Nabii Flora Peter wa Mbezi Beach...

Nabii Flora Peter wa Mbezi Beach...

Ni kweli mtumishi huyu anatumia mafuta ya mzaituni tokea Israeli? Ni kweli mtumishi uyu anatumia sabuni? kuwapa watu? vizuri umejitokeza hapa kusema unamfahamu mtumishi uyu! je kabla ya utumishi alikuwa wap anafanya nn? huduma ya utumishi wake ilianza lini kabla ya kuanzisha kanisa lake? mbezi? huko kigamboni alikuwa mtumishi kanisa gani? kutokana na watu kuwa na hofu ya kwamba siku za mwisho kutakuwa na manabii wengi wa uongo! kufuata mafuta yaliyopo kwa mafuta kwa mtumishi kwangu mimi sio dhambi! maana watu walimtafuta Yesu popote alipo! na ni kweli ufalme wa Mungu hutekwa na wenye nguvu.

Sina nia ya kumnyooshea kidole wala kumsema vibaya! ila nina maswali yangu naamini wengine pia wanayo! naamini mti wenye matunda unapigwa mawe na watu wabaya na watu wazuri tena! pengine ni kitu kigeni sana! hapa Tz kuona nabii mwanamke mwenye mafuta! tukirudi kule juu Mungu alisema tuichunguze kila roho! kabla ya kuiamini naamini pia si dhambi! ivyo kwa maneno hayo! je wewe mwenyewe binafsi kabla ya kuombewa na kufanikiwa je ulishachunguza ukajidhiririsha mtumishi uyu roho inayofanya kazi ya miujiza au uponyaji kweli ni ya Mungu?

kwann kumekuwa na negative sana kuusu uyu Mama nabii? tungejua historia ya mama huyu pengine ingesaidia kuondoa uzushi uliopo? watu wanamshutumu juu ya ngozi yake ya uso! wanamshutumu juu ya nguvu za kuponya na miujiza si za Mungu aliyehai! je ni sababu ya ngozi yake ya uso? je ni sababu anavyovaa! naamini sijaingia katika kumnyoshea kidole nipo katika ile inaitwa " zichunguzeni kila roho" kuna huduma moja ambayo anayo huyu mama ya "delivarence kwa kutumia damu ya Yesu" makanisa mengi yanajua lakini mengi hawayatilii maanani instead wanaanza kuombea kwanza kabla ya vifungo vyote vya nyuma kuachia! je ndo sababu ya kufanikiwa maombi yake! embu endelea kufunguka mdau!

Kila kitu kizuri kinatoka kwa MUNGU,na si kila miujiza inatoka kwa Mungu, tunaambiwa kuna baraka ambazo watu uomba na kupitia malaika baraka hizo zinapokuwa zinashushwa ,shetani naye humvizia malaika aziletaye ana weekness gani,na hizo weekness hutokana na Yale maombi ya kukatisha katisha yasiyo na msimamo na mwendelezo ambayo mwombaji hukata tamaa au vikwazo vingi kumkuta na shetani akifanikiwa kupata baraka hizo ndo uenda kuwagaia watu wake waganga na wale manabii Wa uongo ndo maana hata watu hupata watoto kwa hao hao waganga, Watu wanahimizwa kuomba roho mtakatifu awaongoze kuwatambua watu hawa,
 
Ninamjua Huyo MTUMISHI Wa Mungu Tokea Akiwa Kigamboni, Kisha Kwa Mzee Willy Pale Mbezi Beach Maguruwe Na Mpaka Alipoanzisha Kanisa Lake Salasala.

NINAMKUBALI 100% Kwani MAFANIKIO Yake KIMAOMBI Ni MAKUBWA Na Hayaelezeki Na Tokea NIMFAHAMU Sijawahi Kuona Mtu AKIENDA KWAKE NA ASIFANIKIWE. Lakini Pia TUSISAHAU Kuwa Dini Pia Ni IMANI Ya MTU Na Jinsi UNAVYOJIACHIA Kwa Mwenyezi Mungu au Yesu Kristo.

Kwa Mfano UNAKUTA MTU ANAENDA KUOMBEWA LABDA APATE MUME NA MTUMISHI WA MUNGU AKIMWOMBEA NA KUMTAKA AACHANE NA UMALAYA YEYE AKIRUDI TU KITAA MWENDO NI MDUNDO KWA WAUME ZA WATU Je Hapo UNATEGEMEA NINI MKUU?

Nabii Flora Peter Ni MTUMISHI Wangu Na Namkubali Hadi Sijui Nisemeje Na Nahisi Nina DENI La Kumlipa Kwa Maombi Yake Ya UHAKIKA Kwangu Na Jinsi Mambo Yangu Yanavyozidi KUNYOOKA.

Najisikia Mwenye Furaha Mno KUSALI Kwa Nabii Flora Peter Na Nichukue Nafasi Hii Murua Kuwakaribisheni Na Wengine Wote Ambao Mna IMANI HABA. Mtasikia Mengi Na Mtadanganyana Sana ILA Ushuhuda Wa Maombi Ya Nabii Flora Peter HAUELEZEKI.

Namalizia Kwa Kusema " Kwa Msaada Wa Mungu Tutatenda Makuu Kwa Maana Bwana Atawakanyaga Watesi Wetu Zaburi 60:12 Na 108:13 ".

Kama na wewe umeokoka basi unawadanganya wengi... Mbona post zako humu hazina ushuhuda kuwa umempokea Bwana.
Sura na mwili wa huyo Mama alivoukoboa inakosoa uumbaji wa Mungu na si uahuhuda mzuri kwa waumini, biblia inakataza kuyakosoa maumbile ikiwa pamoja na rangi za asili alizoumbwa nazo mwanadamu.
 
Me nilisha enda sana kwenye maomb lkn siamin ile stika yenye picha yake anayouza 5000 et utembee nayo au uweke chin ya mto uilalie au uweke kwenye maj uwoge iyo iman sikubalian nayo kabisa na unabii naoutoa pia sikubalian nao

Uganga wa Kikiristo ?!?
 
kwa mda mrefu nimekuwa nikisikia kuusu nabii flora na mambo anayoyafanya! Kabla ya kumreccomand mtu aende, waliowahi kwenda embu tupe ushuhuda ipo miujiza kweli? Upo uponyaji kweli?

Je ipo katika misingi ya mungu wa mbinguni! Yani yule mungu wa meshack shedrack na abednego? Toa maoni bila kutukana huduma ya watu bila kumtukana mtumish uyo! Nataka expirience tuu kwa walioenda kama hujaenda usijeandika mungu akakulaani.
Je ni kweli anatumia sabuni iliyoombewa kama njia ya kuleta uponyaji na miujiza? Je anatumia mafuta ya mzaituni kutoka israeli kama njia ya kuleta miujiza na uponyaji?

Kwa wanaojua je sabuni kutumika kulete miujiza au uponyaji kuna mtu mwenye maelezo juu ya ufunuo huo! Ingawa si wa kwako ndio lakini unaweza kuelewa! Katika bible lakini.

ameolewa au bado bikra?
 
Mkuu akhsante kwa kuliona hili.Mimi binafsi sikuwa na shaka na huyu nabii mpaka pale nilipomsoma GENTA,nikaamini kabisa jinsi anavyoandika hapa JF,na uhusika wa huyo mama nabii katika maisha ya GENTA,napata mashaka sana ya uhalali wa huduma yake.

Ameolewa au bado bikra?
 

Attachments

  • image.jpeg
    image.jpeg
    110.5 KB · Views: 847
Mathayo 7
Msihukumu nanyi mtahukumiwa maana kiasi kilekile mnachohukumu ndicho kiasi hiko hiko nanyi mtapimiwa kuhukumiwa.

kuna laana katika
1.Kuhumu wenye haki
2.kunyooshea watumishi wa Mungu vidole
3.Mungu anamwita mtumishi wake katika hali yoyote
4.Mungu usifikiri hakuoni maovu yako, usifikiri hakujui anakujua lakini wewe hajakuhukumu lakini wewe unamuhukumu binadamu mwingine, unamfanya Mungu hana akili? hajui analolifanya?
5.Mungu kamwita jinsi alivyo ili Mungu ajitwalie utukufu wake. Yesu akasema sijaja kwa ajili ya wenye haki nimekuja kwa kwa ajili ya waliopotea ili wapate uzima na uzima tele! Mungu anaweza kukupa maradhi ya cancer ya ngozi ili ujue hapendi dhambi unayofanya. Mungu anaweza kukuparalizisha mkono wako unaoandika hapa. Mungu anaweza kukupa maradhi ya kujinyea na kujikojolea anaweza kuuwa anaweza kufufua! wewe ni nani binadamu unayejihesabia haki mbela ya Mungu? wewe ni mkuu kuliko Mungu wa majeshi? wewe ulimuumba Mungu au yeye alikuumba wewe? na unamhukumu binadamu mwenzako? unamfanya Mungu mjinga? Mungu alikosea kuumba? iyo akili nani kakupa? iyo afya unayoringia mpaka unamhukumu mwingine? unampangia Mungu nani amfanye mtumishi? mbona wewe mzima Mungu kakuruka kamfuata mtumishi wa Mungu? angalia Mungu asije kukuangamiza! Mungu anaweza kukufanya ombaomba maisha yako yakawa magumu! Na akafanya mlangowako kwa Nabii flora alafu ndio wa kukuombea sijui utaenda au utaendelea kumsema? Mungu anaweza kukupiga wewe unayemsema mtumishi wa Mungu alafu kwa makusudi mlango wa wewe kufungulia akaufanya kwa uyu mtumishi. kila mahali unapoenda Mungu hakufungui mpaka kwa uyu nabii sijui utafanyaje? Mungu anaweza kukuletea msiba kwako! anaweza kukutesa! ila anakuangalia tuu unahukumu binadamu mwenzako alafu unamtukana mtumishi wa Mungu. Goliath alikuwa na kiburi zaidi yako lakini Bwana wa majeshi alimpoteza kwa jiwe moja tuu, alijitapa kama wewe! alitukana kama wewe! alijiinua kama wewe! angalia hasira ya Mungu isije kukuangukia. siandiki kukutisha ila nakueleza ya kuwa Mungu hataki na hapendezwi! kujihesabia haki! angalia Mungu asiruusu jiwe lililopiga Goliath likupige na wewe.
 
Hata mm napata mashaka na huyu mama mtumishi utajikoboaje uso hivyo bahan, kwa jina la yesu napingana na nguvu yyte ya giza kutoka kwa huyu mtumishi, twasira yako ndo itatuonyesha kweli huyu mtumishi au njaa tu zinasumbua watu. Twendeni makanisani tuliko kulia kule kuna uponyaji wa kweli maana ni imani yako tu. tafakari
 
Nabiii,nabiii,nabiiii MUNGU atusaidie sana,NABIII ELIA WA KIPINDI KILEEE ALIFANYA NINI?
 
Back
Top Bottom