Nahisi nimetapeliwa sijui nifanye nini?

Nahisi nimetapeliwa sijui nifanye nini?

[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] darasa la saba mzigo, hyo ya kupigiwa simu nakuulizwa kiasi hata Mimi huwa napigiwa nawasikiliza wewe nacheka mwishoni au nawahoji maswali wanakata simu
Hawakutukanagi kweli?, Maana jamaa wanamatusi wale.

Walishawahi kumpigia Mamkwe, Akawastukia wakaishia kutukanana tu
 
Juzi hapa nimepigwa 26,000/ eti naungiwa kifurushi unlimited data, calls na sms cha mwaka mzima halotel!
Nilijua naibiwa ila akili ilihamia kwenye benefits, nikawa najiona ninavyostream Netflix kwa mwaka bureeee!
Mwizi wangu alizima simu yake siku kama 3 tu ila sasa hv ipo hewani tu anadunda!
 
Hawakutukanagi kweli?, Maana jamaa wanamatusi wale.

Walishawahi kumpigia Mamkwe, Akawastukia wakaishia kutukanana tu

Kutukanana?

Hivi unapotezaje muda wako kwa hao wajinga!!
 
Bora uache.

Watakuambia irudishe. Utarudisha ilo kopo lenye Android yenye skin ya iOS watakuambia sio iyo tunataka iPhone yetu.

Itakulazimu kulipa iPhone 11 tena.
Na wao si watapaswa kuthibitisha kuwa kweli waliuza iphone? hiyo watachomoaje?
 
Kuna hawa Juzi wamemliza mdogo wangu wa kike anasoma UDOM, anadai alitoka ATM hapo town, akatokea mwanamke mtu mzima, akamuongelesha kama anayetaka msaada, baada walikuja jamaa wengine wawili. Anadai baada ya muda alijikuta hana simu na mkoba wake wamechukua na hajui hata nini kimetokea.
Bahati mbaya wakaenda ATM wakakomba boom lililobaki maana alikuwa na kadi ya bima kwenye mkoba na password yake alikuwa anatumia mwaka wa kuzaliwa. Alipoenda kutoa taarifa polisi kwa ajili ya lost report , polisi wenyewe wanasema hizi kesi zimekuwa nyingi sana siku hizi hapo DODOMA.
 
Shida ni ulikua na hela mfukoni (cash) kwa hyo zilikua zinakupa mawenge.Pole🤣🤣🤣
 
Kuna hawa Juzi wamemliza mdogo wangu wa kike anasoma UDOM, anadai alitoka ATM hapo town, akatokea mwanamke mtu mzima, akamuongelesha kama anayetaka msaada, baada walikuja jamaa wengine wawili. Anadai baada ya muda alijikuta hana simu na mkoba wake wamechukua na hajui hata nini kimetokea.
Bahati mbaya wakaenda ATM wakakomba boom lililobaki maana alikuwa na kadi ya bima kwenye mkoba na password yake alikuwa anatumia mwaka wa kuzaliwa. Alipoenda kutoa taarifa polisi kwa ajili ya lost report , polisi wenyewe wanasema hizi kesi zimekuwa nyingi sana siku hizi hapo DODOMA.
Wezi wa dar wameamia Makao makuu ya nchi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asanteni sana wanajukwaa kwa pole pamoja na ushauri wenu,Leo nimeweza kurudishiwa 82% ya hela yangu yaani 410,000.Bora nusu hasara kuliko hasara kamili.
Umefanya fanyaje mpaka wamekurudishia?
 
Hapa hakuna kesi. Mnunuzi anasema aliikagua akaridhika na bei akapanga yeye sasa wauzaji wanakosa gani? Ndiyo maana huwa wanasema kagua mali kabla hujaondoka

Sent from my GT-I9300 using JamiiForums mobile app
Kuna vitu vya kiufundi, ina maana twende na mafundi simu dukani kukagua kwa kuifungua kabisa? Eh! Wale wa biashara halali, utaona bidhaa zao zikibuma, huwa wanaruhusu wateja kuzirudisha kwa matengenezo ama kubadilisha. Tumeona haya kwenye kampuni za magari, simu, jokofu n.k. Sasa wewe leo unauza bidhaa X, inakwenda kubadilika kuwa Y, na bado unakomaa. Hivi hata hiyo biashara itadumu kweli?
 
Yaani kwa kujua hilo niliwaambia hata kwa namna yoyote ile asije mtu akakwambia sijui bonyeza namba flani kwenye simu usikubali.Nikawaambia na namba ni 100 tu zingine ni utapeli.
Tena niliwaasa kama kunatakiwa marekebisho yoyote msifanye chochote mpaka mnitaarifu.
Ila ajabu hata moja hakukumbuka. Kapigiwa simu kwenye namba za miamala baadae wakamwambia kuna marekebisho ya mtandao tunafanya kwa mawakala,wakaomba na namba yake kawapa.
Wakampigia kwa namba yake huku wanamwamuru abonyeze anachoelekezwa kwenye namba ya wakala.Yaan watu ni wa tigo wakampitisha tigopesa kawatumia wakaja voda napo kawatumia halotel katuma mpaka kumaliza hela damn!
Mbona umeoa mwanamke Bogas mkuu?

Sent from my SM-G9550 using JamiiForums mobile app
 
Sasa ule ni mnada siyo duka mkuu. Na mara nyingi wanadishaji wa aina ile huwa hawana mahali pakudumu. Dukani bei utakuta zimepangwa wakati mdani wateja ndiyo hupanga hizo kama mtoa mada anavyosema alipanga yeye baada ya kuridhika na bidhaa
Kuna vitu vya kiufundi, ina maana twende na mafundi simu dukani kukagua kwa kuifungua kabisa? Eh! Wale wa biashara halali, utaona bidhaa zao zikibuma, huwa wanaruhusu wateja kuzirudisha kwa matengenezo ama kubadilisha. Tumeona haya kwenye kampuni za magari, simu, jokofu n.k. Sasa wewe leo unauza bidhaa X, inakwenda kubadilika kuwa Y, na bado unakomaa. Hivi hata hiyo biashara itadumu kweli?
 
Sasa ule ni mnada siyo duka mkuu. Na mara nyingi wanadishaji wa aina ile huwa hawana mahali pakudumu. Dukani bei utakuta zimepangwa wakati mdani wateja ndiyo hupanga hizo kama mtoa mada anavyosema alipanga yeye baada ya kuridhika na bidhaa
Hata mnada unaongozwa kwa sheria. Uhalifu utabaki kuwa uhalifu. Halafu hatuzungumzii changamoto zinazojitokeza katika kutafuta haki bali tunatafuta ni kivipi mtu huyu atapata haki yake. Maelezo unayotoa, ni kama vile mauzo ya mnadani hayaongozwi na sheria za nchi na wauzaji wake wanaweza kufanya uhalifu na wasiguswe. Sidhani kama ni sahihi.
 
Back
Top Bottom