ninamjua huyo mtumishi wa mungu tokea akiwa kigamboni, kisha kwa mzee willy pale mbezi beach maguruwe na mpaka alipoanzisha kanisa lake salasala.
Ninamkubali 100% kwani mafanikio yake kimaombi ni makubwa na hayaelezeki na tokea nimfahamu sijawahi kuona mtu akienda kwake na asifanikiwe. Lakini pia tusisahau kuwa dini pia ni imani ya mtu na jinsi unavyojiachia kwa mwenyezi mungu au yesu kristo.
Kwa mfano unakuta mtu anaenda kuombewa labda apate mume na mtumishi wa mungu akimwombea na kumtaka aachane na umalaya yeye akirudi tu kitaa mwendo ni mdundo kwa waume za watu je hapo unategemea nini mkuu?
Nabii flora peter ni mtumishi wangu na namkubali hadi sijui nisemeje na nahisi nina deni la kumlipa kwa maombi yake ya uhakika kwangu na jinsi mambo yangu yanavyozidi kunyooka.
Najisikia mwenye furaha mno kusali kwa nabii flora peter na nichukue nafasi hii murua kuwakaribisheni na wengine wote ambao mna imani haba. Mtasikia mengi na mtadanganyana sana ila ushuhuda wa maombi ya nabii flora peter hauelezeki.
Namalizia kwa kusema " kwa msaada wa mungu tutatenda makuu kwa maana bwana atawakanyaga watesi wetu zaburi 60:12 na 108:13 ".