Nahisi huyu Mtengeneza Matukio na Msahaulishaji Matukio katika Vichwa vya Watanzania analipwa Mshahara mkubwa sana

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
Popote alipo huyu Mtu ajue kuwa Krav Maga namkubali na Mimi pia natamani Siku moja niwe kama Yeye.

Huyu Mtu Yeye Kazi yake ni Kusoma Kwanza upepo wa Watanzania hasa Kifikra kisha anaanza Kucheza na Akili zetu.

Ana uwezo wa Kutengeneza Jambo au Tukio la Kuibua Hisia Kubwa kisha kwa muda mfupi akatuhamisha haraka Kifikra.

Kwa jinsi huyu Mtu alivyoweza kutuhamisba katika Suala la Sabaya, Bajeti na Tozo hakika nampigia Saluti zote tu.

Na nahisi huyu Mtu Akili zote za Watanzania ameziweka Mfukoni mwake na anaziendesha atakavyo Yeye.

Halafu sijui huyu Mtu ana Dawa gani kwani kuna muda Watanzania tunakuwa na Hasira ila Yeye Kiustadi anazituliza zote.

Tumelilia hapa Katiba akatuletea Mzee Mpili na juzi tumelia Tozo katuletea Haji Manara na Barbara Gonzalez.

Nahisi huyu Mtu kama yupo nchini Tanzania atakuwa analipwa Mshahara mkubwa na ana Sifa pia ya Mazingaombwe.

Nasikia tena kwa Tukio la Kihisia la Mwanasiasa lililopo sasa kati ya leo na jumanne kuna Tukio la Kutusahaulisha.

Natamani mno Mwanasaikolojia Nguli anitajie huu Ugonjwa wa Kushadadia jambo kwa Kasi na Mihemko Mitandaoni Kisha Watu hao hao wanalisahau hilo Jambo au wanaacha Kulijadili na Kudakia mengine Kitaalam unaitwaje na Tiba yake hasa ni nini.

Chuo cha huyu Mtu kipo wapi nikijue?
 
Tumelilia hapa Katiba akatuletea Mzee Mpili na juzi tumelia Tozo katuletea Haji Manara na Barbara Gonzalez.
Mimi nilianza kuelewa ile siku yule mstaafu kapewa benzi ya mamilion zikatrend kweli mtandaoni ,mr.propaganda akasema mechi ya simba na yanga ndo inaweza kahamisha hisia za benzi kidogo tuu tukahamia kwenye ligi mtandao ukajaa usimba na yanga hoja ya zawadi ya mamilioni ikakosa nguvu,katiba+tozo zikafunikwa na mwanapropaganda manara na kesi ya ugaidi kesho tunaingia kigoma tutasahau
 
Sudden display; flash; glitter. Kifupi wenyewe wanaitambua kama distriction
Ajali ya treni iligonga mwamba haikututoa kwenye reli

Ila

Swala la mbowe kukamatwa limepoza swala la katiba mpya

Sabaya hafuatiliwi tena kwa kiwango kile
Swala la tozo watu wamehamishwa kabisa
 
Wabongo tushachoka hata tukilalamika hakuna linalofanyiwa Kazi.....Inabid twenze2 na vinavyotrend tu!!

Mengine ni Pasua kichwa
 
Mimi nilianza kuelewa ile siku yule mstaafu kapewa benzi ya mamilion zikatrend kweli mtandaoni ,mr.propaganda akasema mechi ya simba na yanga ndo inaweza kahamisha hisia za benzi kidogo tuu tukahamia kwenye ligi mtandao ukajaa usimba na yanga hoja ya zawadi ya mamilioni ikakosa nguvu,katiba+tozo zikafunikwa na mwanapropaganda manara na kesi ya ugaidi kesho tunaingia kigoma tutasahau
Usisahau na tukio la kuungua soko la Kariakoo lilivyoingia kati na ghafla kabla mjadala na lawama hazijakolea tukahamishwa kabisa

Sasa kesho huko Kigoma ndio itapelekea kwa wiki nzima kujadili matukio ya Simba vs Yanga, maana hii gemu haina droo ni lazima mmoja awe bingwa
 
Kama hayo Matukio ya Mzee mpili hayana mahusiano na Siasa Mzee,

Matukio mengi yapo kulingana na Muktadha wa tasnia husika, na yanajitegemea.

Machache Sana ndio yanauhusiano na kuichota jamii fikra
Hata mimi ndivyo ninawaza hivyo, mambo kama ya mzee mpili sidhani kama yanatumika kisiasa, na pia huyo mtu anaemsemea mleta uzi kazi yake ni ndogo sana.

Mbona ni rahisi sana kutwist akili za wabongo, walio mitandaoni wengi sio wafatiliaji wa siasa, kwahiyo we wape kile wanataka watakuja wenyewe tu. Waambie diamond kafanya hiki, au kamai ivo manara kaisema vibaya simba...
 
Back
Top Bottom