Nahitaji Faraja Moyo wangu Unateketea.

Nahitaji Faraja Moyo wangu Unateketea.

Hakuna mtu anayependa kuambiwa nakupenda huo upendo unatakiwa ujionyeshe wenyewe mzee.

"Eti nakupenda ila sina cha kukupa" huku anaona shoga zake wanapendeza wanatolewa out!

mzee utagongewa saana na atakudharau tu.

Wewe naona unajipa mizigo miwili wa kutafuta kazi na wa kumfikiria mtu mwingine.

Mwache tena mueleze mama sina kazi siwezi kukuhudumia na pia naona nakuchelewesha maisha wenzako wanaolewa naona nakupa wakati mgumu...hapo achague kusuka au kunyoa...
Najua hakuna mtu ambaye anaweza kijitosheleza kwenye maamuzi ila Mungu yupo kwenye kila upande.
 
Huyu jamaa matatizo hayo ni kama anajitakia tu maana dalili kuwa mwanamke huyo hafai zi wazi kabisa. Halafu sijui vichwa vyetu vikoje mpaka MTU awaze kwamba kuajiriwa ni muhimu kiasi hiki.
Asante
 
Ebwanaeeee kimbia mke wa kuishi naye sio huyo. Anakufanyia hivi bado wachumba, akiwa mkeo atafanya zaidi ya hapo, hata kama ukipata kazi akkupenda inamaana si wewe uliyemwoa bali ni hiyo kazi so siku kazi ikikosekana basi hatakuwa na mapenzi tena. Nakushauri nenda kijijini kwenu ukatafute mschana mzuri uoe. Take my advice nina miaka 9 kwe nye ndoa najua mke na ninajua mpigaji anafananaje
 
Ebwanaeeee kimbia mke wa kuishi naye sio huyo. Anakufanyia hivi bado wachumba, akiwa mkeo atafanya zaidi ya hapo, hata kama ukipata kazi akkupenda inamaana si wewe uliyemwoa bali ni hiyo kazi so siku kazi ikikosekana basi hatakuwa na mapenzi tena. Nakushauri nenda kijijini kwenu ukatafute mschana mzuri uoe. Take my advice nina miaka 9 kwe nye ndoa najua mke na ninajua mpigaji anafananaje
Asante sana kwa ushauri nitazingatia kuzuia haya maumivu
 
Asante sana Madam
Fanya mambo yako peke yako utapata mwanamke anaekupenda bila pesa na usimuamboe mambo yako mdanganye hata kua bado unasoma,huku ukifanya michakato yako,uone kama atakupenda ama la,,akikupenda basi jua huyo anafaa nawe utajiongeza
 
Maswahibu yanatukuta wengi Kwa namna tofauti.Nilivyoshinda na kuimaliza siku ya Jana Mungu anajua. Pole Mkuu,relax kama mie na usimweke kipaombele huyo binti.Hawa watu ni hatari.
 
Fanya mambo yako peke yako utapata mwanamke anaekupenda bila pesa na usimuamboe mambo yako mdanganye hata kua bado unasoma,huku ukifanya michakato yako,uone kama atakupenda ama la,,akikupenda basi jua huyo anafaa nawe utajiongeza
Asante sana kwa mara nyingine
 
Mkuu ni hivi;kwa uelewa wangu mdogo ni kwamba,hapo baadae ukija kupata ajira na hata kuwa milionea huyo mwanamke atakuvuruga tuu,na pengine atakutudisha nyuma saaana hutokaa uendelee mbele kwasababu ni MBINAFSI mwanamke uliye nae ana umimi na kujipenda mwenyewe yeye kwakwe pesa/mali vina thamani kuliko UTU. Hivyo kwaufupi huna mke wa kuoa hapo,.wakati huu wekeza nguvu na akili yako katika kujijenga kwanza kiuchumi,kiakili,kimwili na hata kiROHO,. Mke mwema yupo na atakuja kwa wakati wake wewe OMBA tena OMBA BILA KUKOMA,.MUNGU wetu sikio lake si zito mpaka asikusikie MAOMBI yako badili mtazamo wako kifikra,.

Mwisho:Maisha ni yako na kupanga ni kuchagua,.kama utachagua kuishi kwenye tanuri LA moto hiari yako,kama utapenda uishi kwa amani,upendo na furaha pia ni hiari yako vilevile..kuishi tunaishi Mara moja...thamini pumzi yako na jipende ww kwanza,.sisi tupo weeeeengi tena wengi haswaaa lakini kumpata mwema huna budi kukaa magotini pa MUNGU..nikutakie siku njema.

Mumu.
 
Asante sana japo ananivunja moyo sana ila mapenzi ya dhati ninayo kwake.
Inaonekana haukuwahi ku date na msichana mwengine kabla dah! Ilaaa mkuu chukua uamuzi ulio sawa kama umeweza kufuma txt wanazo chat na mtu mwengine vp kuhusu kugegedwa nje mkuu? Ni hivi mwanamke anayekupenda angefanya hata kwa siri sana ww usijue chochote ila mpaka umefuma txt na anavyoku force hivyo huyo hana mapenzi mkuu sasa ni ww na akili yako CHUKUA UAMUZI SASHIHI
 
Wanawake wengine ni hypobolical uncharactisible shortly ni watu wenye hallucination za ajab ajab huyo atazid kukuumiza kama mm nlvyoumizwa na mama swalehe weka chin tembea mbele hakuna mwanamke mmoja hapa dunian hafu ukipenda usipende saana chukulia ka mshikaji akikuzngua chiiin fasta vyuma vyenyewe vmekaza na moyo ukaze aaaah hapana mkuu !!!
 
Sikia kaka jipende nafsi yako kabla ya kumpenda yeye mchukulie ni MTU tu ambae ni MTU tu uliyekutana nae ukubwani.Kitendo cha kukaa muda mwingine unamfikilia yeye kitakurudisha nyuma utashindwa kufanya mambo yako ya maendeleo mambo mengi hapa duniani.

Muache aende akajifunze maisha wewe tafuta pesa.unaumia kwa sababu unamuweka akilini mtoe mawazoni kwako fight wewe ni mwanaume kesho atakuita baba huyo...chukua hii thamani yako ataiona itakavyokuwa nae mbali achana nae tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom