Nabii Flora wa Mbezi DSM ameumbuka Uchaguzi Arumeru!

Nabii Flora wa Mbezi DSM ameumbuka Uchaguzi Arumeru!

Napata taabu wana jf wenzangu. Naomba mwenye kujua anielimishe. MANABII wanapatikana vipi? Nini sifa za kuwa nabii? Je zinaweza kuwa verified kwamba ukimwona tu unajua kwamba ni nabii(na mtume).
Ni kwa nini manabii na mitume wengi wako Dar? Mwingira, Ferbandes kuwataja wachache.

Kama kuna nabii au mtume anapita hapa jf atufafanulie.
 
Haya siyo maneno yangu ni kutoka kwenye BIBLIA....

Mathayo 24:4, 5, 24-26 "
4-5:Yesu akajibu, akawaambia angalieni mtu asiwadanganye. Kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu wakisema, Mimi ni Kristo; nao watadanganya wengi.
24-26 Kwa maana watatokea wakristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule. Tazama, nimekwisha kuwaonya mbele. Basi wakiwaambia yuko jangwani, msitoke; yumo nyumbani, msisadiki."

2Wakorintho 11:4, 13-15 "
4; Maana yeye ajaye akihubiri Yesu Mwingine ambaye sisi hatukumhubiri, au mkipokea roho nyingine msiyoipokea au injili nyingine msiyoikubali mnatenda vema kuvumilia naye."
13-15 "Maana watu kama hao ni mitume wa uongo, watenda kazi kwa hila, wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa Kristo. Wala si ajabu. maana shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru. Basi si neno kuwa watumishi wake nao wakijigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki, ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao."

Shida ya wapendwa wengi sio wasomaji wa Bibilia (neno la Mungu) na wanajikita sana kuona miujiza ikitendeka Kitu ambacho Bwana Yesu alikikemea kwa nguvu zote. Sio wengi wenye uwezo wa kutofautisha kazi za Mungu na za shetani. wengi hupenda kusomewa mistari ya biblia na watumishi na kuomba hata kufunga bila kuwa na dhamira ya kweli moyoni ndiyo maana idadi kubwa ya watu wa aina hiyo ni vigumu sana Mungu kudhihirika katika mahitaji yao.
 
Mahaba ya kimagamba yanawaponza hawa matokeo yake ni aibu, sijui atawaambia nini waumini aliowaongopea wamwaelewe.
 
Hahahaha huyo naye anajiita Nabii? Astaghfirlulah kuna watu kwa kufuru!

Akipita mitaani akisikia Psiiiiiiiiii nyingi asishangae...
 
Jamani, Biblia imefungwa haiongezwi wala haipunguzwi kitu, manabii wote wameandika unabii wao kwenye hicho kitabu takatifu, Hivi hawa wanaojiita manabii wanataka unabii wao uandikwe wapi?:rockon:

Hivi siyo kweli kwamba biblia hiyo hiyo inataja huduma 5 zinazoukamilisha mwili wa kristu,kwa kutaja huduma moja moja ni 1.Wachungaji 2.Manabii 3.Wainjilisti 4.Waalimu 5.Mitume.Mwili wa kristu ni kanisa hivyo Yesu anatuambia huduma hizi ndiyo zinazolikamilisha kanisa ambaye ni yeye mwenyewe.Kama kuna kanisa basi kunapaswa pia kuwa na huduma hizo tano ni sawa na mwili wako ili uwe wewe unahitaji kuwa na kichwa,mikono,kiwiliwili na Miguu.Sasa bila kuwa na hizo five fold Ministry mwili wa Kristu haujakamilika. Kwani kanisa limefungwa pia halipo baada ya kukamilika biblia?? Kama ambavyo kanisa halijafungwa yaani Mwili wa Kristu upo na unaendelea kuwepo na viungo vya mwili wake yaani huduma hizo tano nilizozitaja pia hazijafungwa.

Biblia inazungumza/inatabiri kuhusu kuja/kuwepo Manabii wa Uongo,hawa walikuwepo mmojawapo ni Balaam na watakuwepo hata leo. Siyo tu Manabii wa uongo bali hata wanaojiita watumishi wa Mungu lakini hawamtumikii Mungu bali shetani.

Ni vizuri kulisoma neno la Mungu ili Roho mtakatifu atufunulie/ajifunue kwetu na tuweze kulielewa vizuri neno la Mungu badala ya kuwa washabiki (fans). Yesu anataka tuwe wafuasi/wanafunzi/disciples na siyo mashabiki/fans. Kama hujui neno la Mungu usidakie mambo usiyoyajua.

Ni vizuri tu kuto-comment na kuitafuta kweli ndani ya biblia badala ya kuchangia usichokijua! Ndiyo maana maandiko yanasema Utaijua kweli na kweli itakuweka huru kinyume cha hapo neno la Mungu linasema utaangamia "Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa". Huwezi kulijua neno la Mungu kwa kusimuliwa kama hadithi bali kwa kulisoma ukiongozwa na Roho Mtakatifu

Mungu akupe hamu na kiu ya kuwa msomaji wa Neno maana Neno ni Mungu mwenyewe.
 
Manabii wa siku hizi wanajikoboa? anyway mkimuona muulizeni kama yeye ndiye yule wa kwenye maandiko au tusubiri mwingine?
 
Jamani waumini wanaoongozwa na nabii Flora, mbona hamumtetei nabii wenu? Mlikula pamoja nae, aliwaponya UKIMWI, kisukali, n.k. Leo hii anasimangwa nabii wenu, mmekaa kimya. Au nd'o ile ya kumpiga mchungaji na kondoo wake kutawanyika?
 
Nabii mganga njaa huyo wizi mtupu
 
Kwenye maandiko ya dini zote tulishaambiwa watakuja manabii wa uongo, na ndio hawa tunawaona.
 
Nabii Flora

Wednesday, December 7, 2011
Nabii Flora akiwa kanisani kwake

Akimtabiria mtu

Hivi karibuni jijini Dar es salaam kuna nabii mwingine mpya ambaye amekuwa maarufu kutokana na wingi wa watu wanaohudhuria kanisani kwake na kupata huduma za kiroho. Anajulikana kwa jina maarufu kama Nabii Flora, watu wamekua wakiongelea kazi na shuhuda zinazotokea mahali anapohudumu, kwamba watu wanaponywa magonjwa yote sugu, vipofu wanaona, uvimbe na kila aina ya magonjwa na matatizo mbalimbali.

Mwaka 2011 pamekua na makanisa mengi ambayo watu wanakimbilia kupata huduma za kiroho na kimwili. Na Nabii Flora ni mmoja wa manabii ambaye amefanikiwa kupata watu wengi.


​

Nabii gani mikorogo kibao na makarolight kibao..Mwiziiiiiiiiiiii huyoooooooooooooooooooo
 
Nabii Flora Wa Mbezi Beach aliwambia Waandishi wa habari kuwa ameoteshwa na miungu yake kuwa Mgombea wa CCM Sioni Summari Mkwe wa Edward Lowassa atashinda uchaguzi mdogo Arumeru.Habari hiyo iliandikwa Front page kwenye gazeti la Uhuru!!Kutokana na ushindi wa Mgombea wa Chadema Arumeru ni dhahiri kuwa Nabii Flora ni nabii wa uongo na tapeli!!!Hata hivyo juzi baada ya kutoa utabili huo alijitikeza kwenye vyombo vya habari na kusema kuwa ameombea watu UKIMWI na tayari watu 40 wamepona na kuthibishwa na madaktari. Tangazo hilo lilitolewa kwenye gazeti la tanzania Daima .

Yuko sawa kabisaaaa, alioteshwa na miungu na siyo MUNGU.

MUNGU ndo pekee anayeweza kukupa maona na yakawa KWELI, lakini si miungu.

"...si kila aliitaye JINA la BWANA ataurithi UFALME wa MUNGU..." Kina Kibwetere hata hapa TZ wapo hasa kule CCM.

 
Nabii Flora Wa Mbezi Beach aliwambia Waandishi wa habari kuwa ameoteshwa na miungu yake kuwa Mgombea wa CCM Sioni Summari Mkwe wa Edward Lowassa atashinda uchaguzi mdogo Arumeru.Habari hiyo iliandikwa Front page kwenye gazeti la Uhuru!!Kutokana na ushindi wa Mgombea wa Chadema Arumeru ni dhahiri kuwa Nabii Flora ni nabii wa uongo na tapeli!!!Hata hivyo juzi baada ya kutoa utabili huo alijitikeza kwenye vyombo vya habari na kusema kuwa ameombea watu UKIMWI na tayari watu 40 wamepona na kuthibishwa na madaktari. Tangazo hilo lilitolewa kwenye gazeti la tanzania Daima .

Hivi kumbe kuna nabii mwanamke? Lakini sidhani kama amekosea kwenye red hapo panaonesha kuwa alioteshwa na Miungu yake na siyo Mungu, hivyo basi miungu kamwe haiwezi kushindana na Mungu. Mwisho wa siku nguvu za Mungu zimeshinda. Nabii kajichubua? Amekua kama jini
 
guys idont understand huyu jesus jehova anayetaniwa ivi na wanadam yupo dini ipi huu ni utani sasa
 
Jamani waumini wanaoongozwa na nabii Flora, mbona hamumtetei nabii wenu? Mlikula pamoja nae, aliwaponya UKIMWI, kisukali, n.k. Leo hii anasimangwa nabii wenu, mmekaa kimya. Au nd'o ile ya kumpiga mchungaji na kondoo wake kutawanyika?

Nabii????? Kwa jinsi alivyo na anavyotumiwa na ccm nadhani amerithi nafasi ya sheikh Yahya
 
Ee Mungu wetu uliyehai tuwezeshe kuwatambua manabii wa uwongo na tuwakimbie kabla hawaja maliza kidogo tulichobakinacho baada ya kile kingi kuporwa na akina "Kaisali/ri". Ameni
 
Hakuna nabii anayejipaka mkorogo,huyu ni kibwetere wa kike,anaganga njaa-nawhurumia waumini wanaompelekea hela ya mkorogo,lakini baba wa taifa aliwahi kusema: "kama kuna mtu anataka kubebwa na wako watu wamekubali kumbeba waacheni..." waacheni hao waumini wamchangie vijisenti ila asijifanye mtabili wa mambo ya siasa ,hana karama hiyo.Pia atafute mume aolewe.
 
Back
Top Bottom