Naanzisha thread!

Kwa wale wapenzi wa kandanda aka soka,vilabu vilivyotamba enzi hizo pamba-mwanza,majimaji-songea,cda-dodoma,reli-moro-kigoma,ushirika-moshi,africansport-tanga,sunderland(simba)-dar, etc pamoja na timu nyingi tu zilizokuwa zinamilikiwa na halmashauri za wilaya mbalimbali pamoja na mashirika,zilikuwa za ukweli..japo kwa uchache,na kulikuwa na maplayer wa ukweli,kweli old is gold alwayz
 
tulikuwa tunacheza uki, kiboleni, rede, kombolela, mdako na kusikiliza radio TZ mama na mwana.

ukimuona mtu mkubwa anakuja na mzigo lazima umpokee, mtoto alikuwa ni wa wote akikosea naadhibiwa na yeyote mkubwa,

Tulikuwa tunakimbia mchakamchaka asubuhi kabla ya kuingia darasani

Siku hizi watoto ni kwenye kideo tu, hakuna kuchezea mavumbi labda wale wa vijijini.
 
Nakupongeza sana kwa hii mada. Ni wengi hawajui wapi tumetoka, leo wanakuta ma laptop, mitandao, simu za mikononi, gari nzuri nzuri, ni vyema hapa tukipata wakumbusha au kuwafunda tulipotokea labda watakuwa na mtazamo mwingine katika hii dunia. Vijana kumbukeni, wazee wenu wametoka mbali sana na kukumbana na mengi mpaka leo mkaiona hii nchi kama hivi ilivyo ni neema kubwa sana ambayo inabidi muilinde na kuitunza, endeleeni katika hii mada bila kukwaruzana, kila mmoja ana fursa ya kusema yaliomkuta, yaliokuwepo kwa wakati wake.

Nakupa pongezi mleta mada. Mcheza kwao hutunzwa, chukulia hii kama tunzo kwako.
Ni kweli dada, ila pia kuna vitu vingine vimepotea na hii ni mbaya kwa community. Najua nitasemwa kwa post hii ila ukweli ni kwamba zamani kulikua na control kubwa zaidi ya state over trade and the economic sector in general. na hii ilikua inasaidia sana watu wa vijijini ku-access first necessity goods kwa bei nafuu (or at least affordable) na general discipline od the economic sector ilikuwepo (sio agressive competitions we have today). Kwa kifupi kuna vitu tunashukuru kua navyo leo ila pia kuna vitu muhimu tunavimiss leo
 
Hayo ni kweli kabisa.
 
Kulikuwa na kamata kamata ya wasiolipa kodi yaani ilikuwa
ni udhalilishaji maana walikuwa wanasombwa kwenye karandinga
kama wezi!
 
7- Dar kulikuwa na mabasi ya 'orofa' (double-deckers)
ivi vitu vilikueoko miaka ya ngapi??????????? mana loh!
 
shikamooni wazee mnaojifanya dot com wenzetu..
Hebu uwe na heshima ya kweli wewe unafikiri sisi ni kama
wewe? we umewahi kutumia simu ya kuzungusha huongei
na mtu mpaka apokee operator wa posta na simu kwanza?
hapo ndo umwambie unataka kuongea na nani!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom