Nahitaji busara za Mshana jr na Faizafoxy

Nahitaji busara za Mshana jr na Faizafoxy

Kwa hiyo. Bwana mokaze kuna uchawi ukiutumia vizuri hakuna tatizo?
Hakuna. Ikishakuwa uchawi basi hauwezi kutumika kwa uzuri.

Nililiona hilo kutoka kwa Mokaze lakini nilikuwa kwanza naondosha dhanna ya yale mtu asiyoyaelewa akaona kuwa hayawezekani kwa kukumbusha kisa cha Khidhr. Ingawa sijakielezea lakini ni kisa maaruf cha Mussa na Khidhr.

Pia nilikumbusha Suleiman kwa kuwa kisa chake na Malkia na kiti chake kilivyoletwa mbele ya Suleiman nacho ni maaruf.

Visa hivyo vyote vinahusiana na ilm ya ziyada ambayo si ya uchawi.
 
Hahahaha nimefurahi kusikia na mimi nina impact fulani katika jamii.

Ahsante.

Pamoja na utofauti wa kisiasa wewe ni CCM, ndio lumumba pekee mwenye hoja hata kwenye uzi wa hovyo komment yako lazima iwe na maana

Ccm wote mngekua kama mama yetu huyu nchi ingekua mbali sana.
 
Kwa hiyo. Bwana mokaze kuna uchawi ukiutumia vizuri hakuna tatizo?

Kama umenielewa nilichoandika sidhani kama ungeuliza hilo swali, na kama ungalijua definition ya uchawi "sihr" nadhani usinge uliza hilo swali kabisa.
 
Sijakuelewa ulichoandika ndiyo maana nikauliza kwa kufupisha ili nielewe zaidi.

Mtu ili aelewe vyema anaweza akauliza juu ya mada fulanisasa unapokuwa hutaki kujibu kwa kujiaminisha labda mada yako imejitosheleza huo hauwi uungwana.

Labda niulize tena

Uchawi ukitumika vizuri inakuwa hamna neno?
Kama umenielewa nilichoandika sidhani kama ungeuliza hilo swali, na kama ungalijua definition ya uchawi "sihr" nadhani usinge uliza hilo swali kabisa.
 
Nadhani aya hiyo ya 17:85 ukiisoma vizuri utaona "ila kidogo tu".

Kidogo nini iliyokusudiwa kwenye hiyo aya? Mimi nasema ni "ilm ruh", wapo wachache na kwa uchache waliojaaliwa ilm hiyo.

HAPANA
Kinacho nifurahisha kwako ni juhudi yako ya kufuatili maandiko ya quran Alhamdullilah, ninacho kuomba tafuta tafsiri ya SHEKH IBUN KATHIRI tafsiri hii inasherehe pana na imeweka kilasababu ya kwanini aya fulani ilishuka kwa kila tokeo lake maalum hii itakusaidia sana kufahamu Quran zipo za kingereza pia lakini kama ungefahamu kiarabu ungefaidi mno
Tukienda kwenye tukio aya hii ilishushwa wakati kundi la mayahudi walipo weka bunge wakijadili huyu Muhammad (s.a.w)anatuambia roho itaadhibiwa itakuaje? Hebu tuwendeni tukamuulize. Walipofika wakamuuliza " Hebu tuambie namna gani roho yaweza kuadhibiwa na imo ndani ya mwili na hiyo roho inatokana na Allah na wala roho haijashushiwa chochote( maamrisho) na haitokuwa na chochote cha uovu.
Mtume( s.a.w) alinyamaza kimya.akisubiri majibu kutoka kwa Allah ndipo punde akashuruka Malaika Jibril akaja na jibu "wanakuuliza juu ya roho sema roho ni miongoni wa mambo ya bwana wangu. (yaani roho ni miongoni mwa illmu ya Allah) na nyinyi hamkupewa ilmu ila kidogo( yaani milango yenu ya ufahamu na uwezo wenu wa maarifa niliokupeni ni mdogo hauwezi ukabeba au kuelewa ilmu ya roho someni na mtekeleze hiyo ilmu ndogo miongoni mwa ilmu zangu nilio kushushieni ktk taurati muepukane na adhabu.
HII NDIO MAANA YA " HAMKUPEWA ILMU ILA CHACHE
that so the understanding capacity of human begin can't bear the physical knowledge of soul,
is like just a kindergarten want to know the laws of motion.
 
Dogo umeingia cha kike. Katika watu wasio na busara humu anaongoza Mshana Jr na kufuatiliwa kwa karibu sana na shemeji yake FAIZAFOXY
 
Nilipoongelea ilm ruh sikumaanisha "reincarnation" ambayo kwa uhakika ni dhana potofu.

Nilipoongelea ilm ruh pia sikumaanisha uumbaji (creation) Bali ni uhai ambao "existing".

Ningependa kama ulinielewa hivyo basi ondoa shaka. Mimi naweza kuongelea "incarnation" ambayo dalili zake zipo wazi ndani ya Qur'an...

Qur'an 2:28
How can you disbelieve in Allah when you were lifeless and He brought you to life; then He will cause you to die, then He will bring you [back] to life, and then to Him you will be returned.

Hiyo ni "incarnation" na siyo "reincarnation" kama sintofahamu iliyojitokeza.

Amma kuhusu ilm ruh na uchache wake pia nilikusudia kama ilivyo dalil ya Qur'an...

Quran 17:85
And they ask you, [O Muhammad], about the soul. Say, "The soul is of the affair of my Lord. And mankind have not been given of knowledge except a little."

Kama uonavyo katika aya hiyo kuwa kuna wachache na kwa uchache waliopewa ilm ya roho.

Kwanza nigependa hayo yaeleweke ili tuondoe utata wowote kama upo.

Mkuu, Faiza. Samahani Cm iliishiwa moto.

Yakupasa ukumbuke kauli yako pale uliposema;-

" katika ilm ya roho jee kuna uwezekano wa mtu kuitoa roho au yeye au ya mwingine kwenye kiwiliwili kimoja na kuingiza kwenye kiwiliwili kingine amma cha binadamu au hata cha chui (for the sake of uzi na swali namba mbili) na kukitumia kiwiliwili kile kwa matakwa yake?. Binafsi nasema upo uwezekano huo""

👆🏻Hiyo ni kauli yako, mimi ninasema haikuwezekana,haiwezekani na haitawezekana na kama inawezekana lete mfano hai ili uthibitishe madai yako.

Umenukuu aya ya Qur'an (2:28) kutetea hoja yako hiyo, nadhani hujaitafakari vizuri hiyo aya, aya inataja matukio manne ya maisha ya mwanadamu, inaanza:-

1) lifeless, 2) brought to life, 3) cause to die, 4) Brought back to life.

Ufafanuzi:- 1) Life less ni hali kabla mtu hajaumbwa, 2) brought to life ni pale ambapo mtu kisha umbwa kama mimi na wewe sasa hivi.3) Cause to die ni kwamba baadaye tutakufa, 4) brought back to life ni kwamba baada ya kufa tutafufuliwa siku ya kiyama. Ndiyo maana ya hiyo aya na wala siyo hiyo dhana ya "incarnation".

Umetoa aya nyingine (17:85) kuzungumzia juu ya ilm ya roho, katika hii aya nimeona watu wengi sana wakikosea katika kuifahamu, aya inasema hivi

" Na wanakuuliza kuhusu roho sema: Roho ni katika mambo ya mola wangu. Nanyi hamkupewa katika elimu ila kidogo tu."

Angalia hayo maneno-""------ Nanyi hamkupewa katika elimu ila kidogo", neno "Nanyi" linasimama badala ya wale waliomuuliza mtume mtukufu (saw) kuhusu elimu ya roho ndipo Allah anamwambia mtume (saw) awaambie hao kwamba elimu yao juu ya roho ni ndogo na hawanabudi kumfuata mtume (saw) ili awafundishe elimu ya roho iliyokuwa KUBWA zaidi.

Katika manabii wote ni mtukufuvmtume (saw) ndiye aliyekuwa na elimu kubwa kabisa ya roho.

Soma,somatena na rudia kusoma hiyo aya na tafakari inshallah utaona huu ukweli ninao kueleza.
 
Ilmu ya roho ni ipi kwa mujibu wa ufafanuzi eako mkuu?

Mkuu, Faiza. Samahani Cm iliishiwa moto.

Yakupasa ukumbuke kauli yako pale uliposema;-

" katika ilm ya roho jee kuna uwezekano wa mtu kuitoa roho au yeye au ya mwingine kwenye kiwiliwili kimoja na kuingiza kwenye kiwiliwili kingine amma cha binadamu au hata cha chui (for the sake of uzi na swali namba mbili) na kukitumia kiwiliwili kile kwa matakwa yake?. Binafsi nasema upo uwezekano huo""

Hiyo ni kauli yako, mimi ninasema haikuwezekana,haiwezekani na haitawezekana na kama inawezekana lete mfano hai ili uthibitishe madai yako.

Umenukuu aya ya Qur'an kutetea hoja yako hiyo, nadhani hujaitafakari vizuri hiyo aya, aya inataja matukio manne ya maisha ya mwanadamu, inaanza:-

1) lifeless, 2) brought to life, 3) cause to die, 4) Brought back to life.

Ufafanuzi:- 1) Life less ni hali kabla mtu hajaumbwa, 2) brought to life ni pale ambapo mtu kisha umbwa kama mimi na wewe sasa hivi.3) Cause to die ni kwamba baadaye tutakufa, 4) brought back to life ni kwamba baada ya kufa tutafufuliwa siku ya kiyama. Ndiyo maana ya hiyo aya na wala siyo hiyo dhana ya "incarnation".

Umetoa aya nyingine (17:85) kuzungumzia juu ya ilm ya roho, katika hii aya nimeona watu wengi sana wakikosea katika kuifahamu, aya inasema hivi

" Na wanakuuliza kuhusu roho sema: Roho ni katika mambo ya mola wangu. Nanyi hamkupewa katika elimu ila kidogo tu."

Angalia hayo maneno-""------ Nanyi hamkupewa katika elimu ila kidogo", neno "Nanyi" linasimama badala ya wale waliomuuliza mtume mtukufu (saw) kuhusu elimu ya roho ndipo Allah anamwambia mtume (saw) awaambie hao kwamba elimu yao juu ya roho ni ndogo na hawanabudi kumfuata mtume (saw) ili awafundishe elimu ya roho iliyokuwa KUBWA zaidi.

Katika manabii wote ni mtukufuvmtume (saw) ndiye aliyekuwa na elimu kubwa kabisa ya roho.

Soma,somatena na rudia kusoma hiyo aya na tafakari inshallah utaona huu ukweli ninao kueleza.
 
Kwa hiyo. Bwana mokaze kuna uchawi ukiutumia vizuri hakuna tatizo?

Mkuu Safuha,ningependa uelewe hivi, chochote tulichoumbiwa wanadamu kinayofaida na ipo aya ya Qur'an kuthibitisha hilo (sikumbuki ipo sura gani) .

Ni matumizi ya mwanadamu ndiyo hufanya kitu kikawa kibaya au kizuri, mfano kusema uongo ni dhambi, lakini anapokuja jambazi kwako na akakuuliza mahali ulipoweka fedha je utamuambia ukweli au uongo ela zilipo ?? na wakati ulikuwa unayo nafasi ya kumdanganya ili asichukue ela!!, na hivyo hivyo "sihr" kama itatumika kwa njia ya manufaa hiyo siyo dhambi na ndiyo maana nikasema utafiti ufanywe ili kuona faida ya "sihr" kwa watu, mfano sihr inaweza kutumika kama "Warfare strategy" dhidi ya maadui- kuwapoteza maadui nk,

Katika Qur'an Sihr inatajwa kwa ubaya sababu ni kwamba wale watu kama mfano, wachawi wa Musa (as) walitumia uchawi kupinga haki na hayo ndiyo matumizi mabaya ya "elimu ya Sihr" na elimu hiyo ikitumika katika njia hiyo elimu yote inakuwa haina maana.

Kumbuka kuna sihr na elimu ya kutengeneza sihr.

Mifano mingine ya kukufanya uelewe somo; nguvu za nyuklia zinaweza kutumika kwa ajili ya mabomu hapo hapo zinaweza kutumika kuzalishia umeme, Gongo inaweza kutumika kunywa hapohapo inaweza kutumika kama nishati (fuel), Cocaine inatumika kwa kubuia lakini inapotumika katika prescribed dosage itamsaidia kichaa kama dawa na Bangi ni hivyo hivyo--- kwa msingi huo ni matumizi ndiyo focus ya ubaya au uzuri wa kitu.

Mfano wa mwisho,Nguruwe analiwa hapohapo Viungo vya nguruwe vimethibitika kuwa na nafasi kubwa kabisa kuwa viungo mbadala ya viungo vya binadamu-- katika wanyama wote ni Nguruwe pekee ndiyo mwenye nafasi hiyo, Macho, mafigo, maini nk vinayo nafasi kubwa "to be transplanted" kwa binadamu.

Sasa mkuu, unapoangalia negative side of a matter do not forget also kuangalia its positive side.
 
1.kamuulize mtoto wa mkulima
2.Kaangalie movie za harry porter
3.maombi na visomo yatafyekelea mbali matatizo yote.
 
Ilmu ya roho ni ipi kwa mujibu wa ufafanuzi eako mkuu?

Vipi mkuu, Safuha unaniuliza swali lilelile aliloulizwa mtukufu mtume (saw), na wale makafiri juu ya Roho, Soul, الروح.!!!!

و يسألنك عن الروح ----

"Wa yas'alunaka a'ni ruuh qul rruh min amri rabbi---"

Roho ipo chini ya amri ya Mola wake, na kama ipo chini ya amri ya mola wake je, ni nani mwingine aliyekuwa "closest to Allah??", ni yeye mtume (saw) kuliko mtu yeyote na ni yeye ndiye anayo elimu kubwa ya ROHO kuliko mwanadamu yeyote na elimu hiyo kupewa na mola wake, na wale makafiri waliomuuliza walikuwa na elimu ya Roho kidogo sana, kwa maana hiyo walitakiwa wamfuate , wampokee mtume (saw) ili wapate elimu kubwa ya ROHO. Ni nani kama Nabii Muhammad (saw)-- in that matter??!!
 
Mkuu Safuha,ningependa uelewe hivi, chochote tulichoumbiwa wanadamu kinayofaida na ipo aya ya Qur'an kuthibitisha hilo (sikumbuki ipo sura gani) .

Ni matumizi ya mwanadamu ndiyo hufanya kitu kikawa kibaya au kizuri, mfano kusema uongo ni dhambi, lakini anapokuja jambazi kwako na akakuuliza mahali ulipoweka fedha je utamuambia ukweli au uongo ela zilipo ?? na wakati ulikuwa unayo nafasi ya kumdanganya ili asichukue ela!!, na hivyo hivyo "sihr" kama itatumika kwa njia ya manufaa hiyo siyo dhambi na ndiyo maana nikasema utafiti ufanywe ili kuona faida ya "sihr" kwa watu, mfano sihr inaweza kutumika kama "Warfare strategy" dhidi ya maadui- kuwapoteza maadui nk,

Katika Qur'an Sihr inatajwa kwa ubaya sababu ni kwamba wale watu kama mfano, wachawi wa Musa (as) walitumia uchawi kupinga haki na hayo ndiyo matumizi mabaya ya "elimu ya Sihr" na elimu hiyo ikitumika katika njia hiyo elimu yote inakuwa haina maana.

Kumbuka kuna sihr na elimu ya kutengeneza sihr.

Mifano mingine ya kukufanya uelewe somo; nguvu za nyuklia zinaweza kutumika kwa ajili ya mabomu hapo hapo zinaweza kutumika kuzalishia umeme, Gongo inaweza kutumika kunywa hapohapo inaweza kutumika kama nishati (fuel), Cocaine inatumika kwa kubuia lakini inapotumika katika prescribed dosage itamsaidia kichaa kama dawa na Bangi ni hivyo hivyo--- kwa msingi huo ni matumizi ndiyo focus ya ubaya au uzuri wa kitu.

Mfano wa mwisho,Nguruwe analiwa hapohapo Viungo vya nguruwe vimethibitika kuwa na nafasi kubwa kabisa kuwa viungo mbadala ya viungo vya binadamu-- katika wanyama wote ni Nguruwe pekee ndiyo mwenye nafasi hiyo, Macho, mafigo, maini nk vinayo nafasi kubwa "to be transplanted" kwa binadamu.

Sasa mkuu, unapoangalia negative side of a matter do not forget also kuangalia its positive side.
Sihr haina positive side.

Nitarudi.
 
Unasubili nini nyangau ww umepona mbavu? Au nimuite Tena?
Naona mwezi umeandama mapema.. Nilitaraji ukichaa wako utakurudi mwakani mwezi wa pili... Kunywa dozi mapema kabla hatujakurudisha Lutindi
 
Back
Top Bottom