Je, ushawahi kutana na watu wapenda matukio kiasi kwamba yeye bila kufanya tukio la ovyo hajisikii vizuri?

mr pipa

JF-Expert Member
Jul 26, 2021
2,330
4,853
Kuna jamaa yangu mmoja yeye ni mtu wa kupenda kesi, huyu jamaa ikipita wiki hajafanya tukio jua atakuwa anaumwa.

Moja ya tukio lililoniacha mdomo wazi na kujiuliza kama huyu mwenzangu ni binadamu wa kawaida au vipi?

Kuna siku kaja kwangu anahitaji kibarua cha kulima basi nikamwambia nenda kwa jamaa anataka mfanyakazi wa kulima na kweli akapelekwa site akaoneshwa akaanza kazi, baada ya wiki akampigia simu boss wake uje upande nimemaliza, basi boss akabeba mbegu zake kwenda kupanda kufika kule boss anakuta kamlimia matuta mawili na tayari kashakula pesa nusu.

Mwenye shamba akachukia sana akamtia makofi na kumpeleka polisi, wakamuweka ndani wiki na kuambiwa alipe jamaa akadai anamtafutia pesa yake. Imepita wiki jamaa kapewa pesa yake kumbe alienda tafuta wateja kuuza shamba lile lile la jamaa, hapa ninapoongea kesi ipo mahakamani.

Kiufupi huyu jamaa ana matukio ya ovyo mfano hakuna na wala habadiliki wala kujifunza.

Je, ushawahi kukutana na watu wa aina hiyi kwenye jamii yako?
 
Hii sijui huwa ni laaana ama kitu gani nina mjomba wangu nae hana tofauti na huyo jamaa uliye muuelezeea hapo juu ni mtu wa matukio.

Alafu watu wengi wa namna hiyo huwa wanaaminika ila ukimuamini tu ndani ya muda mfupi anakupga tukio.
 
kuna ndugu yangu (bro) kuna mishe alikuwa anafanya alikuwa anamsimamia nikaona kama inaenda vizuri.Nikamwambia acha mimi nikupe pesa tufanye faida tutagawana kweli bwana biashara kama mwezi kwa kuwa yeye ni mzoefu ikakubali.Nikaongeza mtaji jamaa kutia tu ile pesa nikaanza kouna kona nyingi kufatilia nikaambiwa na mke wake siku hata nyumbani halali kiufupi mtaji amekula wote.Tukazinguana sana hakuna salamu
Muda ukapita yakaisha kama ndugu,akaenda kijijini huko kusalimia ile anakaribia kurudi nikamwambia nataka msichana wa kazi wife akamtumia pesa ya nauli,ile pesa akaipiga ,halafu kule kijijini alipewa debe la karanga aniletee town akauza nalo.
yaani yule jamaa alienda kwa bmkubwa mkoani kumsalimia baada ya muda mrefu ile anaondoka akampiga bmkubwa blanket na akachukua kimkufu cha dogo.
Alienda kwa syster kutembea akampiga kisimu chake cha nokia,aliwahi iba baiskeli ya mshuwa akauza.Yaani msela alikuwa akija kwangu uanakaa nae kimkakati.
Ila ukimuona smart bishoo flani na anapata pisi za viwango kweli
 
Kuna jamaa yangu mmoja yeye ni mtu wa kupenda kesi, huyu jamaa ikipita wiki hajafanya tukio jua atakuwa anaumwa.

Moja ya tukio lililoniacha mdomo wazi na kujiuliza kama huyu mwenzangu ni binadamu wa kawaida au vipi?

Kuna siku kaja kwangu anahitaji kibarua cha kulima basi nikamwambia nenda kwa jamaa anataka mfanyakazi wa kulima na kweli akapelekwa site akaoneshwa akaanza kazi, baada ya wiki akampigia simu boss wake uje upande nimemaliza, basi boss akabeba mbegu zake kwenda kupanda kufika kule boss anakuta kamlimia matuta mawili na tayari kashakula pesa nusu.

Mwenye shamba akachukia sana akamtia makofi na kumpeleka polisi, wakamuweka ndani wiki na kuambiwa alipe jamaa akadai anamtafutia pesa yake. Imepita wiki jamaa kapewa pesa yake kumbe alienda tafuta wateja kuuza shamba lile lile la jamaa, hapa ninapoongea kesi ipo mahakamani.

Kiufupi huyu jamaa ana matukio ya ovyo mfano hakuna na wala habadiliki wala kujifunza.

Je, ushawahi kukutana na watu wa aina hiyi kwenye jamii yako?
Diamond kuibiwa kofia.
 
Hii sijui huwa ni laaana ama kitu gani nina mjomba wangu nae hana tofauti na huyo jamaa uliye muuelezeea hapo juu ni mtu wa matukio.

Alafu watu wengi wa namna hiyo huwa wanaaminika ila ukimuamini tu ndani ya muda mfupi anakupga tukio.
sana na wana bahati sana
 
kuna mwingine alikosa pesa ya kununua malaya akapiga hesabu zake akapata jibu basi akaenda chukua dumu kubwa akatia maji akaongea na demu wakakubaliana akachukua boda mpaka gest na lile dumu na yule demu walipofika gest akawaacha wa boda na yule dem ye akazama ndan akamsomesha muhudumu wa gest akaingia lingi akampatia chumba pamoja na buku tatu ya kumlipa boda mana sijui aliongea nn kilichofuata wakafungua dumu lao na kumsisitiza muhudumu jitahid sana unitunzie huu mzigo bas jamaa akazama ndan kala mzigo kama masaa matatu kavaa zake kamwambia dem usitoke nakuja mana tukitoka wote muhudumu asije akanidhurumu mzigo wangu mi naenda droo pesa bank kilichofuata maumivu kwa wote demu pamoja na muhudumu alikuwa anajua ile ni petroli kwahy jamaa asingeweza kuacha lita 20 kisa buku ten ya gest awakujua awakujua
 
Back
Top Bottom