Nahitaji busara za Mshana jr na Faizafoxy

Wakuu huu ni uzi maalumu kwa hawa wakongwe wawili ambao nimekuwa nikifatilia maandiko yao.ni

Mshana Jr na FaizaFoxy.

Leo naomba wanishauri katika mambo yafuatayo na watoe maneno yao ambayo yanawafanya wawe ni watu wenye kuheshimiwa.

Naomba ushauri kwenye mambo haya hapa.

1.jee naweza kuachana na siasa nikafanya mambo yangu yakaenda pasi na kuwa na chama chochote yaani nikaachana na siasa moja kwa moja?
Je inawezekana kwa tanzania ya leo?

2. Je kuna uwezekano wa mtu mchawi kujigeuza paka au mbwa au kitu kingine mbali na binadamu?
Je upo uwezekano huo?

3.je inawezekana kwangu kumuacha mwanamke kwa sababu ya ujeuri wake na kutokuwa na maelewano mazuri na mama yangu mzazi?

Wakubwa zangu wawili nahitaji busara zenu kwa upana kabisa mdadavue. Huu uzi ni kwa ajili yenu.

Heshima kwenu wakuu.

Nimepitia majibu ya maswali yako mpaka ya wale uliowachagua kukujibu pamoja majibu yao yangekuwa elimu pia kwa wasomaji lakini bado kunaukakasi ktk majibu,

Swali la kwanza majibu ni rahisi kama kumsukuma mlevi halina haja ya kupoteza muda

Sawali la 2,
Binaadamu kujigeuza paka kimaumbile nijambo haliwezekani hata kiuchawi, uwezo wa kiumbe kujibadili ktk maumbile ya kiumbe mwingine ,Mungu kawapa viumbe wawili tu, nao ni Malaika na majini,na ktk eneo hili pia wapo viumbe wengine wamepewa uwezo wa kujibadili rangi kufuatana na mazingira yalivyo na wengine hujibadili mistari ya rangi zao kuvutia mawindo.

Bali uwezo wa binaadam kujificha mbele ya macho ya watu na kuwakilishwa na viumbe wengine kama paka fisi simba na mbwa kiuchawi uwezo huo anao, pia anauwezo wa kufuga na kutumia viumbe wengine kama mamba, fisi na majini kama nyenzo ktk shughuli za kiuchawi, hata wakati mwingine huwaficha binaadamu wenzao mbele ya macho ya watu na badala yake wakaweka gogo au mgomba au chochote watakacho, na nyie mkakiona kile walichokiweka pale kama muwili wa ndugu yenu mkanza kulia na kutangaza amekufa, nawawo wakamchukua binaadamu huyo na kumuweka msukule,(mafichoni)
kwa ujumla hayo yote hufanyawa KICHAWI.

Swali la 3
Inawezekana kabisa kwanza daraja la mama ni kubwa sana kwako kuliko daraja la mke, pia mkeo aweje vyovyote vile hawezi kuwa na huruma au wema kwako zaidi ya mama yako. Pia kuna angalizo kubwa sana juu ya mama zetu, pale mtume Mohammad(s.a.w) aliposema pepo ya kila mmoja wenu iko chini ya nyayo za mama zenu, yaani pamoja na matendo mema yote ya kumpendeza Mungu kama hutokuwa mtiifu namwema kwa mama yako hutoingia peponi( ktk ufalme wa Mungu)
ila sasa ujeuri huwo wa mkeo uwe ndani ya misingi ya kisheria, sio mkeo anakataa kushirikiana na mama yako ktk masuala ya kichawi au masala ya kumkufuru Mungu, eti aonekane mkeo huyo ni jeuri hana mahusiano mema na mama, laahasha hiyo haina mashiko.

NB :- Uchawi na ushirikina ni vitu viwili tofauti,
 
Mtanzania jembe la mkono shingo angani inanauma kushuhudia mkusanyiko mawingu ya mvua. Wanangu mbegu zitachipua.Baba Airbus hiyo hiyo!
 
Mkuu mtoe huyo mbibi hana level za mshana jr
 
Pitia hii ukipata muda, kwa upande wangu naona ipo highly informative kuhusu "sihr"...

Huyu Muhubiri yupo sahihi katika kuelezea maana ya Sihr, kanukuu aya zinazozungumzia tukio la Nabii Musa (as) na wachawi wa Firauni, pia kanukuu aya inayozungumza juu Nabii suleiman (as) na wale mashetani waliofundisha sihr, kifupi anasema jinsi mimi ninavyoamini kwamba sihr ni viini macho, mazingaombwe, kufanya uongo uonekane kuwa ni ukweli.

Hivyo sihr (uchawi) hauwezi kubadilisha kitu kimoja kiwe kitu kingine kidhahiri, mfano uchawi hauwezi kumbadilisha mtu akawa sokwe kidhahiri ila uchawi unaweza kudanganya macho ya watu yakamuona mtu amebadilika kuwa sokwe katika kipindi fulani tu.

Watu wengi huwa wanashangaa inakuaje uchawi unaweza kudanganya macho kwa namna hiyo, wanahoji "mechanism" yake ipo vipi??!!, kifupi ni kwamba hiyo ni miongoni mwa elimu ambayo watu hujifunza kama jinsi watu wanavyojifunza elimu zingine na wakafuzu.

MSINGI WA "SIHR".

Tunajua kwamba si kila kitu macho ya binadamu yanaweza kuona au hata kusikia, ili macho yetu yaone yanahitaji kwanza nishati ya nuru iwepo nishati hiyo imo ndani ya uzio (spectrum) ya mawimbi (430 hadi 770×10^12 HZ) yaani (430----770 THZ), mawimbi ya Electromagnetic yaliyo ndani ya huo uzio ndiyo nishati ya nuru (visible light) inayotusaidia kuona, mawimbi ya Electomagnet yakiwa nje ya huo uzio hapo macho yetu kamwe hayawezi kuona hayo mawimbi, mfano X rays, Gama rays,Infrared, ultraviolet nk.

Katika hiyo spectrum ambamo ndimo nuru ipo,hiyo nuru ukiichambua utapata rangi 7 na kila moja inayo mawimbi yake tofauti na mwenzake na ni kutokana na huo utofauti wa mawimbi ndipo tunaweza tukatofautisha baina ya rangi mbalimbali katika mazingira yetu, kuanzia rangi za msingi; Violet, Indigo, ----Red, na michanganyiko ya rangi hizo.

Sasa tumepata msingi utekelezaji wa Sihr (uchawi), NI UTAALAMU WA KUCHEZA NA MAWIMBI YA NURU ILI KULETA ATHARI ILE AMBAYO MCHAWI ANAIKUSUDIA.

Elimu hiyo ya kucheza na mawimbi ili kuleta athari za Sihr ni lazima mtu ajifunze au afundishwe kwani kuna mambo kadha yanahusika ili mtu awe master katika hiyo elimu kama jinsi mtu anavyojifunza fani zingine za kawaida.
 
Na ndiyo uchawi ulivyo. Uchawi siyo "creation" ni "illusion" na kuna "aspect" nyingine ya ilm ambayo pia umeigusia lakini umeigusia kama nayo pia ni "illusion" ambako sipingi kwa upande huo lakini pia kuna ukweli mwengine wa "NURU" ambao ni "energy".

Nuru pia ni "energy" ambayo inaweza kuwa "transformed physically". Ndiyo tukienda ndani kidogo tunapata vitu kama ilm iliyotajwa kwenye kisa cha Suleiman na pia Khidhr.

Ukiwasoma wanazuoni wa Sufi utaona wanakubali kuwa upo uwezekano wa kuwepo "physically" (not mere illussions) sehemu moja lakini ukaonekana kwengine. Au hata uwezo wa "shape shifting" ku "transform shapes".

Hapa kuna ilm pana na "deeper" na si ya ku "ruleout" kiwepesi wepesi kuikataa upande mmoja kwa kuwa tu haiingii akilini mwako na kukubali upande mwengine kwa kuwa tu inaingia akilini mwako.

Kuna ilm ya roho (ruh au spirits) ambayo wachache sana wamebahatika kupewa tena kwa uchache sana ambayo nnaamini hata hao wachache waliopewa hata wakiielezea na kuifundisha kwa mtu ambae hajapewa basi hatoifahamu, kwa kuwa tu hajapewa.

Katika ilm hii ya roho jee kuna uwezekano wa mtu kuitoa roho au yake au ya mwengine kwenye kiwiliwili kimoja na kuiingiza kwenye kiwiliwili kingine amma cha binaadam au hata cha chui (for the sake ya uzi na swali namba mbili) na kukitumia kiwiliwili kile kwa matakwa yake? Binafsi nasema upo uwezekano huo.

Hakika "sihr" ni kiza.
 
Auntie Faiza, you are a polymath, Mashallah.

Walau tunakubali kuwa "Sihr" ni giza, lakini mimi hapo nitafafanua kidogo kwamba "Sihr" kama elimu inayofuata nidhamu, inayo manufaa kwa binadamu tukizingatia kuwa "in operation" inahusiana na macho (vision), na tunaambiwa na wanasayansi kuwa macho yetu ni sehemu ya Ubongo iliyojitokeza kwa nje hivyo "Sihr" inaweza kutumika kutibu aina fulani ya magonjwa ya akili ikitumika pale inapostahili, kifupi SIO sihr zote ni kwa ajili ya "giza" (wickedness), jambo hilo linataka kufanana na matumizi ya KISU, ambapo kinaweza kutumika kudhuru mtu au kinaweza kutumika kukatia kitunguu, nyanya, nyama nk.

Ni utafiti tu unatakiwa ufanyike kuhusu matumizi bora ya "Sihr".

Kuna mambo umeyaongea ambayo hayakuwa kwenye mada ya "Sihr", kidogo naomba niyagusie japo elimu yangu ni finyu na hapo uniwie radhi kwani mwenye elimu ni Mungu pekee.

Katika aya yako No 2, umesema kwamba --"Energy can be transformed into physical (body, matter??)", hapa sipingi ila ninachoweza kusema hadi sasa hakuna jambo kama hilo limewahi kufanywa na mwanadamu, lakini "its vice verse" tayari inafanyika katika "fission nuclear reaction" (E=mc²).

Katika aya yako No 3,unasema wanazuoni wa Kisufi wanaamini uwezekano wa kuwepo/kuonekana kwa mtu "physically" (if I got you right). Naam, jambo hilo ni KWELI, lakini under certain conditions, na hasavni pale mtu unapokuwa katika deep meditation kitu ambacho wanazuoni wa kisufi walikuwa wana practice kwa sana ambapo hisia za mtu zinahama kabisa katika dunia hii na anakuwa katika hali ya "Irhamu" (aina moja ya revelation), katika hali hiyo mtu anaweza kuona vitu au watu ambao asingeweza kuwaona katika hali ya kawaida (in conscious mind). Katika Qur'an hali hiyo inaitwa "nyuma ya pazia".

Katika aya yako No 5, unasema juu ya uwezekano wa mtu kuitoa roho yake au ya mwingine na kuiweka katika kiwiliwili ama cha binadamu au chui, Hii imani ni potofu na kamwe haijapata na haitapata KUTOKEA to the end of the World, na hii siyo imani ya kiislamu na haina support from either the Qur'an or the Hadith.

Hindus (Mabaniani) wanaamini kwamba mtu akifa na kama alikuwa mtu mwema basi roho yake inahamia kwenye kiunbe mwingine mpole yaani anapozaliwa kiumbe nwingine mpole, mfano kobe roho ya huyo mtu huwa imo ndani ya huyo kobe kadhalika mtu akiwa mbaya hapa duniani na akafa wanaamini kwamba roho yake itahamia ndani ya kiumbe mbaya kama chui, fisi nk, yaani atazaliwa chui au Fisi nk, ambamo ndani yake roho ya huyo mtu itakuwemo, hiyo inaitwa "REINCANATION".(spelling??).
 
Mie siamini kabisa kabisa kama kuna binaadamu yeyote kwa njia ya aina yeyote iwe ya sayansi au ya kichawi anaweza kuelewa elimu ya roho.
Masala ya elimu ya Roho ni tata sana na dadisi mno toka kwa binaadam wa awali, ndio maana Mtume(s.a.w) aliulizwa na waliokuwa wakimzunga wakati ule Mtume alikosa jibu, ndipo jibu likaja ktk Qur'an sura 17:85
"Wanakuuliza juu ya roho, sema roho ni ktk mambo ya bwana wangu, na nyie hamkupewa elemu( juu ya mambo) ila kidogo tu,
Kwa hiyo hapo ni dhahiri shahiri Allah hakutupa elimu ya roho, nakama tungekuwa elimu ya roho kisayansi au kichawi tungeikarabati kama tunvyo karabati moyo mafigo n.k. pia tungeweza kuizuwia wakati inapochomoka kwa mpenzi wako.
 
Hahahaha nimefurahi kusikia na mimi nina impact fulani katika jamii.

Ahsante.
Binafsi napenda michango yako Sana ukianzisha thread lazima niisome tatizo huwa una mwisho mbaya lakini 65% uko sahihi
Kama sio ukada wa ccm ni mtu unajitambua Sana siku ukijiweka kando na u ccm ukajawa na uzalendo huenda unaweza kuanzisha taasisi ya ushauri na utapata wateja wengi.
Pia acha kuwa na hasira sio kila kitu utake kikufurahishe.
 
Auntie Faiza, you are a polymath, Mashallah.

Walau tunakubali kuwa "Sihr" ni giza, lakini mimi hapo nitafafanua kidogo kwamba "Sihr" kama elimu inayofuata nidhamu, inayo manufaa kwa binadamu tukizingatia kuwa "in operation" inahusiana na macho (vision), na tunaambiwa na wanasayansi kuwa macho yetu ni sehemu ya Ubongo iliyojitokeza kwa nje hivyo "Sihr" inaweza kutumika kutibu aina fulani ya magonjwa ya akili ikitumika pale inapostahili, kifupi SIO sihr zote ni kwa ajili ya "giza" (wickedness), jambo hilo linataka kufanana na matumizi ya KISU, ambapo kinaweza kutumika kudhuru mtu au kinaweza kutumika kukatia kitunguu, nyanya, nyama nk.

Ni utafiti tu unatakiwa ufanyike kuhusu matumizi bora ya "Sihr".

Kuna mambo umeyaongea ambayo hayakuwa kwenye mada ya "Sihr", kidogo naomba niyagusie japo elimu yangu ni finyu na hapo uniwie radhi kwani mwenye elimu ni Mungu pekee.

Katika aya yako No 2, umesema kwamba --"Energy can be transformed into physical (body, matter??)", hapa sipingi ila ninachoweza kusema hadi sasa hakuna jambo kama hilo limewahi kufanywa na mwanadamu, lakini "its vice verse" tayari inafanyika katika "fission nuclear reaction" (E=mc²).

Katika aya yako No 3,unasema wanazuoni wa Kisufi wanaamini uwezekano wa kuwepo/kuonekana kwa mtu "physically" (if I got you right). Naam, jambo hilo ni KWELI, lakini under certain conditions, na hasavni pale mtu unapokuwa katika deep meditation kitu ambacho wanazuoni wa kisufi walikuwa wana practice kwa sana ambapo hisia za mtu zinahama kabisa katika dunia hii na anakuwa katika hali ya "Irhamu" (aina moja ya revelation), katika hali hiyo mtu anaweza kuona vitu au watu ambao asingeweza kuwaona katika hali ya kawaida (in conscious mind). Katika Qur'an hali hiyo inaitwa "nyuma ya pazia".

Katika aya yako No 5, unasema juu ya uwezekano wa mtu kuitoa roho yake au ya mwingine na kuiweka katika kiwiliwili ama cha binadamu au chui, Hii imani ni potofu na kamwe haijapata na haitapata KUTOKEA to the end of the World, na hii siyo imani ya kiislamu na haina support from either the Qur'an or the Hadith.

Hindus (Mabaniani) wanaamini kwamba mtu akifa na kama alikuwa mtu mwema basi roho yake inahamia kwenye kiunbe mwingine mpole yaani anapozaliwa kiumbe nwingine mpole, mfano kobe roho ya huyo mtu huwa imo ndani ya huyo kobe kadhalika mtu akiwa mbaya hapa duniani na akafa wanaamini kwamba roho yake itahamia ndani ya kiumbe mbaya kama chui, fisi nk, yaani atazaliwa chui au Fisi nk, ambamo ndani yake roho ya huyo mtu itakuwemo, hiyo inaitwa "REINCANATION".(spelling??).
Nilipoongelea ilm ruh sikumaanisha "reincarnation" ambayo kwa uhakika ni dhana potofu.

Nilipoongelea ilm ruh pia sikumaanisha uumbaji (creation) Bali ni uhai ambao "existing".

Ningependa kama ulinielewa hivyo basi ondoa shaka. Mimi naweza kuongelea "incarnation" ambayo dalili zake zipo wazi ndani ya Qur'an...

Qur'an 2:28
How can you disbelieve in Allah when you were lifeless and He brought you to life; then He will cause you to die, then He will bring you [back] to life, and then to Him you will be returned.

Hiyo ni "incarnation" na siyo "reincarnation" kama sintofahamu iliyojitokeza.

Amma kuhusu ilm ruh na uchache wake pia nilikusudia kama ilivyo dalil ya Qur'an...

Quran 17:85
And they ask you, [O Muhammad], about the soul. Say, "The soul is of the affair of my Lord. And mankind have not been given of knowledge except a little."

Kama uonavyo katika aya hiyo kuwa kuna wachache na kwa uchache waliopewa ilm ya roho.

Kwanza nigependa hayo yaeleweke ili tuondoe utata wowote kama upo.
 
Mie siamini kabisa kabisa kama kuna binaadamu yeyote kwa njia ya aina yeyote iwe ya sayansi au ya kichawi anaweza kuelewa elimu ya roho.
Masala ya elimu ya Roho ni tata sana na dadisi mno toka kwa binaadam wa awali, ndio maana Mtume(s.a.w) aliulizwa na waliokuwa wakimzunga wakati ule Mtume alikosa jibu, ndipo jibu likaja ktk Qur'an sura 17:85
"Wanakuuliza juu ya roho, sema roho ni ktk mambo ya bwana wangu, na nyie hamkupewa elemu( juu ya mambo) ila kidogo tu,
Kwa hiyo hapo ni dhahiri shahiri Allah hakutupa elimu ya roho, nakama tungekuwa elimu ya roho kisayansi au kichawi tungeikarabati kama tunvyo karabati moyo mafigo n.k. pia tungeweza kuizuwia wakati inapochomoka kwa mpenzi wako.
Nadhani aya hiyo ya 17:85 ukiisoma vizuri utaona "ila kidogo tu".

Kidogo nini iliyokusudiwa kwenye hiyo aya? Mimi nasema ni "ilm ruh", wapo wachache na kwa uchache waliojaaliwa ilm hiyo.
 
Kwa hiyo. Bwana mokaze kuna uchawi ukiutumia vizuri hakuna tatizo?

Back
Top Bottom