tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,038
Wakuu! Nisaidieni mimi ni Dada mtu
Nina mdogo wangu alienifuata jinsia (kiume) umri (16) anakabiliwa na madadiliko ya ukuaji kimwili, miongoni mwa mabadiliko hayo ni pamoja na kubadilika kwa sauti yake. Siku za hivi karibuni sauti yake imekua kubwa sana na nzito, hali inawafanya marafiki na majirani wamshangae sana na kumwambia kuwa amekua.
Sasa hizi feedback za watu juu ya mabadiliko hayo ndizo zinazomtatiza. Wakati mwingi ananyamaza kimya, anashindwa kuchangamana na watu so huwa anajitenga muda wote, hata ukijaribu kumsemesha anaitikia kwa sauti ya chini tena huku akiwa ameinamisha kichwa chini, hawezi hata kutazamana na watu kisa tu kuambiwa hivyo kuwa anasauti kubwa au kuwa amekua.
Matokeo ya yeye kuji-isolate kunamfanya aanze kudhoofika, anakosa amani hawi huru tena. Namimi hiki kinaniumiza natamani sana kumuona akiwa katika hali nzuri ya amani na ya uhuru na kwa asili yeye ni mchangamfu sana ila sasahivi amekua wa tofauti mno na sauti yake licha ya kuwa imekuwa nzito na kubwa ila ni nzuri mno na kidogo akiwa namimi angalau anakuwa huru kidogo, sasa nitakaa nae mpaka lini?.
Nafanyaje ili aweze kuekubailiana na hii hali au kuendana na hayo mabadiliko maana anakoelekea anaweza kugeuka na kuanza kujenga tabia ambazo zinaweza kuja kuwa hatarishi baadae maana tayari kuna watu hawezi hata kusalimiana nao. Naombeni ushauri