NACTE: Tuna changamoto ya vyuo ambavyo havijasajiliwa, Watanzania wengi wanavipenda kwa ada yake ya chini

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,445
7,816
Mkurugenzi wa udhibiti NACTE, Geofrey Oleke amesema ipo changamoto ya vyuo ambavyo havijasajiliwa pamoja na wao kuhakikisha havipo kwa kuvifuta na kwakuwa huwa vina ada ya chini, watanzania wengi wanavikimbilia bila kujua kwamba vimesajiliwa ama La.

Pia mkurugenzi huyo amesema vipo ambavyo vimesajiliwa lakini vinafanya utapeli kwa kuwapigia simu wanafunzi sasa waende vyuoni badala ya mwezi wa kumi na kuwaongezea gharama. Pia amesema inamnyima mwanafunzi fursa ya uchaguzi

Amesema vyuo hivyo vinawasiliana na mkuu wa shule anayotoka mwanafunzi na kuwatumia ujumbe mfupi wa maneno kudai wamechaguliwa kwenye vyuo vyao.
 
Unafuta vipi kitu ambacho haujakisajili?! Kama mamlaka inayosimamia elimu ya juu haijaisajili taasisi hiyo inamaana ipo kinyume cha sheria, watu wanaibia wanafunzi.
 
Back
Top Bottom