ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 43,898
- 50,629
Sasa wewe unadhani yeye hajui.inachoongea? Hao wanaoutwa wateule hakuna Cha maana wanafanya kumsaidia Rais ndio maana kampa Rungu Makonda.Mawaziri na watendaji wanaolalamikiwa ni wateule/waajiriwa wa serikali ya CCM. Chama kimejaza mawaziri na bureaucracy kubwa serikalini. Hiyo ndiyo maana sahihi ya chama kuwa kazini; ndivyo chama kinavyodhibiti na kusimamia serikali. Kawaida, si sahihi kwa viongozi wa chama (except Rais) kuwa na mawasiliano ya moja kwa moja ya kikazi na watendaji wa serikali bali kupitia wateule wake wa kisiasa serikalini (mawaziri, RCs, DCs, etc.) nje ya ofisi za umma.
May seem complicated to many lakini huo ndio usahihi wenyewe.
Sasa hii ya Katibu Mwenezi wa CCM kutembea na misafara mikubwa na kuitisha mikutano ya hadhara yenye gharama kubwa kusikiliza malalamiko ya individuals dhidi ya viongozi na watendaji wa serikali ya CCM, ni ufujaji mkubwa wa hazina ya taifa usiokuwa na tija yoyote zaidi ya kupeana faraja ya kisaikolojia kwa watu wenye uwezo mdogo sana wa kufikiri.
Tumuone Sasa wa kumbishia