Thelonious
JF-Expert Member
- Dec 11, 2017
- 218
- 452
(Niki)??Nkimpenda siwezi kuangalia mali za mtu....upendo wa kweli hauangalii pesa wala mali za mtu..mana hizo zinatafutwa na zipo tu
(Niki)??Nkimpenda siwezi kuangalia mali za mtu....upendo wa kweli hauangalii pesa wala mali za mtu..mana hizo zinatafutwa na zipo tu
Thank you Muchuna umri gani unalia lia ? hii serikali ya matamko ndio unasubiri ikuajiri ? utakua na mtindio wa ubongo,, halafu mbona kama unalalamika sana kama huyo mpenzi wako ndio kila kitu ? babu mkono mtupu haulambwi, mapenzi ya kuambiana nakupenda huku huwezi hata kumpa elfu tano ya kununua pedi nani akuvumilie ? move on, kama sio rizki atakuja mwingine alie bora kuliko huyo unaemlilia.... grow up man
PamojaAsante sana Mima
.....Vijana acheni kulia lia, be strong...wekeza nguvu zako kutafuta kazi badala ya kuwekeza kumfurahisha mtu ambaye kwa maelezo yako mwenyewe hakupendi kabisa, na wewe umeshajua.Asante sana japo ananivunja moyo sana ila mapenzi ya dhati ninayo kwake.
Asante sana.Bora kufa mara moja kuliko kufa mara laki yaani kila siku we utakuwa unakufa na kufufuka!jilipue tu mara moja muache huyo dem aende zake!mwanamke ukishampa attention sana atakutesa hutaona faida ya kupenda.mdogo wangu wanawake wapo wengi tuu jikaze mkatie mawasiliano mwanzo utaona mgumu lakini wazungu wanasema TIME HEALS EVERYTHNG.
hii trick nzuri sana, na usilazimishe kupata faraja kwa mtu asiyejali juhudi zakoDah hakuna kitu ninachokichukia kwenye mapenzi kama dharau hata mwanamke awe mzuri vipi akionesha kunidharau huwa sirembi ni kumpiga chini tu. Wewe jamaa kama unataka faraja ni kumuacha tu hiyo ndiyo faraja yako ingawa ni ngumu kumuacha, lakini jitahidi. Njia ya kumuacha bila yeye kukuchukia ni kumuacha kimya kimya, hakuna kumtafuta mpaka akutafute mwenyewe, akikutafuta ongea na kuchat nae vizuri tu akikuuliza baby mbona umebadilika siku hizi? Hiyo nafasi ndiyo utaitumia kumpa za uso!
Acha kulia Lia tafuta pesa wanawake wapo tu muache aolewa kwani wewe hutokuja kuoa ujue mahusiano yanatufanya vijana wengi tupoteze direction kwenye mambo ya msingi katika maisha badala yake unaanza waza upate pesa umfurahishe mwanamke hili halijaja kwa bahati mbaya achana Na huyu mwanamke jijenge kiuchumi....Napenda kutumia nafasi hii kuwashukuru wale wote ambao watashiriki kwa namna fulani ama nyingine kunisaidia ili niwe sawa kiakili na kimawazo nahisi huwenda nikiendelea hivi nitaingia kwenye matatizo hasa ya Kiafya.
Miaka ya nyuma kidogo nimekuwa ndani ya mahusiano na binti mmoja ambaye ametumia nafasi hiyo kuniumiza kila leo kwa kuniponda sana moyo wangu, Siwezi kumaliza wiki moja kabla sijaumizwa na makosa ambayo ninaona anafanya makusudi kwangu ili tu niumie na kila siku amekuwa mtu wa kushuhudia natokwa na machozi kwa ajili yake ila anatumia mwanya huo kuniponda kila leo, Nimejaribu kumweka sawa japo bado nipo kwenye utafutaji najua kesho na keshokutwa Mungu atanifungulia milango ya ajira ili niweze kuishi nae kama mke wangu ila pia hali yangu inachangia sana anione kama siwezi kupata ajira daima ila naamini katika Mungu yote yanawezakana.
Nimekuwa najitolea sehemu mbalimbali ila hata pale napopata kidogo najitahidi sana hata nusu apate yeye na nusu nipate mimi, ili tu ajue kwa namna gani ninahangaika kupata kazi ili baadae tuishi wote lakini juhudi zangu anaziona hazina maana kwake, Hivi karibuni nilipanga kwenda kumtembelea nilitamani sana ningepata walau chochote nipeleke kama zawadi lakini hali yangu ilikuwa mbaya sana na kushindwa kupata zawadi yoyote kwake, lakini aliniambia kama ungekuwa na pesa ningependa sana uniletee pete ya uchumba nikamwambia kama Mungu akipenda ajira nikapata basi yote yatawezekana kwa jina lake. Yote haya yanakuja kwa sababu baadhi ya marafiki zake wameolewa na wengine wamevishwa pete hivyo kwa hali yangu huwenda anaona kama ninamchelewesha sana, Ana tabia za kufuata na kutaka awe kama wao ila hali yangu haijakaa sawa mimi kuweza kumudu kile ambacho anakitaka.
Nimeshuhudia Sms kwenye simu yake akiwa anachat na wanaume na kuwaomba pesa kwakweli inaniuma sina la kufanya ila najua penzi langu halipo kwenye taswira nzuri hata kama ni uaminifu nimeanza kumshusha sana kutokana na yale ninayoyaona, najitahidi sana ila anaona juhudi zangu zote ni kupoteza muda. Kuna wakati inafikia hadi namdanganya kuwa mwezi ujao nitaajiriwa anafurahi wana na kuwa karibu namimi ila mwezi ukiisha ukaribu wake na mimi hupotea. Na sikupenda siku moja nipate ajira kisha niachane nae nahisi atanihisi vibaya na kuona kama nimemsaliti baada ya kupata ajira.
Usiku mwili wangu iligeuka kuwa tanuru la moto nimechomwa sana rohoni kwa sms nilizoona wakichat na Mtu nilikuwa naona kifo na macho ila najua ombi langu Mungu atalisikia, japo kazoea kila siku namwambia nitapata kazi ila najua muda si mrefu nitapata kazi hata kama ni kuzibua chemba ili tu nisije kudharaulika kwake.
Nahitaji sana faraja kwa kipindi hiki jamani hali yangu japo iko vibaya ila hili linanitia sana simanzi, nadharauliwa sana.
Mungu Simama nami.
Awwww! you've fallen deeply deeply in love.Nashukuru sana kwa nasaha zako, Ila najua milango itafunguka japo sikupenda ifunguke yeye akiwa nje nilitaka wote tuingie ndani.![]()
![]()
![]()
![]()
Huwa naona ni vigumu kufanya maamuzi hayo kwake maana hata kama nikiyafanya hawezi hata kuumia hata robo ya maumivu yangu, ninahisi kama nitajitesa sana kuliko sasa.
Yaaani Mungu amfanyie wepesi huyu ndugu yetu,.huyo mtu sio kabisaaamumu huyoo kwenye ubora wakee
Nataman Mungu angemfungua huyu kijana atambue kua huyo msichana sio kabsaaa
Daaaah! Sasa kama unajua fika kabisa kwamba mzani uko upande, kwa nn upate stress kiasi iko?, Anyway you never know!!Huwa naona ni vigumu kufanya maamuzi hayo kwake maana hata kama nikiyafanya hawezi hata kuumia hata robo ya maumivu yangu, ninahisi kama nitajitesa sana kuliko sasa.
AminaAsante sana mkuu ushauri wako ni msaada kwangu.