Nimeanza kuuelewa kwa nini Karl Max ,yule mwanashosholojia na mkomunisti wa Kijerumani alikuwa akiuchukia sana ukristo.Akiamini katika umuhimu wa wanyonywaji kujitambua na kuchukua hatua ya kujikomboa, aliiona dini, hasa uktisto ,kama kikwazo katika kuleta mapinduzi (mabadiliko ya ghafla ya kiuchumi , kiutamaduni ,kijamii na kisiasa) .Aliamini kabisa kuwa dini ni 'bangi ya watu' akimaanisha,mara baada ya kukolea katika imani za dini zao,waamini hushindwa kuwa na uwezo wa kuwa na utambuzi sahihi wa vyanzo vya hali zao,hasa ufakara wao na hivyo kukosa uwezo wa kujua mbinu za kujikwamua kutoka katika hali hizo kama matokeo ya kwa kupandikizwa 'false consciousness' katika akili zao na viongozi wao wa kidini.Haishangazi ,basi,kuona makanisa ya leo yanajaa watu wanaodhaniwa ni wafuasi wa Yesu Kristo,wakati ukweli ni kuwa kinachowavutia kufanya hivyo ni kutafuta relief na / au utajiri wa haraka,wala kumpenda Yesu hakupo mioyoni mwao.Hawaelewi kuwa maombi pekee,kama tendo la kiimani, bila kuambatana na matendo,hayawezi kuleta mkate mezani, wala kuleta karo ya shule ya watoto.
Nabii huyu, huenda hakujua kuwa, kwa miaka mingi Wameru wamekosa maji na ardhi.Hata kama alijua, ni wazi kabisa naye ni mhanga wa 'faslse consciousness" inayomfanya asielewe kwa nini Arumeru walihitaji mabadiliko kwa kupata mbunge mwanabadiliko.Ninaamini,Yesu si mwanadamu na hasemi uongo kama sisi wanadamu wakiwemo wanaojiita Manabii wa Mbezi ambao hata hawavutiwi kwenda kufungua kazi zao Temeke Mikoroshini ama Tandale wanapoishi watu maskini.
Kwa kuwa uongo haukabaliki- maana ni dhambi mbele za Mungu - mtu huyu ana neema ya kutubu na kujutia kosa lake mbele ya wafuasi wake, jumapili ijayo.Akifanya hivyo,atambue kuwa ipo tofauti kubwa kati ya 'maono toka kwa Mungu' na 'matamanio ama ndoto za mwanadamu '.Asipofanya hivyo,adhabu muafaka ,ambayo waumini wake wanayo mikononi mwao ni kutafuta mahali kwingine pa kumwabudu Mungu.Lakini kama nilivyosema hapo awali, ile 'false consciousness' na 'bangi' wanayopandikizwa haiwaruhusu kufanya hivyo.
Yesu hakuwa na ushirika na watawala wa wakati huo kutokana na maovu yao.Watawala hao hawakufurahishwa na ujio wake duniani na ndio waliopanga na kuratibu mateso na kifo chake.Watumishi wa kweli wa Mungu wanapaswa kuwa upande wa wanaonyonywa na kugandamizwa.Kwa Arumeru ,walionyonywa na kugandamizwa walifahamika ,kama ilivyo kwa wagandamizaji na wanyonyaji.Aidha, mkombozi wa kweli wa Arumeru alikuwa anafahamika na tunafurahi amepatikana jana.