Napenda kutumia nafasi hii kuwashukuru wale wote ambao watashiriki kwa namna fulani ama nyingine kunisaidia ili niwe sawa kiakili na kimawazo nahisi huwenda nikiendelea hivi nitaingia kwenye matatizo hasa ya Kiafya.
Miaka ya nyuma kidogo nimekuwa ndani ya mahusiano na binti mmoja ambaye ametumia nafasi hiyo kuniumiza kila leo kwa kuniponda sana moyo wangu, Siwezi kumaliza wiki moja kabla sijaumizwa na makosa ambayo ninaona anafanya makusudi kwangu ili tu niumie na kila siku amekuwa mtu wa kushuhudia natokwa na machozi kwa ajili yake ila anatumia mwanya huo kuniponda kila leo, Nimejaribu kumweka sawa japo bado nipo kwenye utafutaji najua kesho na keshokutwa Mungu atanifungulia milango ya ajira ili niweze kuishi nae kama mke wangu ila pia hali yangu inachangia sana anione kama siwezi kupata ajira daima ila naamini katika Mungu yote yanawezakana.
Nimekuwa najitolea sehemu mbalimbali ila hata pale napopata kidogo najitahidi sana hata nusu apate yeye na nusu nipate mimi, ili tu ajue kwa namna gani ninahangaika kupata kazi ili baadae tuishi wote lakini juhudi zangu anaziona hazina maana kwake, Hivi karibuni nilipanga kwenda kumtembelea nilitamani sana ningepata walau chochote nipeleke kama zawadi lakini hali yangu ilikuwa mbaya sana na kushindwa kupata zawadi yoyote kwake, lakini aliniambia kama ungekuwa na pesa ningependa sana uniletee pete ya uchumba nikamwambia kama Mungu akipenda ajira nikapata basi yote yatawezekana kwa jina lake. Yote haya yanakuja kwa sababu baadhi ya marafiki zake wameolewa na wengine wamevishwa pete hivyo kwa hali yangu huwenda anaona kama ninamchelewesha sana, Ana tabia za kufuata na kutaka awe kama wao ila hali yangu haijakaa sawa mimi kuweza kumudu kile ambacho anakitaka.
Nimeshuhudia Sms kwenye simu yake akiwa anachat na wanaume na kuwaomba pesa kwakweli inaniuma sina la kufanya ila najua penzi langu halipo kwenye taswira nzuri hata kama ni uaminifu nimeanza kumshusha sana kutokana na yale ninayoyaona, najitahidi sana ila anaona juhudi zangu zote ni kupoteza muda. Kuna wakati inafikia hadi namdanganya kuwa mwezi ujao nitaajiriwa anafurahi wana na kuwa karibu namimi ila mwezi ukiisha ukaribu wake na mimi hupotea. Na sikupenda siku moja nipate ajira kisha niachane nae nahisi atanihisi vibaya na kuona kama nimemsaliti baada ya kupata ajira.
Usiku mwili wangu iligeuka kuwa tanuru la moto nimechomwa sana rohoni kwa sms nilizoona wakichat na Mtu nilikuwa naona kifo na macho ila najua ombi langu Mungu atalisikia, japo kazoea kila siku namwambia nitapata kazi ila najua muda si mrefu nitapata kazi hata kama ni kuzibua chemba ili tu nisije kudharaulika kwake.
Nahitaji sana faraja kwa kipindi hiki jamani hali yangu japo iko vibaya ila hili linanitia sana simanzi, nadharauliwa sana.
Mungu Simama nami.