Nafasi za kazi Jeshi la Polisi Tanzania

Wale Wa Uhamiaji
 

Attachments

  • KUITWA-KWENYE-MAFUNZO-MARCH-2024.pdf
    169.4 KB · Views: 4
Tarehe 25/03 Jumatatu Mapema Kabla Ya Saa 5 Asubuhi Vijana 3701 Waliapa Na Kukamilisha Mafunzo Ya Awali Ya Jeshi La Polisi Katika Kambi Ya KILELEPORI Iliyopo Kilimanjaro Wilaya Ya SIHA Karibu Na BomaNg'ombe Huku Mgeni Rasmi Akiwa Ni Waziri Wa Mambo Ya Ndani Eng. Masauni...

Wageni Mbalimbali Walikuwepo Ikiwemo Kutoka Jeshi La Polisi, Makao Makuu Ya Polisi, Jeshi La Magereza, Jeshi La Wananchi, Mkuu Wa Mkoa Wa Kilimanjaro, Mkuu Wa Wilaya Ya SIHA Na Wageni Wengi.

Wahitimu 1200 Walibaki Kambini KILELEPORI Kuendelea Na Mafunzo Ya Kutuliza Ghasia (Field Force Unit - FFU) Ambapo Watahitimisha Kozi Tarehe 04/04/2024, Wahitimu Wengine Zaidi Ya 250 Wakibaki Kwa Kozi Ya Intelligency Kwa Muda Wiki 2. Pia Wahitimu Zaidi Ya 300 Walibaki Kuendelea Na Masomo Ya CERTIFICATE IN POLICE SCIENCE Na Watahitimisha Mwezi Wa 8 Kisha Kuelekea Kwenye Vituo Vyao Vya Kazi Walivyopangiwa.

Wahitimu Wengine Wote Wamesharipoti Katika Vituo Vyao Vya Kazi Mikoani Ambapo Kutakuwa Na Mafunzo Mengine Ya Wiki 8 (Miezi 2) Yakayoendelea Mikoani Mwao Kwa Ajili Ya Utayari Wa Kuanza Kazi Baada Ya Mafunzo.

Itoshe Kusema KOZI Ilikuwa Ndefu Na Ngumu Hasa Kutokana Na Sheria Za Chuo Na Mazoezi Ya Utayari. Kwa Muda Wa Mwaka Mzima Vijana Wamepambana Wakizunguka Kambi Zote Tatu Kuanzia Kambi Ya CCP/TPS, Kambi Ya KILELEPORI, Kambi Ya KAMBAPORI (West).

Ni Wakati Wa Vijana Kulitumikia Taifa Kwa Kuonesha Uzalendo Katika Ufanyaji Wa Kazi Kwa Usalama Wa Raia Na Mali Zao.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom