JWTZ mnatangaza ajira zenu lini?

Team Samia

Member
Jan 9, 2022
16
13
Kwanza niwapongeze kwa kazi nzuri sana mnayofanya, kwangu nyie ndo taasisi bora zaidi Tanzania hii.

Nikija kwenye mada, lini mtatangaza ajira ?

Mwaka uliopita 2021 walianza Polisi, wakaja Magereza, kisha Uhamiaji na mwisho Zimamoto.
Mwaka huu (2022) mwanzoni Uhamiaji wakatangaza tena.

Kulikoni JWTZ? Mbona kimya.

Kwa unyenyekevu kabisa naomba kuwajulisha kuwa kuna vijana wengi mtaani katika makundi tofautitofauti ambao wanasifa za kujiunga na jeshi.

1. Wapo ambao wamemaliza kidato cha nne ambao hawajabahatika kwenda JKT ila sifa zote wanazo.

2. Wapo waliomaliza kidato cha sita ila hawakubahatika kuchaguliwa jkt kwa mujibu wa sheria kwa sababu ya ukosefu wa nafasi makambini ila wana sifa na moyo wa kulitumikia jeshi letu.

3. Mwisho ni kundi la wasomi wa ngazi ya shahada/ stashahada nk ambao baada ya kuhitimu masomo yao wangependa kujiunga na jeshi.

4. Walioenda jkt kisha muda wao ukaisha wakarudi mtaani.

Kukaa kwenu kimya ni kuyanyima makundi yote hayo fursa.

Pamoja na kwamba kuna vijana kwenye kambi mbalimbali za JKT, vijana walio mtaani nao wana haki na ndo wengi zaidi.

Tangazeni ajira kisha iwepo free and fair competition.

Hata hivyo kama utaratibu wenu wa ajira umebadila muujulishe uma kuliko kukaa kimya.

Jenerali Venance Mabeyo na timu yako naamini kuwa nyie ni weledi na mtalifanyia kazi hili.
 
Namwomba tu CDF Jenerali Mabeyo amuidhinishe rasmi huyu Luteni Kanali Gervas Ilonda awe Mkuu ( Mkuregenzi ) rasmi wa Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa JWTZ na asiendelee tena Kukaimu kwani ameshaonyesha Uwezo na ukiona hadi GENTAMYCINE nakukubali jua hata Malaika wa Mbinguni akina Mikaela na Gabriel nao kwa Niaba ya Mwenyezi Mungu wamekubali ( wamekukubali ) pia.
 
Namwomba tu CDF Jenerali Mabeyo amuidhinishe rasmi huyu Gervatius Ilonda awe Mkuu ( Mkuregenzi ) rasmi wa Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa JWTZ na asiendelee tena Kukaimu kwani ameshaonyesha Uwezo na ukiona hadi GENTAMYCINE nakukubali jua hata Malaika wa Mbinguni akina Mikaela na Gabriel nao kwa Niaba ya Mwenyezi Mungu wamekubali ( wamekukubali ) pia.
Yuko kwenye matazamio
 
Tupo wengi tunao subiri hizo ajira, watu tukapigike pale RTS na oljoro.. Watu tuvae baka,

Sent from my Infinix X572 using JamiiForums mobile app
Bro bakabaka halivaliwi kirahisi kama nguo ya mtumba unayokwenda pale Ilala kuchukua, sikukatishi tamaa ila mpaka kuja kuvaa bakabaka umeumia sana kwenye mafunzo na ikibidi hata kufa. Cha msingi hakikisha uko timamu kiafya huna tatizo lolote linalokusumbua,omba Mungu nafasi nikitoka apply ukibahatika nenda kafanye mafunzo ya awali, ukibahatika kutoboa six weeks wee umemaliza depo, subiri kupass out na kupangiwa kituo cha kazi.
 
Amadhani kuvaa bakabaka ni rahisi kama kutangaza Baraza la Mawaziri.
 
Bro bakabaka halivaliwi kirahisi kama nguo ya mtumba unayokwenda pale Ilala kuchukua, sikukatishi tamaa ila mpaka kuja kuvaa bakabaka umeumia sana kwenye mafunzo na ikibidi hata kufa. Cha msingi hakikisha uko timamu kiafya huna tatizo lolote linalokusumbua,omba Mungu nafasi nikitoka apply ukibahatika nenda kafanye mafunzo ya awali, ukibahatika kutoboa six weeks wee umemaliza depo, subiri kupass out na kupangiwa kituo cha kazi.
Acha kutisha watu na stori za vijiweni wewe kufa watu huwa wanakufa kutokana na maradhi ni mara chache wanakufa kutokana na mafunzo kitu ambacho ni kawaida hata fundi ujenzi anaweza kufa akiwa kazini kwahiyo acha mboyoyo mingi
 
Sijamkatisha mtu tamaa naeleza reality, ili likitokea tatizo kusiwe na wa kulaumiwa.
 
Sijamkatisha mtu tamaa naeleza reality, ili likitokea tatizo kusiwe na wa kulaumiwa.
Acha uongo wa vijiweni mafunzo yanayo tolewa ni mafunzo ya ukakamavu na medani za kivita biashara za kutishia watu vifo kila wakitaka kujiunga na jeshi huo ni ushamba wa kizamani, hakuna anae uwawa mafunzoni
Na wala hakuna alie wahi kulaumiwa kisa mtu kafa kwenye mafunzo kifo kinatokea ukiwa sehem yoyote
 
Acha uongo wa vijiweni mafunzo yanayo tolewa ni mafunzo ya ukakamavu na medani za kivita biashara za kutishia watu vifo kila wakitaka kujiunga na jeshi huo ni ushamba wa kizamani, hakuna anae uwawa mafunzoni
Umeelewa nilichokiandika au unadandia treni kwa mbele, hayo mafunzo ya ukakamavu unayoyasema kama afya mbovu si utajifia hata kabla hujamaliza mafunzo yenyewe.
 
Umeelewa nilichokiandika au unadandia treni kwa mbele, hayo mafunzo ya ukakamavu unayoyasema kama afya mbovu si utajifia hata kabla hujamaliza mafunzo yenyewe.
Hakuna anaejiunga mafunzo ya jeshi lolote bila kupimwa afya mzee na mtu yoyote ambae Hana ulemavu wala magonjwa sugu anaweza kumudu hayo mafunzo hakuna Cha ajabu
Acheni kutisha watu humu
 
Back
Top Bottom