Na Ndiyo Maana Jeshi Pia Huwachukua Vijana Waliomaliza Form Six unafikiri wale wanabakiaga Form Six Milele? Nina ndugu yangu anapiga Course China Aerospace Engineering yeye alingia na PGM mwaka 2014 kwa hiyo Usitake Kulazimisha Miaka Uliyonayo wewe Kama Una Miaka 27 kuna Majeshi Mengi Sana Tanzania Nenda Magereza Patakufaa. Ila JWTZ Umri mwisho miaka 25.
Kujiunga JWTZ
Uandikishaji
Askari
Mtu yeyote ataandikishwa kujiunga na Jeshi
la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)
kwa sifa zifuatazo: -
*. Awe raia wa Tanzania
*. Awe na Elimu ya kidato cha nne
nakuendelea na awe amefaulu..
*. Awe hajaoa/hajaolewa
*. Awe na umri kuanzia miaka 18 hadi 25
*. Awe na tabia na mwenendo mzuri
*. Awe na akili timamu na afya nzuri
Masharti ya Utumishi
*. Askari atapewa nambari ya utumishi
baada ya kufaulu mafunzo ya awali.
*. Atalitumikia Jeshi kwa kipindi cha mwanzo
cha miaka sita, baada ya hapo atafanya kazi
kwa mkataba wa miaka miwili miwili kwa
kibali cha Mkuu wa Majeshi.
Maafisa
*. Bodi ya Uteuzi wa Maafisa
(OfficersSelection Board)
huwafanyia usaili askari wenye elimu ya
kidato cha sita na kuendelea toka Vikosini na
Shule za askari wapya (Recruitment
Schools).
*. Watakaofaulu masailiano hayo hupewa
hadhi ya Afisa Mwanafunzi (Officer Cadet),
na hupelekwa Chuoni (Tanzania Military
Academy) kwa mafunzo yauafisa kwa muda
wa mwaka mmoja.
Source:
www.tpdf.mil.tz (website yao kwa Sasa haiko hewani)