Nabii Flora Peter wa Mbezi Beach...

Nabii Flora Peter wa Mbezi Beach...

Ninamjua Huyo MTUMISHI Wa Mungu Tokea Akiwa Kigamboni, Kisha Kwa Mzee Willy Pale Mbezi Beach Maguruwe Na Mpaka Alipoanzisha Kanisa Lake Salasala.

NINAMKUBALI 100% Kwani MAFANIKIO Yake KIMAOMBI Ni MAKUBWA Na Hayaelezeki Na Tokea NIMFAHAMU Sijawahi Kuona Mtu AKIENDA KWAKE NA ASIFANIKIWE. Lakini Pia TUSISAHAU Kuwa Dini Pia Ni IMANI Ya MTU Na Jinsi UNAVYOJIACHIA Kwa Mwenyezi Mungu au Yesu Kristo.

Kwa Mfano UNAKUTA MTU ANAENDA KUOMBEWA LABDA APATE MUME NA MTUMISHI WA MUNGU AKIMWOMBEA NA KUMTAKA AACHANE NA UMALAYA YEYE AKIRUDI TU KITAA MWENDO NI MDUNDO KWA WAUME ZA WATU Je Hapo UNATEGEMEA NINI MKUU?

Nabii Flora Peter Ni MTUMISHI Wangu Na Namkubali Hadi Sijui Nisemeje Na Nahisi Nina DENI La Kumlipa Kwa Maombi Yake Ya UHAKIKA Kwangu Na Jinsi Mambo Yangu Yanavyozidi KUNYOOKA.

Najisikia Mwenye Furaha Mno KUSALI Kwa Nabii Flora Peter Na Nichukue Nafasi Hii Murua Kuwakaribisheni Na Wengine Wote Ambao Mna IMANI HABA. Mtasikia Mengi Na Mtadanganyana Sana ILA Ushuhuda Wa Maombi Ya Nabii Flora Peter HAUELEZEKI.

Namalizia Kwa Kusema " Kwa Msaada Wa Mungu Tutatenda Makuu Kwa Maana Bwana Atawakanyaga Watesi Wetu Zaburi 60:12 Na 108:13 ".
" ongea kwa sauti", ni maneno aliyomwambia muumini wake ili kuwahadaa waliohudhuria.
Sasa hivi kuanzisha kanisa ni sawa na kufungua Hardware, ni kupiga hela kwenda mbele kutoka kwa wajinga.Biblia wanazo lakini wanapotea.
Kwa nini nabii Flora anahamahama? Is she looking for greener pasture?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba nifunguliwe na nyie hapa swala la hawa manabii kutumia mafuta ,sijui maji ya upako ni sahihi?.
Na je lipo au lina mofano kibiblia??
 
Watu mnadanganywa na kupigwa pesa kama hamna akili. Yeyote aingie YouTube halafu aandike "Paramahasa Nithyananda~The Third eye." Huyo ni mwalimu wa kiroho huko India anawafundisha watu kuhusu "Jicho la tatu" na kuna kitu kinaitwa "Chakras na Kundalini" hayo masomo yanapatikana huko India wanawafundisha watu kujitambua na kuona mambo yaliyo fichika, na kushinda changamoto za Ulimwengu, ikiwemo kutabiri, kuona mapepo, kuponya magonjwa na mengine mengi. Elimu hiyo sasa hivi imeenea kote ulimwenguni, huku Africa tumelala Sana hatutaki kujifunza Acha tupigwe na makanjanja waliojitambua. Mtu akikutabiria tu eti tayari kawa nabii.
Wajinga ndio waliwao. Hata kuna threads kadhaa humu ziliwahi kuzungumzia kidogo elimu hii. Tafuta thread ya Pascal Mayalla #physic power (uwezo/ nguvu za kutenda miujiza.)
Jambo la kujiuliza, kwanini hawapendani na wakati wote wanahubiri Injili ya Kristo? Mwenye akili na afahamu. Wapi Nabii Elisha alimponda nabii Eliya? Wapi Nabii Yesu alimponda nabii Musa? Sasa tazama hawa Manabii wa sasa wanavyopondana kwenye makanisa yao kupitia mitandao ya kijamii, kila mmoja anamwita mwenzie feki yeye ndio Originally, hapo kama una akili timamu utagundua kuwa hamna kitu ila wanagombania tonge tu. Kama ni kweli wanamtangaza Yesu Kristo kwanini kwenye sticker zao wanaweka picha zao badala ya picha ya Yesu? Anae-promotiwa hapo ni Yesu au yeye mwenyewe? maana picha kwenye sticker anaweka yakwake. Nina mifano mingi tu.
Jamani mambo ni mengi muda ni mchache,,,
Ngoja ninywe chai ntaendelea wakati mwingine.
,,,,,very soon Nitakuja kuwaanika hao Manabii wenu feki
 
Back
Top Bottom