhusa ya miezi isiyozidi 18, yaan wakiamini unaenda kujiendeleza kwa ngazi ya masters! Ungekuwa umeajiriwa na diploma ungekuwa na nafasi hiyo

ila kwa degree hapana!
USHAURI
Achana na mawazo ya kubadili hiyo fani kwani ni ngumu kupata ruhusa.
Jambo la msingi pambana ukasome Masters yoyote inayorelate na mambo ya uongozi na zaidi na zaid... Wakati huo kama utaweza jiingize kwenye siasa ya chama tawala uuze CV yako na
ili uweze pata connection mbalimbali ikiwemo kuteuliwa kuwa afisa elimu wilaya au mkoa!
Kusoma Masters tofauti na degree ni kupoteza muda.
Kuruhusiwa unaweza kabisa.
Ngoja Nikupe mifano miwili ya watu niwajuao.
1. Huyu Alisoma BAED with IT, kwahiyo aliajiriwa kama mwalimu Ila alipambana akahamishiwa bomani kuwa IT.
Akiwa bomani amesoma Dip ya IT na na mwaka huu ameomba ruhusa akasoma Bach. Ya IT.
Na taarifa chini ya kapeti ni kwamba barua yake imetoka, unasubiriwa muda muafaka wapewe barua zao waliomba. Na jina lake lipo..!!
2. Huyu Alisoma BAED, alipambana akaingia bomani, Ila yeye ndoto zake ni kuwa Muhasibu.
Hivi navyoandika hapa kamaliza semester ya kwanza open ya Accounts.
Kusoma masters tofauti na bachelor yako sio ushauri mzuri.
Hata waziri mkuu (Majaliwa) alishawahi kulisema hili.
Na alishauri watumishi wasome masters za bachelor zao.
Simshauri kabisaa asome masters isiyo ya bachelor yake Wala diploma.
Chakusoma ni hiyo Bach ya IT.
Na si lazima aende full time (huenda ana michongo yake, then akienda chuo itafeli), asome tu open.
Maana changamoto ya kwenda chuo mtumishi wa Umma, kama unategemea posho kutoka ofisini ina maana utazikosa zotee.
#YNWA