Naanzisha thread!

Naanzisha thread!

Sijali

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2010
Posts
2,700
Reaction score
1,857
Thread yenyewe ni mambo au vitu ulivyoviona/vijua ulipokuwa mdogo na sasa vimetoweka kabisa. Hii ni kwa sababu ya kujikumbusha, na pia kuwazindua wale waliokuwa bado hawajazaliwa. Naomba mwanzo uwe mwaka wa 1960. Wale wote waliozaliwa katika mwaka huo au baada ya mwaka huo waelezee mambo yaliyotoweka, mazuri na mabaya. Nadhani iko wazi sasa. Naanza....

Wakati nainukia miaka ya sabini, mambo haya na tabia hizi zilikuweko sasa hakuna tena.
1-Kulikuwa na viwarsha vingi vidogo vidogo mitaani: fundi cherahani, sonara, watengeneza sufuria, fundi viatu n.k.
2-Wake wengi wa nyumbani walikuwa hawaendi sokoni kwani vitu vilikuwa vinapitishwa mitaani na wafanyibiashara kama wauza samaki, mboga n.k.
3- Kulikuwa na waarabu tuliowaita washihiri. Hawa walikuwa wanatembeza nguo barabarani wakiuza (sasa ndio mabosi!)
4- Wahindi walikuwa wakijulika sana kwa viduka vya pembeni (corner shops) tukiwaita 'dukawalla' (hawakua na ubaguzi kama walionao sasa, kwani huwezi kumbagua mteja wako unayemtegemea kwa ulaji wako wa kila siku)
5-Wakati huo kuvaa shati au suruali iliyokwisha tengenezwa (ready made) ilikuwa jambo la aibu, mtu huchekwa kwa kuvaa 'tungua' (kwa vile mwuzaji huwa na fimbo ndefu ya kutungulia shati mahali lilipo). Nguo zilizothaminiwa ni zile zilizoshonwa na fundi cherahani!
6-Watu walikuwa wakiitana 'ndugu'
7- Dar kulikuwa na mabasi ya 'orofa' (double-deckers)
8- Kulikuwa na magari mengi ya ma-trailer yanayotoka Kenya kwenda Zambia
9-Kulikuwa na michezo iliyovutia maelfu kama East African Challenge Cup, mashindano ya mikoa ambapo Dar, Mwanza, Kilimanjaro na Tanga ilikuwa ikiwika sana. Wakati fulani fainali ilirudiwa kwa siku tatu ndipo alipopatikana mshindi!
10- Kulikuwa hakuna AIDS!

Sasa endelea.
 
- Kulikuwa na Volkswagen Kombi ambulance zenye rangi ya cream na taa ya bluu.

- Yalikuwepo magari ya ice cream yaliyokuwa yakipita mitaani huku yakipiga muziki na watoto tuliyafurahia sana.

- Vituoni (DSM) watu walikuwa wanapanda mabasi kw kupanga foleni na mabasi yalikuwa na Inspector kuhakikisha taratibu zote zinafuatwa.

- Kampuni ya UDA ilileta mabasi ya Icarus "kumbakumba" na kuna moja lilikuwa maarufu sababu lilipakwa rangi za pundamilia.

- Kulikuwa na maziwa fresh na mtindi ambayo yalikuwa kwenye pakiti zenye umbo la pyramid.

- Magari ya serikali yalikuwa Land Rover 109 mara nyingi zikiwa na rangi ya kijivu.

- Tulinunua sana viatu kwenye maduka ya Bora.

- Kulikuwa na baiskeli aina ya Swala zilizotengenezwa hapahapa nchini.

- Kulikuwa na nyama za kusindika kwenye makopo kama sikosei kutoka Tanganyika Packers.

Kumbukumbu nzuri kweli hizi!
 
Mbadala wa hayo yote siku hizi nini? vilikuwa na umuhimu wakati huo, siku hizi maendeleo au ulipendelea kuvaa kaniki? au ulipendelea ule ugali wa unga wa mahindi wa rangi ya yanga kama zamani? au unataka kusema nini kwamba hivyo vilikuwa bora kuliko vya sasa? nini hasa lengo la kutaka amoni yetu
 
No rememberance of those times, zaidi ya kua kulikua na shida sana kupata sukari, ukikutwa una kilo zaidi ya 10 at a time ni shida sana. lol
 
....Nakumbuka kipindi hicho namsindikiza Baba kwa Kinyozi... kinyozi walikuwa wanakaa kando ya barabara kwenye mti mkubwa au kivuli cha kueleweka.

Marazote nikisikiliza hii track, napata wazo la kuanzisha thread kama hii...

"Hey u know! Everybody is talkin about good old days ryt??,
lets talk about good old days uh...."

Thanks 'Sijali' kwa huu uzi.
 
Last edited by a moderator:
Kulikuwa na malori ya ushirika kama moretco,kitco, vyama vya ushirika vilifanya kazi sana.kulikuwa na maonyesho ya Sinema kila tarehe 15 ya mwezi,kulikuwa na redio moja tu ya taifa.Aliyesoma mpaka chuo kikuu alikuwa mungu mtu,kulikuwa hakuna shule za kata ,!
 
kulikuwa na bwana/bibi afya wanapita nyumba kwa nyumba kupuliza dawa za wadudu hata kwenye madimbwi barabarani
 
1. Kulikuwas hakuna Mobile phone.
2. Post Card zilikuwa dili.
3. Hakuna Facebook, Twiter wala JF.
4. Gazeti lilikuwa Mfanyakazi mengine yote Kimeo.
5. Sukari kwa foleni na ni kilo moja kwa wiki mgao na mpaka balozi athibitishe wewe ni mkazi wake.
6. Redio ilikuwa RTD, Kusikiliza MUsic mpaka vipindi vya mashirika , mfano, BP, Bwana Umeme, nk
7. Ulaya walikuwa wanakwenda MADINGI tu.
8. Mtilkila alikuwa juu na sera zake za *********.
 
ilikuwa siku ya kusoma bajeti watu wanajikusanya vikundi vikundi kusikiliza radio tz,
kuliwa na waranti kwa ajili ya wanafunzi wanaposafiri,
 
Kulikuwa na Senema za bure mnazi mmoja za Aspro kila tarehe 3 ya mwezi za Omo sikumbuki tarehe.
 
Kulikuwa hakuna kanda mbili (zimeadimika) tulilazimika kuvaa viatu vya matairi, ukirudi nyumbani utafute arita (sabuni ilikuwa anasa) kusuguwa miguu, inakuwa mieusi kwa mpira kubaki kwenye ngozi.
 
Mzee wa nyumba ya jirani unamheshimu kama mzazi wako
kwenda shule inabidi ufunge safari
vyakula vingi vya kiasili na vilikuwa poa sana
 
Dawa za meno za kichina zikiitwa Maxim ukipigia mswaki asubuhi husikii ladha ya chakula kutwa nzima. Ukiletewa zawadi ya Colgate kutoka Kenya unaona kama umeletewa kitu cha ajabu na unaiminya kiduuchu kutia kwenye mswaki isiishe haraka, hujui lini utaipata tena.
 
Huyu wa 90's kawani haya Matrailer yalikuwa sooo! yakiingia kituoni ni full kukomba hawaachi kitu!

Hata kama nikiwa wa 20's so what??
Ok tufanye we ulikuwa wa 18th C, haya tukumbushe vita kuu za dunia....
Haya sio majukwaa ya kuumbuana tu mkuu, we toa kumbukumbu zako sepa.
 
Thread yenyewe ni mambo au vitu ulivyoviona/vijua ulipokuwa mdogo na sasa vimetoweka kabisa. Hii ni kwa sababu ya kujikumbusha, na pia kuwazindua wale waliokuwa bado hawajazaliwa. Naomba mwanzo uwe mwaka wa 1960. Wale wote waliozaliwa katika mwaka huo au baada ya mwaka huo waelezee mambo yaliyotoweka, mazuri na mabaya. Nadhani iko wazi sasa. Naanza....

Wakati nainukia miaka ya sabini, mambo haya na tabia hizi zilikuweko sasa hakuna tena.
1-Kulikuwa na viwarsha vingi vidogo vidogo mitaani: fundi cherahani, sonara, watengeneza sufuria, fundi viatu n.k.
2-Wake wengi wa nyumbani walikuwa hawaendi sokoni kwani vitu vilikuwa vinapitishwa mitaani na wafanyibiashara kama wauza samaki, mboga n.k.
3- Kulikuwa na waarabu tuliowaita washihiri. Hawa walikuwa wanatembeza nguo barabarani wakiuza (sasa ndio mabosi!)
4- Wahindi walikuwa wakijulika sana kwa viduka vya pembeni (corner shops) tukiwaita 'dukawalla' (hawakua na ubaguzi kama walionao sasa, kwani huwezi kumbagua mteja wako unayemtegemea kwa ulaji wako wa kila siku)
5-Wakati huo kuvaa shati au suruali iliyokwisha tengenezwa (ready made) ilikuwa jambo la aibu, mtu huchekwa kwa kuvaa 'tungua' (kwa vile mwuzaji huwa na fimbo ndefu ya kutungulia shati mahali lilipo). Nguo zilizothaminiwa ni zile zilizoshonwa na fundi cherahani!
6-Watu walikuwa wakiitana 'ndugu'
7- Dar kulikuwa na mabasi ya 'orofa' (double-deckers)
8- Kulikuwa na magari mengi ya ma-trailer yanayotoka Kenya kwenda Zambia
9-Kulikuwa na michezo iliyovutia maelfu kama East African Challenge Cup, mashindano ya mikoa ambapo Dar, Mwanza, Kilimanjaro na Tanga ilikuwa ikiwika sana. Wakati fulani fainali ilirudiwa kwa siku tatu ndipo alipopatikana mshindi!
10- Kulikuwa hakuna AIDS!

Sasa endelea.

Nakupongeza sana kwa hii mada. Ni wengi hawajui wapi tumetoka, leo wanakuta ma laptop, mitandao, simu za mikononi, gari nzuri nzuri, ni vyema hapa tukipata wakumbusha au kuwafunda tulipotokea labda watakuwa na mtazamo mwingine katika hii dunia. Vijana kumbukeni, wazee wenu wametoka mbali sana na kukumbana na mengi mpaka leo mkaiona hii nchi kama hivi ilivyo ni neema kubwa sana ambayo inabidi muilinde na kuitunza, endeleeni katika hii mada bila kukwaruzana, kila mmoja ana fursa ya kusema yaliomkuta, yaliokuwepo kwa wakati wake.

Nakupa pongezi mleta mada. Mcheza kwao hutunzwa, chukulia hii kama tunzo kwako.
 
Sigara zikiitwa Kali na Baridi. Hazikuwa na filter. Au bado zipo??
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom