Nabii Flora wa Mbezi DSM ameumbuka Uchaguzi Arumeru!

Nabii Flora wa Mbezi DSM ameumbuka Uchaguzi Arumeru!

Mwamakula

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2010
Posts
1,890
Reaction score
384
Nabii Flora Wa Mbezi Beach aliwambia Waandishi wa habari kuwa ameoteshwa na miungu yake kuwa Mgombea wa CCM Sioni Summari Mkwe wa Edward Lowassa atashinda uchaguzi mdogo Arumeru.Habari hiyo iliandikwa Front page kwenye gazeti la Uhuru!!Kutokana na ushindi wa Mgombea wa Chadema Arumeru ni dhahiri kuwa Nabii Flora ni nabii wa uongo na tapeli!!!Hata hivyo juzi baada ya kutoa utabili huo alijitikeza kwenye vyombo vya habari na kusema kuwa ameombea watu UKIMWI na tayari watu 40 wamepona na kuthibishwa na madaktari. Tangazo hilo lilitolewa kwenye gazeti la tanzania Daima .
 
[h=2]Nabii Flora[/h] Wednesday, December 7, 2011
Nabii Flora akiwa kanisani kwake

Akimtabiria mtu

[h=3]Hivi karibuni jijini Dar es salaam kuna nabii mwingine mpya ambaye amekuwa maarufu kutokana na wingi wa watu wanaohudhuria kanisani kwake na kupata huduma za kiroho. Anajulikana kwa jina maarufu kama Nabii Flora, watu wamekua wakiongelea kazi na shuhuda zinazotokea mahali anapohudumu, kwamba watu wanaponywa magonjwa yote sugu, vipofu wanaona, uvimbe na kila aina ya magonjwa na matatizo mbalimbali.[/h] [h=3]Mwaka 2011 pamekua na makanisa mengi ambayo watu wanakimbilia kupata huduma za kiroho na kimwili. Na Nabii Flora ni mmoja wa manabii ambaye amefanikiwa kupata watu wengi.[/h]

​
 
Nabii Flora (aliyeshika maiki) akiendesha maombezi kwa wenye matatizo.
Watu wenye matatizo wakishiriki maombi ya kuponywa kanisani kwa Nabii Flora.
WATU wengi wamekuwa wakifurika kutafuta uponyaji kwa njia ya maombezi kutoka kwa Nabii Flora ambaye mashuhuda wanasema anaponya magonjwa mbalimbali kama vile Ukimwi, kansa, kupoteza fahamu, magonjwa ya moyo, upofu, ulemavu na kadhalika.

Maombi hayo yaendeshwa na Nabii Flora huko Mbezi Beach maeneo ya Tangi Bovu jijini Dar es Salaam ambapo watu wenye kufuata huduma hiyo wamekuwa wakiwasiliana naye kwa kutumia namba za simu 0657 442699.

Zifuatazo ni picha zaidi za uponyaji katika kanisa la Nabii Flora:
 
Mhhh,.Kweli tunahitaji Roho wa Mungu kuwatambua wa ukweli na uongo.Na hii miujiza inachanganya watu sana.
Kazia maombi ZD vinginevyo utaliwa sadaka tu...
Wenzio wanang'ara kama hivyo na mkorogo
 
Dini ni biashara inayolipa ile mbaya. Mikoa kama Mbeya, makanisa yaeanziswa kila mtaa, yapo mengi kama baa. Je unakumbuka vikombe vya mwaka jana? Watanzania ni wadanganyika. Wanasiasa wanatudanganya, viongozi wa duni wanatudanganya, wazungu wanatudanganya, watu walitaka kwenda kuhubiri bila visa wala pasport.... Nasema tena, ipo siku watu watchomewa ndani kama alivyofanya Kibwetele wa Uganda.
 
MATAYO 7: 21-23
21
Si kila aniambiaye, Bwana, Bwana, ataingia katika Ufalme wa mbinguni; ila ni yule tu anayetimiza mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. 22 Wengi wataniambia Siku ile ya hukumu: Bwana, Bwana! kwa jina lako tulitangaza ujumbe wako, na kwa jina lako tuliwatoa pepo na kufanya miujiza mingi. 23 Hapo nitawaambia: Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni mbele yangu, enyi watenda maovu.
 
kama huyu ndio wa christ embassy basi kwishnei, ni moja ya makanisa yasiyo na nidhamu, kanisani ni full vimini na disco la yesu!
 
itakuwa hao mungu wake ni sawa na wale wa majimarefu,alaf Arusha haitabrki kama tanga bana,sisi tuna MUNGU wao wana pesa na mamiungu mia
 
Sipati picha nabii wa kike halafu bomba hivyo. Halafu namuwazia jinsi anavyokunjwa usiku na jamaa sipati picha.
 
haahahahhaha, daaah lengo si kwamba nilitaka cheka lakini weakness kubwa ya uoga wa mtanzania ni kifo. Babu wa loliondo aligundua hilo naye akajichotea maela sa hivi ametulia.
Kila kukicha manabii wapya wanaibuka na makanisa mapya.
Swali la kujiuliza ina maana kabla ya hawa manabii wa makanisa ya leo watu wote walikuwa wamepotoka au walikuwa katika madhehebu ya shetani.


Cowards die many times before their
deaths.
The valiant never taste of death but once.
Of all the wonders that I yet have heard,
It seems to me most strange that men
should fear, Seeing that death, a necessary end,
Will come when it will come.
 
Mbona nabiii mwenyewe kurumbembe?? uso fanta mikono pepsi..kajiparua hivo gubeli hana lolote..
 
HIYO NI MIUNGU NDIYO ILIYOMWOTESHA NA SI MUNGU( JEHOVA) WA MBINGUNI. TUNASHUKURU KWAMBA PAMOJA NA UOZO WA CCM KUENDELEA KUFUNULIWA, MUNGU PIA ANAENDELEA KUTUFUNULIA AKINA NANI SIYO WATUMISHI WAKE ILA WANATUMIKIA MATUMBO YAO KWA KIVULI CHA MUNGU- roho wa Manabii wa kweli daima huongozwa na Mungu na siyo misisimuko ya posho toka kwa watu
 
Nabii Flora

Wednesday, December 7, 2011
Nabii Flora akiwa kanisani kwake

Akimtabiria mtu

Hivi karibuni jijini Dar es salaam kuna nabii mwingine mpya ambaye amekuwa maarufu kutokana na wingi wa watu wanaohudhuria kanisani kwake na kupata huduma za kiroho. Anajulikana kwa jina maarufu kama Nabii Flora, watu wamekua wakiongelea kazi na shuhuda zinazotokea mahali anapohudumu, kwamba watu wanaponywa magonjwa yote sugu, vipofu wanaona, uvimbe na kila aina ya magonjwa na matatizo mbalimbali.

Mwaka 2011 pamekua na makanisa mengi ambayo watu wanakimbilia kupata huduma za kiroho na kimwili. Na Nabii Flora ni mmoja wa manabii ambaye amefanikiwa kupata watu wengi.


​

Ameolewa? Mbona kajichubuka kama shankupe fulani hivi!!!!!!!!!
 
Huyo siyo Nabii wa YESU.
Itakuwa ana roho ya kuzimu na uzima hauko ndani yake,kwa sababu neno la Mungu halimo kwake.Ananena yaliyo ya kwake si ya YESU.
 
wakati mwingine nakosa la kuchangia tehe.....tehe.... kalolite
 
Nabii Flora Wa Mbezi Beach aliwambia Waandishi wa habari kuwa ameoteshwa na miungu yake kuwa Mgombea wa CCM Sioni Summari Mkwe wa Edward Lowassa atashinda uchaguzi mdogo Arumeru.Habari hiyo iliandikwa Front page kwenye gazeti la Uhuru!!Kutokana na ushindi wa Mgombea wa Chadema Arumeru ni dhahiri kuwa Nabii Flora ni nabii wa uongo na tapeli!!!Hata hivyo juzi baada ya kutoa utabili huo alijitikeza kwenye vyombo vya habari na kusema kuwa ameombea watu UKIMWI na tayari watu 40 wamepona na kuthibishwa na madaktari. Tangazo hilo lilitolewa kwenye gazeti la tanzania Daima .

Paulo alipofika Efeso alikuta kuna mungu mke anaitwa Artemi
Hawa manabii waoteshwa na mungu yupi ni swali la kujiuliza maana Mungu wa kweli hasemi uongo
 
Back
Top Bottom