Nabii Flora wa Mbezi DSM ameumbuka Uchaguzi Arumeru!

Ufunuo: na mwenye macho na asikie. Siku za mwisho hizooo!!!!! bahati mbaya sana hizi za manabii ndo dalili za mwisho mwisho.
 
KAKOBE alitapatapa 95 kuwa Mungu wake amemwambia NCCR watashinda,ikala kwake!
2005 Kilaini alibwatuka kuwa JK ni chaguo la Mungu...ukweli unaonekana!
Jamani,NJAA HAINA ADABU!
 
No wonder ana mkorogo wa kuua mtu. Halafu eti anajiita nabii!!! Nafikiri wenye matatizo makubwa ni hao wanaojazana kanisani kwake na kumnyenyekea eti ni "nabii". Wajinga ndio waliwao.

Tiba
 
Jamani, Biblia imefungwa haiongezwi wala haipunguzwi kitu, manabii wote wameandika unabii wao kwenye hicho kitabu takatifu, Hivi hawa wanaojiita manabii wanataka unabii wao uandikwe wapi?:rockon:
 
Nabii Flora (aliyeshika maiki) akiendesha maombezi kwa wenye matatizo.
Watu wenye matatizo wakishiriki maombi ya kuponywa kanisani kwa Nabii Flora.
WATU wengi wamekuwa wakifurika kutafuta uponyaji kwa njia ya maombezi kutoka kwa Nabii Flora ambaye mashuhuda wanasema anaponya magonjwa mbalimbali kama vile Ukimwi, kansa, kupoteza fahamu, magonjwa ya moyo, upofu, ulemavu na kadhalika.

Maombi hayo yaendeshwa na Nabii Flora huko Mbezi Beach maeneo ya Tangi Bovu jijini Dar es Salaam ambapo watu wenye kufuata huduma hiyo wamekuwa wakiwasiliana naye kwa kutumia namba za simu 0657 442699.

Zifuatazo ni picha zaidi za uponyaji katika kanisa la Nabii Flora:

Huyu ni mchawi mwingine kama TB Joshua na wengine wengi kama kina maji marefu.
Huu aliokuwa akiufanya ni mchezo wa kitoto unaitwa 'SPINNING'.
Tulianza na Mungu, Tumemaliza na Mungu.
 
Manabii walishakufa miaka lukuki ilopita, huyo shankupe, hakuna nabii mwnmke, yupo kibiashara zaidi. hana tofauti na babu wa loliondo hyu mdada.
 
Wizara ya Ardhi imemgomea kubadilisha matumizi ya kiwanja toka makazi kuwa kanisa, alishaambiwa ila jeuri anaendelea kufanya kanisa
 
Bado wa LOWASA yule mNIGERIA almaarufu km TB JOSHUA almtabiria kua ndo RAIS ajae wa TANZANIA basi LOWASA akaanza kulobby makanisa kwa kua km ndo fundraiser...sasa na yeye ajiandae kwani janja yao ya kuwatia hofu kwa kujifanya eti wana link na MUNGU inajulikana.....ama kweli wajinga ndio waliwao hivi watu bado wanamuamini huyo anae jiita nabii?
 
unabii ulioutoa hakutoka kwa MUNGU, na huenda anachoongoza sio kanisa ila cult fulani kama ile cult ya si.......malizia
 
hivi unabii wanautoa wapi?
Maana kila anayeibuka anajiita nabii, kama yule anayejiita mtume na nabii mwanzilishi wa kanisa ..........

Wanautoa wapi unabii?
 
Nabii Flora Wa Mbezi Beach aliwambia Waandishi wa habari kuwa ameoteshwa na miungu yake kuwa Mgombea wa CCM Sioni Summari Mkwe wa Edward Lowassa atashinda uchaguzi mdogo Arumeru.Habari hiyo iliandikwa Front page kwenye gazeti la Uhuru!!Kutokana na ushindi wa Mgombea wa Chadema Arumeru ni dhahiri kuwa Nabii Flora ni nabii wa uongo na tapeli!!!Hata hivyo juzi baada ya kutoa utabili huo alijitikeza kwenye vyombo vya habari na kusema kuwa ameombea watu UKIMWI na tayari watu 40 wamepona na kuthibishwa na madaktari. Tangazo hilo lilitolewa kwenye gazeti la tanzania Daima .

Huyu si Nabii,wa Mungu, ni MDWANZI, mpiga debe wa EL. Alisema kujipendekeza ili asifiwe akidhani mbinu kongwe ya "KUIBA KURA" Ingefanikiwa kama kawa!
 
nabii flora

wednesday, december 7, 2011
nabii flora akiwa kanisani kwake

akimtabiria mtu

hivi karibuni jijini dar es salaam kuna nabii mwingine mpya ambaye amekuwa maarufu kutokana na wingi wa watu wanaohudhuria kanisani kwake na kupata huduma za kiroho. Anajulikana kwa jina maarufu kama nabii flora, watu wamekua wakiongelea kazi na shuhuda zinazotokea mahali anapohudumu, kwamba watu wanaponywa magonjwa yote sugu, vipofu wanaona, uvimbe na kila aina ya magonjwa na matatizo mbalimbali.

mwaka 2011 pamekua na makanisa mengi ambayo watu wanakimbilia kupata huduma za kiroho na kimwili. Na nabii flora ni mmoja wa manabii ambaye amefanikiwa kupata watu wengi.


hako kadada na wenzake wanaojitangaza manabii na washirikina wa kutupwa.ona iyo picha wajinga walivyojazana kumsikiliza.wakienda hapo naigeria kwa t.b. Joshua kuchukuwa mazingaumbe basi watanzania tupendavyo maisha mazuri ya duniani tutajazana huko na maushuhuda ya uongo.yesu aliteseka mwanzo mwisho wewe unataka raha duniani.eti usiugue ,eti upate pesa,magari baada ya maisha ya hapa duniani vitakusaidia nini?nyie nendeni tuu.tena zungukeni kila anapoibuka tapeli mpya na mazingaumbe kabambe.siku ya mwi
 
KAKOBE alitapatapa 95 kuwa Mungu wake amemwambia NCCR watashinda,ikala kwake!
2005 Kilaini alibwatuka kuwa JK ni chaguo la Mungu...ukweli unaonekana!
Jamani,NJAA HAINA ADABU!


Acha maneno ya kutunga kuhusu Kakobe. Hakuwahi kusema lolote kuhusu NCCR, mwaka 1995. Ni mwaka 2000, ndipo alipompigia kampeni Mrema, wakati yuko TLP. Hata hapo, hakutoa UNABII wowote kuhusu Mrema. Kuna tofauti kubwa kati ya kutoa unabii, na kupiga kampeni. Kakobe hajawahi kujiita Nabii, wakati wowote ule!

Kampeni za Kakobe, mwaka 2000, alipokiponda chama cha magamba, kwa kusema alikuwa na sababu 1000 za kukichukia, ndizo zilikuwa moja ya vyanzo vya mwamko wa upinzani nchini. Na mwaka 2010, elimu yake ya uraia iliyokwenda shule, aliyoitoa katika TV, ilisaidia sana kuzima kampeni chafu za magamba, dhidi ya CDM. Hivyo, acha kuleta michanganyo hapa. Mada iliyoletwa hapa, ni juu ya NABII FLORA, na unabii wake, kuhusu Arumeru.
 
huyu mama kajikoboa kama jini..nabii gani anaishi kwa nguvu ya mkorogo.
 
Back
Top Bottom