Nafikaje udsm(main campus)

Nafikaje udsm(main campus)

Jamani Dar siyo nyepesi hivyo, na huo mzunguko wa afike Ubungo, aende mpaka Kivukoni, avuke kwenda Kigamboni, Tuangoma, halafu arudi UDSM, siyo jambo dogo kabisa.

Nina uhakika atachemsha, na si ajabu akapigwa pale Ubungo hiyo usiku.

Mkuu Usimtishe Bhana! 😀😀😀
Si Ubungo Mwendo Kasi ipo palepale Moja kwa Moja Mpaka Ferri. 😀😀😀
 
Anaenda kusalimia mwalimu mkuu wa chuo

Atoe maelezo mazuri anaweza kusaidiwa, kama unaenda kujoin chuo kunakuwa mzunguko ile wiki ya kwanza, hustle za Tuangoma mpaka UDSM kwa mgeni hili jiji ni changamoto.

Otherwise kuwe na mtu wa kumpokea ampeleke Tuangoma then UDSM, walau mara moja tu.
 
Wamechangia vizuri wachangiaji ila nadhani hawafahamu Tua ngoma ipo eneo gani. Tua ngoma ipo mara tu baada ya kupita kongowe hivyo kupitia feri ni kuzunguka sana. Kuna mabasi ya moja kwa moja kutoka Tuangoma hadi kariakoo nadhani hiyo ndio itakuwa njia nafuu na fupi, akifika Kariakoo sasa hapo atapanda Mwendo kasi na kufuata maelekezo kama yalivyotolewa hapo juu ya kushuka Ubungo Maji na Kupanda boda boda kushuka Utawala

Kwa Ninvyoijua Kariakoo Basi Unataka Kwenda Kumuibisha
 
Umemshauri Vizuri Sana Kutoka T/Ngoma Mpaka UDSM.

Mimi Namuongezea Kwa Sehemu Ulioiacha.

• Kutoka TUNDUMA Mpaka UBUNGO (DAR) utafika SAA MBILI usiku au Zaidi.

• Ukishafika UBUNGO utaona Daraja (Flyover) watu Wanapanda Juu Kwahiyo Nawewe Panda Juu halafu Shukia Kwa Ndani Utakata Tiketi Ya Mwendo Kasi (Basi) Kwa Shilingi 650/=.. Lakini Kwa Muda Huwo Mabasi Yanajaa Nyomi Kwahiyo Likisimama tu Basi Kimbilia Uingie Hivyohivyo.

• Ukiwa Ndani Ya Mwendo Kasi Ukiangalia Kwa Dereva Kule Juu ya WindScreen Basi linasoma Vituo Vyote Linavyosimama.
Wewe Hakikisha Unashuka Kituo Cha Mwisho Kabisa Ambacho Basi Litasoma Final Destination Ferri Terminal.

• Ukifika Ferri Shuka Utaona Watu Wanakoelekea Kutoka Hapo Stand, Then Elekea Upande Wa Pwani Utaona Bango Kubwa Hivi then Mbele Ya Hilo Bango ndiyo Utaelekea Kukata Tiketi Ya Kivuko Kwa Sh. 200/= Na Kuingia Jengo la Abiria.
Note: Tiketi Za Kivuko Kama Hujawahi Kuzitumia Zinaweza Zikakuzingua Wakati Wakuingia Kwenye Jengo la Abiria Kwani Zinasoma Kielectronic. Kwahiyo Zikikuzingua Basi Angalia Upande Wa Kushotoni Utakuta Kuna Uwazi Wewe Pita tu Kwanye Huo Uwazi, Haina Shida Wala Usijali.

• Lango la Jengo la Kusubiria Abiria Likifunguliwa tu Utaona Watu Wanakimbilia Kwenye Kivuko, Lakini Wewe Hata Usijilazimishe Kukimbilia Bali nenda Taratibu tu Mpaka Ndani Ya Kivuko.

• Kivuko Kikishafika Upande Wa Pili Abiria Nyote Mutashuka...
Ukishashuka Fuata Abiria Wenzio Wanakoelekea Mpaka Nje Ya Geti Utakutia Njia Panda; Njia Moja imeelekea Kushoto Na Nyengine imeelekea Kulia. Hakikisha Unaiacha Njia Ya Kushoto Usiifuate, Na hapo Fuata Njia Ya Kulia.

Hiyo Njia Ya Kulia ifuate Moja Kwa Moja Bila Ya Kupinda Popote baada Ya Masafa Kama Ya Mita 150m hivi itakupeleka Mpaka Stand Kuu ya Kigamboni.
Njiani Kuelekea Stand Na Hapo Stand Wenyewe Muna Biashara Kibao za Vyakula, Vinywaji na Matunda Kama Una Ubao Basi Unaweza Ukajipendelea tu.

Hapo Stand Tafuta Gari iliyoandikwa T/NGOMA - FERRI. Ukishapanda Gari ya Abiria Mpigie Simu Mwenyeji Wako Ushuke Gari Kituo Gani then Yeye atakusubiri Hapo.

Note: Hakikisha Usije Ukapanda Gari ya KIBADA - FERRI utaishia Njiani Kibada Stand.
Aisee mkuu umeua hatari aisee,kweli Watz ni wakalimu sana sema vyama vya siasa vinatuvuruga aisee!! Hongera!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Usimtishe Bhana! 😀😀😀
Si Ubungo Mwendo Kasi ipo palepale Moja kwa Moja Mpaka Ferri. 😀😀😀

Siku hizi tochi barabarani hazina guarantee, anaweza akafika saa tano na nusu na mwendo kasi haifanyi kazi.

Hata akifika mapema, logistics za mwendo kasi ni lazima aulize kwa mtu, Ubungo unamuliza nani?

Maana pale kuna wazee wa fursa (wanaosubiri watu kutoka mikoani wawalize).

Aisee pale ni pabaya sana kwa mgeni.
 
Nakushauri tu huyo mwenyeji wako mwambie kuwa we we dar ndio mwanzo unafika akupereke hadi chuo.

Vinginevyo utapigwa mapema tu ukifika
 
Mkuu Usimtishe Bhana! 😀😀😀
Si Ubungo Mwendo Kasi ipo palepale Moja kwa Moja Mpaka Ferri. 😀😀😀
Kop kwa Dar ilivyo tena Ubungo mida hiyo gari inafika na saivi vyuma vilivyokaza na mtu ndio first time anafika, possibility ya kupigwa ni kubwa sana.

Mimi namshauri mleta uzi ajitahidi kuongea na mwenyeji wake ili amuombe awepo Ubungo muda basi litakapofika. Yani akishuka tu anakutana na mwenyeji wake wanaondoka. La sivyo hali inaweza kuwa tete.

Kesho yake ndio huyo mwenyeji wake ampeleke UDSM ana kumzungusha zungusha maeneo muhimu ya jiji. Baada ya hapo anaweza kuanza kufanya mambo mengine mwenyewe.
 
Hicho ndo nilichoshauri pia, ubaya kwa mishe za mji huu kupata mtu wa hivyo ni ngumu.

Labda awe linked na madogo wengine wanaoenda kuanza chuo.
 
Hicho ndo nilichoshauri pia, ubaya kwa mishe za mji huu kupata mtu wa hivyo ni ngumu.

Labda awe linked na madogo wengine wanaoenda kuanza chuo.
Yeah ni kweli, ila ushauri ni muhimu hapa jamaa achague upi unamfaa. Maana naamini mtu anatokea Tunduma ni mjanja mjanja sio waki kwasababu miji iliyopo boda watu wanakuwa wajafanja kiaina.

Chamuhimu pia kama kuna uwezekano asijibebeshe mizigo mingi isiyokuwa ya lazima.
 
Khaaaa toangoma palefu nahisi iyo ipo kongwe mbagara sasa unapanda gar toka kongowe mpka mbagara then mbagara panda za mbgara makumbusho shuka makumbusho chukua za makumbusho mbenzi au gongoramboto shuka magufuli hostel
Mpaka hapo kishapotea!!!. Hahaahhaaaaa mi nadhan mwwnyej wake ampe kampani tu
 
Yeah ni kweli, ila ushauri ni muhimu hapa jamaa achague upi unamfaa. Maana naamini mtu anatokea Tunduma ni mjanja mjanja sio waki kwasababu miji iliyopo boda watu wanakuwa wajafanja kiaina.

Chamuhimu pia kama kuna uwezekano asijibebeshe mizigo mingi isiyokuwa ya lazima.

Huo Ujanja Wake Wote Wa Tunduma Hawezi Kuufanya Dar tena Hata Kule Tegeta Hawezi Kuufanya achiliambali Ubungo.

Tena Kibaya Zaidi Ole Wake Akifika Ubungo Aibiwe Simu! Hapo Nakuhakikishia Ataondoka na Boxer tu pamoja na Korodani Zake.
 
Back
Top Bottom