rafiki pole sana,lakini rafiki mapenzi ya pesa siyo,huyo hata ukipata kazi asiporidhika na kipato atakutesa tu,mapenzi ya kweli ni yale yasiyojali chochote.huyo achana naye,japo unampenda fanya maamuzi magumu.Napenda kutumia nafasi hii kuwashukuru wale wote ambao watashiriki kwa namna fulani ama nyingine kunisaidia ili niwe sawa kiakili na kimawazo nahisi huwenda nikiendelea hivi nitaingia kwenye matatizo hasa ya Kiafya.
Miaka ya nyuma kidogo nimekuwa ndani ya mahusiano na binti mmoja ambaye ametumia nafasi hiyo kuniumiza kila leo kwa kuniponda sana moyo wangu, Siwezi kumaliza wiki moja kabla sijaumizwa na makosa ambayo ninaona anafanya makusudi kwangu ili tu niumie na kila siku amekuwa mtu wa kushuhudia natokwa na machozi kwa ajili yake ila anatumia mwanya huo kuniponda kila leo, Nimejaribu kumweka sawa japo bado nipo kwenye utafutaji najua kesho na keshokutwa Mungu atanifungulia milango ya ajira ili niweze kuishi nae kama mke wangu ila pia hali yangu inachangia sana anione kama siwezi kupata ajira daima ila naamini katika Mungu yote yanawezakana.
Nimekuwa najitolea sehemu mbalimbali ila hata pale napopata kidogo najitahidi sana hata nusu apate yeye na nusu nipate mimi, ili tu ajue kwa namna gani ninahangaika kupata kazi ili baadae tuishi wote lakini juhudi zangu anaziona hazina maana kwake, Hivi karibuni nilipanga kwenda kumtembelea nilitamani sana ningepata walau chochote nipeleke kama zawadi lakini hali yangu ilikuwa mbaya sana na kushindwa kupata zawadi yoyote kwake, lakini aliniambia kama ungekuwa na pesa ningependa sana uniletee pete ya uchumba nikamwambia kama Mungu akipenda ajira nikapata basi yote yatawezekana kwa jina lake. Yote haya yanakuja kwa sababu baadhi ya marafiki zake wameolewa na wengine wamevishwa pete hivyo kwa hali yangu huwenda anaona kama ninamchelewesha sana, Ana tabia za kufuata na kutaka awe kama wao ila hali yangu haijakaa sawa mimi kuweza kumudu kile ambacho anakitaka.
Nimeshuhudia Sms kwenye simu yake akiwa anachat na wanaume na kuwaomba pesa kwakweli inaniuma sina la kufanya ila najua penzi langu halipo kwenye taswira nzuri hata kama ni uaminifu nimeanza kumshusha sana kutokana na yale ninayoyaona, najitahidi sana ila anaona juhudi zangu zote ni kupoteza muda. Kuna wakati inafikia hadi namdanganya kuwa mwezi ujao nitaajiriwa anafurahi wana na kuwa karibu namimi ila mwezi ukiisha ukaribu wake na mimi hupotea. Na sikupenda siku moja nipate ajira kisha niachane nae nahisi atanihisi vibaya na kuona kama nimemsaliti baada ya kupata ajira.
Usiku mwili wangu iligeuka kuwa tanuru la moto nimechomwa sana rohoni kwa sms nilizoona wakichat na Mtu nilikuwa naona kifo na macho ila najua ombi langu Mungu atalisikia, japo kazoea kila siku namwambia nitapata kazi ila najua muda si mrefu nitapata kazi hata kama ni kuzibua chemba ili tu nisije kudharaulika kwake.
Nahitaji sana faraja kwa kipindi hiki jamani hali yangu japo iko vibaya ila hili linanitia sana simanzi, nadharauliwa sana.
Mungu Simama nami.
Ni Kwel mkuu lakini pia nakukumbusha tuu wanawake hawaridhikagi hata kidogo ..unaweza ukawa una muhudumia vizur lakini bado wahuni wakawa wanakugongea .yan hawa viumbe inatubidi tutumie akili sana kuishi naoHakuna mtu anayependa kuambiwa nakupenda huo upendo unatakiwa ujionyeshe wenyewe mzee.
"Eti nakupenda ila sina cha kukupa" huku anaona shoga zake wanapendeza wanatolewa out!
mzee utagongewa saana na atakudharau tu.
Wewe naona unajipa mizigo miwili wa kutafuta kazi na wa kumfikiria mtu mwingine.
Mwache tena mueleze mama sina kazi siwezi kukuhudumia na pia naona nakuchelewesha maisha wenzako wanaolewa naona nakupa wakati mgumu...hapo achague kusuka au kunyoa...
una umri gani unalia lia ? hii serikali ya matamko ndio unasubiri ikuajiri ? utakua na mtindio wa ubongo,, halafu mbona kama unalalamika sana kama huyo mpenzi wako ndio kila kitu ? babu mkono mtupu haulambwi, mapenzi ya kuambiana nakupenda huku huwezi hata kumpa elfu tano ya kununua pedi nani akuvumilie ? move on, kama sio rizki atakuja mwingine alie bora kuliko huyo unaemlilia.... kale kamsemo ka mwanaume mashine ndio kanakupa kiburi, pochi nayo ina nafasi yake.......
mumu huyoo kwenye ubora wakeeMkuu ni hivi;kwa uelewa wangu mdogo ni kwamba,hapo baadae ukija kupata ajira na hata kuwa milionea huyo mwanamke atakuvuruga tuu,na pengine atakutudisha nyuma saaana hutokaa uendelee mbele kwasababu ni MBINAFSI mwanamke uliye nae ana umimi na kujipenda mwenyewe yeye kwakwe pesa/mali vina thamani kuliko UTU. Hivyo kwaufupi huna mke wa kuoa hapo,.wakati huu wekeza nguvu na akili yako katika kujijenga kwanza kiuchumi,kiakili,kimwili na hata kiROHO,. Mke mwema yupo na atakuja kwa wakati wake wewe OMBA tena OMBA BILA KUKOMA,.MUNGU wetu sikio lake si zito mpaka asikusikie MAOMBI yako badili mtazamo wako kifikra,.
Mwisho:Maisha ni yako na kupanga ni kuchagua,.kama utachagua kuishi kwenye tanuri LA moto hiari yako,kama utapenda uishi kwa amani,upendo na furaha pia ni hiari yako vilevile..kuishi tunaishi Mara moja...thamini pumzi yako na jipende ww kwanza,.sisi tupo weeeeengi tena wengi haswaaa lakini kumpata mwema huna budi kukaa magotini pa MUNGU..nikutakie siku njema.
Mumu.
Wewe utaweza kuwa na Me asiye na kitu na je upo naye kwasasa?mumu huyoo kwenye ubora wakee
Nataman Mungu angemfungua huyu kijana atambue kua huyo msichana sio kabsaaa
Asante sana mkuu ushauri wako ni msaada kwangu.Mkuu ni hivi;kwa uelewa wangu mdogo ni kwamba,hapo baadae ukija kupata ajira na hata kuwa milionea huyo mwanamke atakuvuruga tuu,na pengine atakutudisha nyuma saaana hutokaa uendelee mbele kwasababu ni MBINAFSI mwanamke uliye nae ana umimi na kujipenda mwenyewe yeye kwakwe pesa/mali vina thamani kuliko UTU. Hivyo kwaufupi huna mke wa kuoa hapo,.wakati huu wekeza nguvu na akili yako katika kujijenga kwanza kiuchumi,kiakili,kimwili na hata kiROHO,. Mke mwema yupo na atakuja kwa wakati wake wewe OMBA tena OMBA BILA KUKOMA,.MUNGU wetu sikio lake si zito mpaka asikusikie MAOMBI yako badili mtazamo wako kifikra,.
Mwisho:Maisha ni yako na kupanga ni kuchagua,.kama utachagua kuishi kwenye tanuri LA moto hiari yako,kama utapenda uishi kwa amani,upendo na furaha pia ni hiari yako vilevile..kuishi tunaishi Mara moja...thamini pumzi yako na jipende ww kwanza,.sisi tupo weeeeengi tena wengi haswaaa lakini kumpata mwema huna budi kukaa magotini pa MUNGU..nikutakie siku njema.
Mumu.
Asante sana mkuuUnazingua mhengaaaa maisha yenyewe mafupi haya tupa chini hicho kiumbe kihadhifina
Nkimpenda siwezi kuangalia mali za mtu....upendo wa kweli hauangalii pesa wala mali za mtu..mana hizo zinatafutwa na zipo tuWewe utaweza kuwa na Me asiye na kitu na je upo naye kwasasa?
Ni wa tatu kwangu kwenye mahusianoInaonekana haukuwahi ku date na msichana mwengine kabla dah! Ilaaa mkuu chukua uamuzi ulio sawa kama umeweza kufuma txt wanazo chat na mtu mwengine vp kuhusu kugegedwa nje mkuu? Ni hivi mwanamke anayekupenda angefanya hata kwa siri sana ww usijue chochote ila mpaka umefuma txt na anavyoku force hivyo huyo hana mapenzi mkuu sasa ni ww na akili yako CHUKUA UAMUZI SASHIHI
Sawa kaka nimeelewaWanawake wengine ni hypobolical uncharactisible shortly ni watu wenye hallucination za ajab ajab huyo atazid kukuumiza kama mm nlvyoumizwa na mama swalehe weka chin tembea mbele hakuna mwanamke mmoja hapa dunian hafu ukipenda usipende saana chukulia ka mshikaji akikuzngua chiiin fasta vyuma vyenyewe vmekaza na moyo ukaze aaaah hapana mkuu !!!
Asante sana MimaSikia kaka jipende nafsi yako kabla ya kumpenda yeye mchukulie ni MTU tu ambae ni MTU tu uliyekutana nae ukubwani.Kitendo cha kukaa muda mwingine unamfikilia yeye kitakurudisha nyuma utashindwa kufanya mambo yako ya maendeleo mambo mengi hapa duniani.
Muache aende akajifunze maisha wewe tafuta pesa.unaumia kwa sababu unamuweka akilini mtoe mawazoni kwako fight wewe ni mwanaume kesho atakuita baba huyo...chukua hii thamani yako ataiona itakavyokuwa nae mbali achana nae tu.
Asante kwa mchango mdau nazidi kupanua fikra zanguPole sana kaka...ila nikwambie tu ya kuwa kwa huyo hata ukipata ajira ataona wanaume wengine wanalipwa vizuri zaidi yako hivyo ataendelea kukudharau...kama hujaoa ni bora kupiga chini mapema ...ndani ya ndoa hakunaga kujaribu
Asante sana mkuurafiki pole sana,lakini rafiki mapenzi ya pesa siyo,huyo hata ukipata kazi asiporidhika na kipato atakutesa tu,mapenzi ya kweli ni yale yasiyojali chochote.huyo achana naye,japo unampenda fanya maamuzi magumu.