Naamini kwa dhati kabisa nguvu ya Makonda haitokani na kuwa kwake katibu mwenezi wa CCM, lazima kuna chanzo kingine kinampa kujiamini kiasi hiki

Niite jina lolote, lakini mimi ni mojawapo ya watu ambao huwezi hata kabisa kunishawishi kwamba hii nguvu na mbwembwe ambazo Makonda amekuwa akizionyesha zinatokana na kuwa kwake na cheo cha katibu mwenezi wa CCM. Tusidanganyane hapa.

Makonda sio katibu mwenezi wa kwanza CCM, na wamekuwapo wengine huko nyuma, lakini ni mara ya kwanza tunapata katibu mwenezi wa CCM ambae anaonyesha kujiamini kupita mamlaka yanayostahili ya katibu mwenezi wa CCM.

Leo hii katibu mwenezi awapigie simu mawaziri, amkebehi mwanasheria mkuu wa serikali, awaamrishe wakuu wa mikoa, ma-RPC, eti kwa sababu yeye ndie msemaji mkuu wa chama, hilo tu? Haiwezekani.

Leo hii katibu mwenyezi apewe bajeti, misafara ya magari, kuliko inavyokuwa kwa makamu mwenyekiti wa CCM au katibu mkuu wa CCM, kwa sababu gani? Kwamba katiba ya CCM imebadilishwa kisiri na hawa wote wameambiwa kuanzia sasa bosi wenu ni katibu mwenezi wa CCM? Pamoja na mawaziri? Wakuu wa mikoa? Mwanasheria Mkuu? Wenyeviti wa CCM wa mikoa?

Sote tunajua msemaji mkuu wa chama chochote anasema yale chama kilichoamua katika vikao vyake rasmi. Kuwa msemaji wa chama haina maana wewe ndio unakuwa unakisemea chama, hata siku moja. Kuwa katibu mwenyezi sio katika mpangilio wa vyeo vya chama, ni nafasi tu. Huwezi hata kusema katibu mwenezi wa CCM ni mkubwa kuliko mwenyekiti wa CCM wa mkoa. Lakini sio hivyo kwa Makonda. Yeye amejipa madaraka ambayo nadhani yanazidi hata ya kuwa makamu mwenyekiti wa CCM, au katibu mkuu wa CCM. Kujiamini huko kunatoka wapi? Mamlaka haya yanatoka wapi? Kwamba siku zote hatukujua kuwa katibu mwenezi wa chama ni mtu mkubwa namna hii? Ni kweli?

Nyie watu wa CCM, nyie mawaziri, nyie wakuu wa mikoa, tuambieni ukweli. Kinachowafanya muufyate Makonda akiunguruma ni nini hasa, Ukatibu mwenezi wa CCM? Na kwa nini sasa wenye akili tukiwauliza mbona mambo yako hivi, mnaishia kutabasamu tu bila kusema lolote? Kuna kitu gani msichotuambia?

Na niwaambie wazi nyie watu wa CCM. Kama nguvu ya Makonda sio ya kikatiba ndani ya CCM, kama kuna chanzo kingine kisicho rasmi kinampa nguvu na kujiamini kiasi hiki, basi anguko la CCM liko karibu sana!
Nikuambie tu Paul Makonda siyo mtu wa kawaida. Nafasi ya sasa ni ndogo kuliko yeye. Muda utaongea! Hata alipokuwa mkuu wa mkoa Dar ilikuwa kama yeye ndiyo prime minister. Jamaa ni hatari.
 
Naona sasa mmeanza kuweweseka kama kawaida yenu. Hata kabla ya kuwa mkuu wa wilaya na baadaye mkuu wa mkoa kila mmoja hakufahamu majukumu ya nafasi hizo, pamoja na mamlaka yake katika kuchochea maendeleo.ni mpaka alipoteuliwa mwamba mwenyewe Mheshimiwa Makonda kijana jasiri kusini mwa jangwa la sahara.

Mheshimiwa Makonda ni kijana jasiri na anayetambua majukumu yake.afanyayo ni majukumu yake kabisa. Chama ndicho kilichounda serikali na siyo serikali iliyounda chama. Ni chama kinachokwenda kwa wananchi kuomba kura na siyo serikali inayokwenda. Ni CCM Ndio itakayoulizwa maswali majukwaani na wananchi na siyo serikali.serikali ikiharibu kinachochukiwa ni chama kilichounda serikali na ndicho kitakacho adhibiwa kwenye sanduku la kura wakati wa uchaguzi.

Sasa kwa akili yako unataka chama kikawa kimya? Unataka chama kinyamaze bila kuwasemea watanzania? Unataka chama kisiende kwa wananchi kuwasikiliza kero zao na kuwapa majibu? Unataka wananchi wasipelekee kero zao kwa chama walichokichagua wao wenyewe?

Kwa akili yako hiyo hiyo unafirikiri chama kikianguka hao wakuu wa mikoa watabaki? Hao mawaziri watakuwepo ? Hao madc na na Ded watabakia? Sasa kwanini wasikiheshimu chama kilichowapa nafasi hizo kwa ajili ya kusimamia utekelezaji wa ilani ya CCM? Kwanini wasikumbushwe wajibu wao na majukumu yao katika kuwatumikia wananchi?
Ccm bwana ww si ulikuwa unamponda sanq
 
Unafrahisha sana kujiita mlokole!
Na kutabili uongo kiasi hicho
Inawezekana nafasi IPO ila watu hawakujua /kupenda kuitumia ipasavyo!!
Baba huyo ndo msemaji wa CCM!!!
MAKONDA Baba lao endelea kusafisha mapito !!
 
Rais awapige chini watendaji wote wabovu. Haingii akilini mtu anaharibu wizara ya nishati badala kufukuzwa anapewa wizara ya nje. Mara aseme mitambo chakavu, ukarabati, mvua, watu kuchepusha maji greda.

Lukuvi, kalemani walizimudu wizara zao. Uhuni ulipungua huko. Unawatoa kisa woga, fitina, majungu.

Inatakiwa watendaji wote wapige kazi zao na kuwajibishwa. Rais awe mfano.
 
Niite jina lolote, lakini mimi ni mojawapo ya watu ambao huwezi hata kabisa kunishawishi kwamba hii nguvu na mbwembwe ambazo Makonda amekuwa akizionyesha zinatokana na kuwa kwake na cheo cha katibu mwenezi wa CCM. Tusidanganyane hapa.

Makonda sio katibu mwenezi wa kwanza CCM, na wamekuwapo wengine huko nyuma, lakini ni mara ya kwanza tunapata katibu mwenezi wa CCM ambae anaonyesha kujiamini kupita mamlaka yanayostahili ya katibu mwenezi wa CCM.

Leo hii katibu mwenezi awapigie simu mawaziri, amkebehi mwanasheria mkuu wa serikali, awaamrishe wakuu wa mikoa, ma-RPC, eti kwa sababu yeye ndie msemaji mkuu wa chama, hilo tu? Haiwezekani.

Leo hii katibu mwenyezi apewe bajeti, misafara ya magari, kuliko inavyokuwa kwa makamu mwenyekiti wa CCM au katibu mkuu wa CCM, kwa sababu gani? Kwamba katiba ya CCM imebadilishwa kisiri na hawa wote wameambiwa kuanzia sasa bosi wenu ni katibu mwenezi wa CCM? Pamoja na mawaziri? Wakuu wa mikoa? Mwanasheria Mkuu? Wenyeviti wa CCM wa mikoa?

Sote tunajua msemaji mkuu wa chama chochote anasema yale chama kilichoamua katika vikao vyake rasmi. Kuwa msemaji wa chama haina maana wewe ndio unakuwa unakisemea chama, hata siku moja. Kuwa katibu mwenyezi sio katika mpangilio wa vyeo vya chama, ni nafasi tu. Huwezi hata kusema katibu mwenezi wa CCM ni mkubwa kuliko mwenyekiti wa CCM wa mkoa. Lakini sio hivyo kwa Makonda. Yeye amejipa madaraka ambayo nadhani yanazidi hata ya kuwa makamu mwenyekiti wa CCM, au katibu mkuu wa CCM. Kujiamini huko kunatoka wapi? Mamlaka haya yanatoka wapi? Kwamba siku zote hatukujua kuwa katibu mwenezi wa chama ni mtu mkubwa namna hii? Ni kweli?

Nyie watu wa CCM, nyie mawaziri, nyie wakuu wa mikoa, tuambieni ukweli. Kinachowafanya muufyate Makonda akiunguruma ni nini hasa, Ukatibu mwenezi wa CCM? Na kwa nini sasa wenye akili tukiwauliza mbona mambo yako hivi, mnaishia kutabasamu tu bila kusema lolote? Kuna kitu gani msichotuambia?

Na niwaambie wazi nyie watu wa CCM. Kama nguvu ya Makonda sio ya kikatiba ndani ya CCM, kama kuna chanzo kingine kisicho rasmi kinampa nguvu na kujiamini kiasi hiki, basi anguko la CCM liko karibu sana
Tatizo linaanzia hapo juu kabisa. Uwezo mdogo wa kiuongozi. Unafikiri wateule wakisikia kauli zake wanajali. Wakiiba wanajua watahamishwa au kupewa kazi nyingine, hakuna uwajibikaji.

Watu wanamsikiliza zaidi Majaliwa na Makonda kuliko Rais. Mifano, teuzi na vitendo vyake vinaonyesha hajali maisha na shida za watu wa chini.

Unawaita wengi wajinga, elimu, afya, ajira, umeme, maji, mazingira wezeshi wanyanyuke watoe ujinga.

Weka mifumo, viongozi, taasisi imara zitakazolinda usalama na mali zao.
 
Ninyi ndio wajinga lakini watanzania siyo wajinga . Watanzania wanatambua kazi njema na yakutuka inayofanywa na Mheshimiwa Makonda katika kuwatetea na kuwasemea watanzania.watanzania wanaona namna ziara za Mheshimiwa Makonda zilivyochochea uwajibikaji kwa viongozi mbalimbali waliokuwa wanafanya kazi kwa mazoea na kukaa maofisini tu bila kutoka kwenda kuwasikiliza wananchi.

Hata hivyo napenda kukwambia kuwa kaa ukijiandaa maana huyo ipo siku moja utamtizama kupitia Tv akiapishwa kuwa Rais wa Tanzania.
"If wishes were horses, beggars would ride".
 
Hayo Mambo mengine ni Ujinga wa Watanzania wenyewe....!

Lakini haiondoi ukweli kuwa Mikutano ya Makonda kuna watu inawasaidia, na hiyo ndo Muhimu......!

Mkuu mimi sio Mpiga Debe wa CCM kama wengi wao hapa, Binafsi siwapendi CCM mpaka naingia Kaburini, ila kama CCM ikiendelea kuongoza, hakuna siku hata moja, System ya Uongozi chni ya CCM itakuja kutatua matatizo ya Watu wa hari ya chini kwa kusubiri Viongozi wa Umma, kila siku zinavyokwenda ndo matatizo yanazidi....!

Ni bora akitokea Mtu kama Makonda akafanya anachokifanya angalau kuna watu wanasaidika, japo anapigwa Vita mpaka na Viongozi wa CCM...!
Ametatua tatizo gani la msingi kwenye kuzunguka kwake kimaigizo!!??
 
Nimekuelewa Sana, na kwa upeo wangu na pia kwa historia iliyokuwepo kwa muheshimiwa pamoj na hizi chaguzi zijazo ni wazi kabisa zote hizi huenda zikawa siasa.
 
Mpaka sasa amefanya nini Makonda? Ila watu mna muda wa kupoteza, alikopita kote ni wapi umesikia kuna tume iko kazini kwa madudu aliyoyaibua Makonda? ni wapi umesikia watumishi wamewekwa ndani kwa upotevu wa mabilion, maigizo ni maigizo tu hayajawahi kuwa kitu halisi.
 
Niite jina lolote, lakini mimi ni mojawapo ya watu ambao huwezi hata kabisa kunishawishi kwamba hii nguvu na mbwembwe ambazo Makonda amekuwa akizionyesha zinatokana na kuwa kwake na cheo cha katibu mwenezi wa CCM. Tusidanganyane hapa.

Makonda sio katibu mwenezi wa kwanza CCM, na wamekuwapo wengine huko nyuma, lakini ni mara ya kwanza tunapata katibu mwenezi wa CCM ambae anaonyesha kujiamini kupita mamlaka yanayostahili ya katibu mwenezi wa CCM.

Leo hii katibu mwenezi awapigie simu mawaziri, amkebehi mwanasheria mkuu wa serikali, awaamrishe wakuu wa mikoa, ma-RPC, eti kwa sababu yeye ndie msemaji mkuu wa chama, hilo tu? Haiwezekani.

Leo hii katibu mwenyezi apewe bajeti, misafara ya magari, kuliko inavyokuwa kwa makamu mwenyekiti wa CCM au katibu mkuu wa CCM, kwa sababu gani? Kwamba katiba ya CCM imebadilishwa kisiri na hawa wote wameambiwa kuanzia sasa bosi wenu ni katibu mwenezi wa CCM? Pamoja na mawaziri? Wakuu wa mikoa? Mwanasheria Mkuu? Wenyeviti wa CCM wa mikoa?

Sote tunajua msemaji mkuu wa chama chochote anasema yale chama kilichoamua katika vikao vyake rasmi. Kuwa msemaji wa chama haina maana wewe ndio unakuwa unakisemea chama, hata siku moja. Kuwa katibu mwenyezi sio katika mpangilio wa vyeo vya chama, ni nafasi tu. Huwezi hata kusema katibu mwenezi wa CCM ni mkubwa kuliko mwenyekiti wa CCM wa mkoa. Lakini sio hivyo kwa Makonda. Yeye amejipa madaraka ambayo nadhani yanazidi hata ya kuwa makamu mwenyekiti wa CCM, au katibu mkuu wa CCM. Kujiamini huko kunatoka wapi? Mamlaka haya yanatoka wapi? Kwamba siku zote hatukujua kuwa katibu mwenezi wa chama ni mtu mkubwa namna hii? Ni kweli?

Nyie watu wa CCM, nyie mawaziri, nyie wakuu wa mikoa, tuambieni ukweli. Kinachowafanya muufyate Makonda akiunguruma ni nini hasa, Ukatibu mwenezi wa CCM? Na kwa nini sasa wenye akili tukiwauliza mbona mambo yako hivi, mnaishia kutabasamu tu bila kusema lolote? Kuna kitu gani msichotuambia?

Na niwaambie wazi nyie watu wa CCM. Kama nguvu ya Makonda sio ya kikatiba ndani ya CCM, kama kuna chanzo kingine kisicho rasmi kinampa nguvu na kujiamini kiasi hiki, basi anguko la CCM liko karibu sana!
Kikubwa Watanzania wamepata sehemu ya kuongelea shida zao na zinatatuliwa hayo mengine hayajalishi.
 
Mpaka sasa amefanya nini Makonda? Ila watu mna muda wa kupoteza, alikopita kote ni wapi umesikia kuna tume iko kazini kwa madudu aliyoyaibua Makonda? ni wapi umesikia watumishi wamewekwa ndani kwa upotevu wa mabilion, maigizo ni maigizo tu hayajawahi kuwa kitu halisi.

Wewe ungekuwa Mkurugenzi mwizi, afisa ardhi mwizi mkubwa umedhulumu wengi ukisikia anakuja mwezi ujao ana ziara eneo lako ungeendelea na wizi ungekuwa kwenye hali gani? Utafanya kazi yako vipi?

Ukijua hadi Rais, mawaziri, wakubwa zako, Tanzania nzima itaona wizi wako? Utaitwa jukwaani kujieleza?
 
Back
Top Bottom