Planner
JF-Expert Member
- Apr 5, 2011
- 348
- 149
Wadau Mchana wa leo (saa 6 mpaka 8 mchana) kumetokea vurugu mchana huu hapa Nachingwea hali iliyofanya polisi kujihami kwa kuanza kurusha mabomu ya machozi.
CHANZO CHA TUKIO:
Vijana waendesha pikipiki almaarufu bodaboda wengi wao yasemekana wakitokea Masasi wamefika kituo cha polisi hapa Nachingwea wakidai kumtafuta mtuhumiwa aliyempora pikipiki mwenzao,baada ya muda hali ikachafuka na polisi wa hapa wakajihami kwa mabomu.
Muda si mrefu maduka yote na biashara yakafungwa na hali ya mjini ikawa tete! Kilichonishangaza wakati niko na gari natoka nje ya mji nikakutana na lori la jeshi likiwa na askari wamevalia kivita na silaha linaingia mjini kwa kasi kuimarisha usalama, which implies polisi wamezidiwa nguvu.
Kwa sasa hali imetulia ila hofu imejaa mitaani.
My take:
Hivi jeshi la polisi litasukwa vizuri lini liweze kuhimili majukumu ya aina hii manake sidhani ni vizuri jeshi la wananchi kuingia mtaani hata katika mambo ambayo polisi wangeweza (labda pale inapobidi)-Hizi chokochoko za bodaboda vs polisi zitafutiwe ufumbuzi otherwise tutakujajilaumu baadae.
SOURCE: Mimi mwenyewe nimeyashuhudia leo hii mchana.