Kuna maana zaidi ya moja neno sihr limetumika ndani ya Qur'an? Kama ipo na ni njema haihusiani na uchawi na kiini macho utakuwa umemaliza kunielewesha. Kama hakuna itakuwa vigumu sana kubadilisha maana kusudiwa na ijulikanayo na itakuwia ugumu kunielewesha.
Kuna maneno ambayo nafahamu yanatokana na root word " shr" kama vile (suhur) ikimaanisha daku au "sahr" kukesha, lakini hayo yote hayabadilishi maana ya neno "sihr" kuwa ni uchawi. No pun intended.
Auntie Faiza, sikiliza kile ninachosema; mimi ninaunga mkono kauli ya Mungu (swt) ndani ya Qur'an kuhusu maana ya neno "sihr" lilivyotumika, mimi sipingi aslan.
Ila lazima uuangalie muktadha mzima wa habari, neno "sihr" limetumika ndani ya Qur'an kwa maana hiyo uliyoisema na ndiyo maana kama hii iliyofafanuliwa na kamusi la "Aqrab":-
The noun سحر means anything the source of which is not quite visible; showing off FALSEHOOD in the form of truth; a crafty device; craftness;mischief; enchantment.
Katika kamusi la Lane iko hivi:-
----- it also means producing what is false in the form of TRUTH; any event of which the cause is hidden and which is imagined ti be different from what it really is; embellishment by falsification and deceit.
Sasa tuache "Sihr" inayozungumzwa na Qur'an, na hapa ninazungumzia matumizi ya "sihr" kwa manufaa ya binadamu "in positive sense" ambapo tunapata katika maana hii iliyopo hapo juu kwenye Lane:-
"Any event of which the cause is hidden and which is imagined to be different from what it really is"
👆🏻katika hali hiyo mtu anaweza kwa matumizi mazuri ya hiyo "phenomenon" kutengeneza kitu cha manufaa kwa watu, nikatoa mfano, phenomenon hiyo inaweza kutumika kama "War strategy" vitani, yaani unatengeneza "sihr" kumpumbaza adui asikuone nk,
Maana yangu ndiyo hiyo na si vinginevyo, na hapa nilitaka watu wajue matumizi mazuri ya "sihr" (the good use of sihr).
Nitakupa mfano, katika miaka ya 1800, ni mtu gani ungeweza kumuambia atumie kinyesi cha binadamu, (ambacho kwa mafundisho ya dini kinaitwa NAJISI), kwa ajili ya manufaa yake angalikubali??!!😁😁, lakini leo kinyesi hicho watu tunakitumia kwa ajili ya kuzalisha BIOGAS na mbolea hasa huko china, na tomato likitoka hapo wewe Antie Faiza ukiunga mchuzi wake ni balaa!!😁😁.
Hayo ndiyo matumizi mazuri ya akili zetu na elimu aliyotujalia Allah, na hapo ndiyo maana ya positivity na sio Negativity ile inayozungumzwa na Qur'an kuhusu "sihr".
Lugha ya kiswahili ni finyu kulinganisha na kiarabu au kiingereza, Maneno, Magic,Black magic, sorcery, witchcraft, voodoo juju,juggling nk, yote hayo Kwa kiswahili tunatumia neno moja tu UCHAWI, uwe wa tunguli na kuwanga, kusambira nk, wote huo waswahili tunaita UCHAWI no distinction !!?