Nachingwea: Mabomu ya machozi yarindima mchana wa leo...

Nachingwea: Mabomu ya machozi yarindima mchana wa leo...

Kaka, hiyo nchi yako ...mabingwa wa kutatua na kuingilia migogoro ya nchi nyingine, kama jeshi la polisi tu ni weak ths much, nina mashaka sana na jeshi linalokimbilia kwenda 'kusafishia' jina kwa madreva bodaboda wenye mawe tu na petrol! Hii mikwara ya JW naombea iishie humu humu, tusijetia aibu ... wasiwasi wangu usjekuta hata MALAWI wakatupimia...

Kuna watu wasio na akili watasema ni vyama vya upinzani viko nyuma yao subiri wataanza kusema
 
Ukweli ni kwamba madereva wa bodaboda ni 'jeshi' lingine la kuangaliwa. Polisi wanabidi kujifunza namna ya kushughulika nao
 
wa kusini nimewapendaaaaaaa!! how i wish nchi nzima ingekuwa hivi!!
Wewe utajificha wapi Au wewe Ni kifo proof. Nenda Syria Au hata angalia Kwenye tv. Unashabikia vurugu ila zikikukuta wa kwanza kulia mamaaaa
 
Yani bodaboda wa Kusini ndiyo wababe wa polisi. Wanawezaje kufunga vituo vya POLISI???
Kumbuka kwamba wawndeshaji wengi wa bodaboda ni vibaka na wavuta bangi wastaafu!
Nadhani timbwili yake unaifahamu!
 
Chamuhimu sasa naona serikali ifungie usafiri wa Boda boda. Hawa vijana wamekuwa kero sana. Vifo, vilema, na matatizo mengi yameanza gafla baada ya huu usafiri kuwepo. Ukizingatia hata hauna tija kwa serikali cuz hauchangii chochote kwenye pato la taifa. Chamsingi ni vijana watafute means nyingine za kujikwamua kiuchumi. Boda boda is not everything!!

Ila TIJA yao inakuwepo pale wanapotumika kusindikiza msafara wa chama chetu na kuwapa 10,000 za mafuta na kipande cha siku. Rajao acha madharau bana.

12.jpg CHWAKA 024.jpgpikipiki.jpg
 
Huu ushemeji Shemeji mpaka kwenye uongozi wa nchi matokeo yake ndio haya,polisi wamekuwa kama mbwakoko,mkia masaburini....
 
Kusini wamepiga Arusha bao Tayari kwa Arakati za dhati.
 
Tunajua wachochezi ni nani. Mbona hamfanyi hivyo huko kwenu. Wabinafsi sana. Viongozi wa fujo Masasi wote ni wageni na wamekimbia.

Nani sasa mchochezi? Mnadanganyana kweli nyinyi!.... nani kawaambia kuongoza watu ni kwa kubahatiha bahatisha. Mnavuna mnayopanda.
 
JK anavuna wizi wa kura hata kabla hajatoka madarakani? Nchi kwa kweli haiwezi hii na kama alivyosema mhenga haitawaliki.
 
hawa bodaboda sasa wadhibitiwe kwa mbinu mbadala....mabomu na risasi havisaidii
 
Chamuhimu sasa naona serikali ifungie usafiri wa Boda boda. Hawa vijana wamekuwa kero sana. Vifo, vilema, na matatizo mengi yameanza gafla baada ya huu usafiri kuwepo. Ukizingatia hata hauna tija kwa serikali cuz hauchangii chochote kwenye pato la taifa. Chamsingi ni vijana watafute means nyingine za kujikwamua kiuchumi. Boda boda is not everything!!
Umeshasahau kuwa Babaako Kikwete aliposema ametoa ajila milioni kwa vijana zilikuwa pamoja na bodaboda.(aliyeunguzwa na moto hachezi na mkaa) Hekima inahitajika sio mabavu.maana Jibu la upole ugeuza hasira.
 
Polisi wakitumia nguvu wanaambiwa wametumia nguvu kupita kiasi, wakiepusha shari wanaitwa Goigoi, Haingii akilini vurugu wiki nzima maiti hazifiki angalau 50! Mamba hawezi jua kama ameumia mpaka waone Damu! Wangewapa kichapo kama kile walicholishwa wapemba au Watoto wa Arusha!
Nenda wewe Kashike Bunduki ukaue wafike 50 unaotaka au zaidi.Wapemba na wa arusha walipokufa kumbe ulifurahia.Kumbuka Mungu ataitaka damu yao mikononi mwa wauwaji.Kabla ya uharibifu moyo wa mwanadamu hujivuna.Na ukiona Heshima fahamu ulitangulia Unyenyekevu
 
Wadau Mchana wa leo (saa 6 mpaka 8 mchana) kumetokea vurugu mchana huu hapa Nachingwea hali iliyofanya polisi kujihami kwa kuanza kurusha mabomu ya machozi.

CHANZO CHA TUKIO:
Vijana waendesha pikipiki almaarufu bodaboda wengi wao yasemekana wakitokea Masasi wamefika kituo cha polisi hapa Nachingwea wakidai kumtafuta mtuhumiwa aliyempora pikipiki mwenzao,baada ya muda hali ikachafuka na polisi wa hapa wakajihami kwa mabomu.

Muda si mrefu maduka yote na biashara yakafungwa na hali ya mjini ikawa tete! Kilichonishangaza wakati niko na gari natoka nje ya mji nikakutana na lori la jeshi likiwa na askari wamevalia kivita na silaha linaingia mjini kwa kasi kuimarisha usalama, which implies polisi wamezidiwa nguvu.

Kwa sasa hali imetulia ila hofu imejaa mitaani.

My take:
Hivi jeshi la polisi litasukwa vizuri lini liweze kuhimili majukumu ya aina hii manake sidhani ni vizuri jeshi la wananchi kuingia mtaani hata katika mambo ambayo polisi wangeweza (labda pale inapobidi)-Hizi chokochoko za bodaboda vs polisi zitafutiwe ufumbuzi otherwise tutakujajilaumu baadae.

SOURCE: Mimi mwenyewe nimeyashuhudia leo hii mchana.
kwa hiyo unashauri hao polisi wangemwachia huyo mtuhumiwa?
 
Vurugu zenyewe bado washaanza kutumia jeshi mapema hv,zikianza watatumiza nn?
 
Back
Top Bottom