N/korea Watest Kombora lililosafiri kilometer 700

Marekani ana makombora yanayofika popote duniani korea anatest km 700, marekani wana ndege za kivita za kisasa zenye gharama na zisizomilikiwa na nchi yeyote duniani, marekani huwez kumpiga kwa nuclear wala kwa mtutu tena bora korea kusini na china wanaweza kujaribu kumpiga marekani lakini sio N.korea
Unawezaje kujikomba kwa taifa katili kama Marekani? Umesahau kwamba hawa pekee duniani ndio wamefanya shambulio la bomu la nuclear kwa hao hao Japan wanaojikomba kwao Marekani kwa sasa? Niambie ni nchi gani North Korea wapeleka wanajeshi wao kupiganisha vita na kuuwa wananchi wasio na hatia kama Marekani inavyofanya kwa nchi nyingi za kiarabu na hata ulaya na Amerika kusini kwa kisingizio cha kurudisha demokrasia na kulinda wananchi wa nchi hizo na badala yake kuwauwa , mfano Iraq , Libya vietnam, Yugoslavia na nchi kadha wa kadha?

Ndugu umepotoka, North Korea sio Iraq, bw.mdogo Kim yuko vizuri kivita , kama kweli Trump anaweza kushambulia N.Korea mbona amebaki na vitisho tu na dogo anaendelea na majaribio yake kama kawaida licha ya vitisho hivyoPpp. Kwa sasa North Korea wanazo ICBM zilizofungwa Nuclear war heads ambazo zimeelekezwa kwenye majiji mengi ya America , stand put for swiftly actiion in the event the Americans spark it .
 
NK ni muziki mnene na wa aina yake. Hata huyu chizi wa US hawezi kuingia NK kichwa kichwa tu.
Anaogopa kuiletea aibu nchi yake.
 
Wengine waliwahi kusema, US amepandikiza Virus kwenye mifumo ya makombora ya NK.
Leo sijui kama watasemaje.

Well said, tatizo hapa utakuta watu ambao hawajui masuala ya control system zinavyo fanya kazi ndiyo wanakuja na upuuzi huu jamvini - eti Wamerika walipandikiza virusi - ajabu sana, wavipandikize kupitia njia hipi? Mtandaoni, flashstick, simu za mkononi, tablet au njia zipi ambazo wataalamu wa ICT wa Korea Kasikazini hawazijui hivyo kuchukua tahadhali mapema inapobidi, Wakorea Kasikazini si mambumbu kama baadhi ya watu wanavyo wafikiria.

Madai ya watu baki kwamba USA ilipandikiza virus kwenye mfumo wa Roketi za KK madai hayo hayana ukwei wowote ndiyo maana USA imekaa kimya kwa kuwa wanaelewa madai hayo ni ndoto za mchana, ma-layman ndiyo wanaeneza uzushi huo: Kitu cha kwanza si rahisi majasusi wa USA kupata access ya kuingia kwenye Assembly line ya Roketi za KK waka-upload virus kwenye control modules zinazo ongoza fuel pumps na combustors za injini za roketi - tatizo hapa mtu kama uelewi vizuri mambo haya unaweza kudanganyika kirahisi sana lakini kwa wale ambao wamewahi kujifunza mambo haya wanajua kwamba uwezi kuandika/code virus kama ujui type ya microprocessor vile vile na computer language iliyo tumika ku-code system/apps software zinazo tumika kwenye roketi - kama huna taarifa hizo nyeti basi uwezekano wa wewe kukorofisha injini za roketi kwa kupitia njia ya kupandikiza virus ambavyo language yake sio native na system/apps software za logic controller kwenye roketi, basi uwezekano wa majasusi kukorofisha injini haupo kabisa.

Msifikiri mambo yaliyo wahi kuwapata Wairan kwenye vinu vyao vya kufua Plutonium yanaweza kujirudia Korea ya kasikazini, Wairan walipata hasara kutokana kwanza:kutokuwa makini, pili PLC walizo kuwa wanazitumia kwenye vinu vyao zinajulikana sana kwenye Industry za wahundaji wa Programmable Logic Controllers, Controller za Iran zilikuwa zinatoka Ujerumani (Siemens) watu wengi Duniani wanajua PLC za Siemens zitatumia Step5/7 language kuzi program hivyo majasusi wa USA na Israel walijua jinsi ya kuandika virus za kufanya PLC zizungushe aluminium Centrifuge Canisters kwa spidi/kasi kubwa sana mpaka to distraction - hicho ndicho kiliwapata Wairan, walilazimika kuomba msaada kutoka kwa Warusi (Karspesky Lab) kuondoa virusi kwenye PLCs zao.
 
Marekani hawaendi kichwakichwa kama huna mafuta wala chochote wanachoweza kuchukua hawaji ng'ooo, hata Tanzania leo ikitangaza vita na marekani hawaji kama hakuna cha kuchukua.
Somalia na Vietnam walifata nini?.. walikipata walichokifata?.. kama hawakupata mbona waliondoka?.. Na kama kipo bado kwanini hawajarudi kifata walichoacha?.. NIENDELEE ULIZA?
 
Mkuu umesahau Cuba, Vietnam, Yugoslavia ya zamani na Grenada nk!! Binafsi huwa napata wakati mgumu kuwaelewa Waswahili wanao sifia Taifa la kijahili linalo jihusisha katika mauuji ya raia kwa kutumia mabom ya nuclear kwa mara ya kwanza, mabom ya sumu, depleted uranium bombs. cluster bomblets, kulazimisha Mataifa yakubaliane na upuuzi wao wa kubariki ndoa za jinsia moja husipo kubali nao unanyimwa misaada! Wanawalisha watu GMOs bila kuwambia walaji, wanashirikiana na corrupt Govts za Dunia ya tatu kueneza mbegu zao ambazo ni modified genetically ili mwisho wa siku ziharibu mbegu asili mwendelee kuwa tegemezi wa mbegu za Mossanto, wanarubuni wakulima watumie weed killer aina ya Roundup huku wakijua wazi inasababisha kansa - yaani ukufatilia historia ya ushenzi wao wa miaka nenda rudi unaweza kuandika Encyclopedia.

Raia wa Marekani hawana tatizo, tatizo ni Viongozi wao ambao hawajali maisha ya binadamu wenzao hapa Duniani linapo kuja suala kutimiza malengo yao katika nyanja za Geopolitics, wapo radhi ku-assasinated mpaka kiongozi yeyote Duniani atakaye watilia kiwingu katika azma zao, hawana utu hata kidogo.
 
North korea wana kelele nyingi maonyesho mengi lakini vita hawawezi
Hivi wakati wa Korean war 1950-1953 ulikuwa na umri gani? Kama ulikuwepo ukiwa unajua kinachoendelea usingesema hayo unayosema!
Hivi haujiulizi mkwata wa marekani kusombelea mimeli ya vita kwenye rasi ya Korea uliishia wapi?
Sasa hivi Trump haongei tena lugha ya vitisho vya vita Bali vikwazo vya kiuchumi ambavyo jamaa alishavizoea!
 
Marekani ana makombora yanayofika popote duniani korea anatest km 700, marekani wana ndege za kivita za kisasa zenye gharama na zisizomilikiwa na nchi yeyote duniani, marekani huwez kumpiga kwa nuclear wala kwa mtutu tena bora korea kusini na china wanaweza kujaribu kumpiga marekani lakini sio N.korea
Korea ya kaskazini haina nia hata siku moja ya kuipiga marekani! Lakini wanachosema ni kuwa kama marekani akichokoza wama uwezo wa kujibu mashambulizi kwa silaha za nyuklia! Marekani analijua hilo ndo maana keshafyata mkia! Makeke ya kusafiri maelfu ya maili na mimeli ya vita yameishia wapi? Nyuklia si mchezo! Hakuna mbabe mbele ya nyuklia! Ndo maana China walimwaambia Trump kuwa vita ikitokea hapatakuwa na mshindi! Kutokuwepo mshindi ni sawa na marekani kushindwa!
Halafu wahanga wakubwa watakuwa ni vibaraka wa marekani Japan na korea ya kusini ambao wako umbali wa pua na mdomo kutoka NK!
 
Marekani hawaendi kichwakichwa kama huna mafuta wala chochote wanachoweza kuchukua hawaji ng'ooo, hata Tanzania leo ikitangaza vita na marekani hawaji kama hakuna cha kuchukua.
Marekani wataenda popote lakini penye nguvu ya nyuklia hawagusi ng'o!
Missile yenye kubeba nyuklia aliyorusha NK Leo linakwenda 4500km! Wakiongeza fuel kidogo tayari litaweza kufika zaidi ya km 7000, hivyo kutungua miji mingi tu ya marekani!
 
Kombora limeenda juu 2000km na kutua 700km katika bahari ya Japan,USA wao wamefanya tafiti na kuundua sio intercontinental ballistic missile...
Hilo ni intercontinental! Likiwekewa fuel (nishati) ya kutosha lina uwezo wa kusafiri zaidi ya kilomita 7000! Kama umegundua Trump keshaanza kuwa mpole!
 
Hakuna Taifa lenye unyama kama marekani! Ona walichokifanya Iraq na Libya!
Walimdanganya Gaddafi aachane na mipango yake ya nyuklia halafu wakamwangamiza!
Kim hataki huo upuuzi!
Kama silaha za nyuklia ni mbaya mbona yeye anazo?
 
Well said, tatizo hapa utakuta watu ambao hawajui masuala ya control system zinavyo fanya kazi ndiyo wanakuja na upuuzi huu jamvini - eti Wamerika walipandikiza virusi - ajabu sana, wavipandikize kupitia njia hipi? Mtandaoni, flashstick, simu za mkononi, tablet au njia zipi ambazo wataalamu wa ICT wa Korea Kasikazini hawazijui hivyo kuchukua tahadhali mapema inapobidi, Wakorea Kasikazini si mambumbu kama baadhi ya watu wanavyo wafikiria.

Madai ya watu baki kwamba USA ilipandikiza virus kwenye mfumo wa Roketi za KK madai hayo hayana ukwei wowote ndiyo maana USA imekaa kimya kwa kuwa wanaelewa madai hayo ni ndoto za mchana, ma-layman ndiyo wanaeneza uzushi huo: Kitu cha kwanza si rahisi majasusi wa USA kupata access ya kuingia kwenye Assembly line ya Roketi za KK waka-upload virus kwenye control modules zinazo ongoza fuel pumps na combustors za injini za roketi - tatizo hapa mtu kama uelewi vizuri mambo haya unaweza kudanganyika kirahisi sana lakini kwa wale ambao wamewahi kujifunza mambo haya wanajua kwamba uwezi kuandika/code virus kama ujui type ya microprocessor vile vile na computer language iliyo tumika ku-code system/apps software zinazo tumika kwenye roketi - kama huna taarifa hizo nyeti basi uwezekano wa wewe kukorofisha injini za roketi kwa kupitia njia ya kupandikiza virus ambavyo language yake sio native na system/apps software za logic controller kwenye roketi, basi uwezekano wa majasusi kukorofisha injini haupo kabisa.

Msifikiri mambo yaliyo wahi kuwapata Wairan kwenye vinu vyao vya kufua Plutonium yanaweza kujirudia Korea ya kasikazini, Wairan walipata hasara kutokana kwanza:kutokuwa makini, pili PLC walizo kuwa wanazitumia kwenye vinu vyao zinajulikana sana kwenye Industry za wahundaji wa Programmable Logic Controllers, Controller za Iran zilikuwa zinatoka Ujerumani (Siemens) watu wengi Duniani wanajua PLC za Siemens zitatumia Step5/7 language kuzi program hivyo majasusi wa USA na Israel walijua jinsi ya kuandika virus za kufanya PLC zizungushe aluminium Centrifuge Canisters kwa spidi/kasi kubwa sana mpaka to distraction - hicho ndicho kiliwapata Wairan, walilazimika kuomba msaada kutoka kwa Warusi (Karspesky Lab) kuondoa virusi kwenye PLCs zao.

Kitu nilicho gundua au jifunza kuwa pro NK wote wanauwezo mkubwa wakufikiri outside the box, above normal thinking line, kwakuchambua mambo in realist way ila PRO US ni watu wapenda cinema na wanaamin wanayo yaona kwenye cinema za kimarekan basi wao ndio hatar zaid.

Kifupi pro us wanapenda mapicha tuuu
 
Hilo la USA lipo wazi ana nguvu na uwezo wa kila aina

Mgogoro wote ni sababu ya south Korea.NK shida yao na tatizo lao ni south ila USA anajiita mtetezi ndio kaingilia

Hebu nikupe mfano Iran juzi walisema wakiguswa basi makombora yao yatarushwa Tel Aviv na Bahrain

Seoul na Pyongyang ni karibu mno na Seoul ndio chanzo kwahiyo akirusha karibia makombora yake yote seoul nmna machache ya ICBM huko California japo hayatokuwa effective.. South atapoteza mengi kuanzia uchumi wao nk

Hiyo mindege ,makombora ya USA hazina maana kama Seoul ikiangamia..kuhusu Thaad kila kitu kina loophole ndio maana USA anataka diplomasia saizi sababu lazima south watapata majanga tu
Unesahau Japan
 
Hivi wakati wa Korean war 1950-1953 ulikuwa na umri gani? Kama ulikuwepo ukiwa unajua kinachoendelea usingesema hayo unayosema!
Hivi haujiulizi mkwata wa marekani kusombelea mimeli ya vita kwenye rasi ya Korea uliishia wapi?
Sasa hivi Trump haongei tena lugha ya vitisho vya vita Bali vikwazo vya kiuchumi ambavyo jamaa alishavizoea!

Well said mkuu, kitu nilicho gunduwa humu jamvini baadhi ya wachangiaji hawajui historia hasa masuala ya Geopolitics, wengi wao ni wabishi balaa - ukisikiliza/soma majibu yao unajua wazi wazi kwamba mambo mengi wanayo yaleta jamvini yanatokana na aidha kwa kuwa influenced by watching make believe movies zinazo zalishwa katika moja ya Studio sita za Hollywood au kucheza video games kwenye play stations basi!!!! Wana amini sana wanayo yaona kwenye movies vile vile na news kutoka MSM wanaziabudu bila ya kujihoji kwanza.
 
Hakuna Taifa lenye unyama kama marekani! Ona walichokifanya Iraq na Libya!
Walimdanganya Gaddafi aachane na mipango yake ya nyuklia halafu wakamwangamiza!
Kim hataki huo upuuzi!
Kama silaha za nyuklia ni mbaya mbona yeye anazo?
Mkuu marekani Yuko tayari kufanya chochote kwa ajili ya Security ya taifa lake.
Ndio maana anapambana Silaha za nyuklia ziwe angalau mikononi mwa mataifa ambayo tayari ukute hata viongozi wengi ni mapandikizi wake au mtu ambae hawezi kumchokoza. N.K haeleweki na akiachwa uwezo ukue atasumbua
 
Mkuu umesahau Cuba, Vietnam, Yugoslavia ya zamani na Grenada nk!! Binafsi huwa napata wakati mgumu kuwaelewa Waswahili wanao sifia Taifa la kijahili linalo jihusisha katika mauuji ya raia kwa kutumia mabom ya nuclear kwa mara ya kwanza, mabom ya sumu, depleted uranium bombs. cluster bomblets, kulazimisha Mataifa yakubaliane na upuuzi wao wa kubariki ndoa za jinsia moja husipo kubali nao unanyimwa misaada! Wanawalisha watu GMOs bila kuwambia walaji, wanashirikiana na corrupt Govts za Dunia ya tatu kueneza mbegu zao ambazo ni modified genetically ili mwisho wa siku ziharibu mbegu asili mwendelee kuwa tegemezi wa mbegu za Mossanto, wanarubuni wakulima watumie weed killer aina ya Roundup huku wakijua wazi inasababisha kansa - yaani ukufatilia historia ya ushenzi wao wa miaka nenda rudi unaweza kuandika Encyclopedia.

Raia wa Marekani hawana tatizo, tatizo ni Viongozi wao ambao hawajali maisha ya binadamu wenzao hapa Duniani linapo kuja suala kutimiza malengo yao katika nyanja za Geopolitics, wapo radhi ku-assasinated mpaka kiongozi yeyote Duniani atakaye watilia kiwingu katika azma zao, hawana utu hata kidogo.
mkuu ninachofahamu kuhusu hwa jamaa, wao wako tayari kufanya chochote kwa faida ya raia wao. Pia inaonekana michongo mingine huwa wanafanya wenda kwa faida ya viongozi wenyewe na sio hata wananchi. Au kwa faida ya watu ambao wako upande wao. Tutegemee mengi, na wakipata justfication ya kuingia kwa nguvu huku wakihakikisha Raia wao watakuwa salama na nucklia hawashindwi kuvamia N/K. Ndio maana S/Korea wengi wanamuona trump kama adui yao, maana muda wowote anaweza kufanya maamuzi ambayo yanaweza kugharimu maisha ya mamillioni ya raia wao.
 
Mkuu marekani Yuko tayari kufanya chochote kwa ajili ya Security ya taifa lake.
Ndio maana anapambana Silaha za Nyuclia ziwe angalau mikononi mwa mataifa ambayo tayari ukute hata viongozi wengi ni mapandikizi wake au mtu ambae hawezi kumchokoza. N.K haeleweki na akiachwa uwezo ukue atasumbua

Kabla sijakuhoji labda turudi nyuma kidogo tuangalie historia ya USA - Amerika iliacha kuwa koloni la Uingereza in late 1770s sasa ni takribani miaka 400 (mia nne) tangu wajitawale - unaweza kutupatia ushahindi wowote wa kuonyesha Taifa lolote lililo wahi kuvamia Amerika, kuondoa utawala wao madarakani au kulazimisha utawala wao ufuate siasa za mlengo fulani? Historia inaonyesha Amerika imewahi kupigana vita vya kuvamivi Mataifa mengine zaidi ya mara mia tatu , sasa hizi adhithi za kusema eti alitaki Mataifa mengine yamiliki silaha kali eti kwa ajili ya usalama wa Taifa lao - Taifa gani liliwahi kutamka kwamba lina mpango wa kuivamia na kukialia Taifa la Marekani - hakuna.

Matatizo ya kiusalama yanayo kabiri Taifa lao yanatokana na wao kijitia kimbelembele kuvamia Matifa ya watu wengine, kuwauua viongozi wa Mataifa mengine bila sababu, kupiga mabom mashule, hospitali, misikiti na makazi ya raia wasio na hatia, kuwafanya raia kuwa wakimbizi - hivi Amerika inategemea ndugu na jamaa walio uwawa na uvamizi/majeshi ya Marekani watafanya nini kama siyo kulipiza kisasi kwa njia ya kutumia ugaidi - ugaidi umeshamiri Duniani kutokana na matendo ya kishenzi/kikatiri ya Taifa hilo ambalo alina hofu ya Mungu.

Jaribu kufatilia nini kilijiri baada ya Amerika kufanikiwa kuhunda Bomb ya Nuclear kwa msaada wa wanasayansi kutoka Ulaya, je kulikuwa na sababu zozote za msingi za kulitumia bom hilo kuua Wajapan wakati vita ilisha fikia tamati - unaweza kuamini kwamba Wamerika walitaka kutumia bom hilo kutishia Mataifa mengine specifically Urusi ambayo walikuwa wana ogopa nguvu zake za kijeshi baada ya kutoa mchango mkubwa wa kushinda jeshi la Hitler ambalo lilikuwa imara na hatari, Wajapan wakapigwa bom la Nuclear na Marekani kwa lengo la kuitisha Urusi!!! Nilisha wahi kusema humu kwamba Churchil alimshauri Truman watumie mabom ya nuclear kupiga miji muhimu ya Urusi ili waisambaratishe kabisa Taifa hilo na kulikalia wakati likiwa bado linaombeleza raia wake millioni ishirini walio poteza maisha kukomboa Taifa lao na Mataifa mengine mengi ya Ulaya Mashariki na kati,Waingereza walipoteza watu laki nne tu na Amerika laki saba - ndiyo maana walikuwa na jeuri ya kutaka kuivamia Urusi.

Kilicho wafanya Waingereza na Wamerika wasitishe mpango wao wa kuivamia Urusi kilitokana na Amerika kutokuwa na mabom ya Nuclear ya kutosha kushambulia Urusi ambayo eneo lake la mraba ni robo ya Dunia, actually walibakiwa na bom moja tu baada ya kudondosha mabom mawili Japan na moja lilifanyiwa majaribio huko Los Almos Nevada Desert ,mabom walio kuwa wamehunda yalikuwa manne tu ndiyo maana walilazimika kuhairisha mpango wa kuishambulia Urusi mpaka watakapo hunda mabom ya kutosha, kwa bahati nzuri wanasayansi walio saidia Amerika kuhunda bom wakaona Amerika ikiendelea kuwa Taifa pekee linalo miliki Mabom ya nuclear basi Dunia haitakuwa salama, hivyo wakahamua kuwapatia majasusi wa Urusi siri za kuhunda Bom la Nuclear, baada ya miaka 3/4 Urusi nayo ikafanikiwa kulipuwa bomb la Nuclear - Serikali ya Amerika ilishikwa kiwewe akianza kumtafuta mchawi, jamaa mmoja na mkewe wakatiwa mbaroni na kuhukumiwa kifo kwa ujasusi wa kuwapatia siri Warusi, cha kushangaza mwanasayansi aliye kuwa kiungo muhimu wa ujasusi alifungwa tu na baade kubadirishwa na jasusi wa Kimerikani aliye kuwa anashikiliwa na Warusi.

Sasa hii inatufundisha nini kuhusu hulka za USA - ni kwamba walitaka wao ndiyo wawe wamiliki pekee wa mabom ya Nuclear, walitaka kuyatumia kutishia na blackmail mataifa mengine, Taifa lao ndilo pekee ambalo liliwahi kutumia mambom hayo hatari kwa binadamu wenzao consequently hawana moral Authority ya kukemea Mataifa mengine wasiwe nayo, kama wao wanafikiri mambom hayo yana wahakikishia Usalama wao kwanini hawataki Mataifa mengine kuyamiliki - they have a choice aidha waache Mataifa yenye uwezo wa kuyahunda na kuyamiliki wabaki nayo au wamiliki wa mabom hayo wakubaliane wote kuyahabiru including ya Wamerika wenyewe 4 the benefit/amani ya wakazi wote Dunani - atuwezi kuendelea kui-entertain double standard.
 
mkuu ninachofahamu kuhusu hwa jamaa, wao wako tayari kufanya chochote kwa faida ya raia wao. Pia inaonekana michongo mingine huwa wanafanya wenda kwa faida ya viongozi wenyewe na sio hata wananchi. Au kwa faida ya watu ambao wako upande wao. Tutegemee mengi, na wakipata justfication ya kuingia kwa nguvu huku wakihakikisha Raia wao watakuwa salama na nucklia hawashindwi kuvamia N/K. Ndio maana S/Korea wengi wanamuona trump kama adui yao, maana muda wowote anaweza kufanya maamuzi ambayo yanaweza kugharimu maisha ya mamillioni ya raia wao.

I commend you for this clever comment.
 
Kabla sijakuhoji labda turudi nyuma kidogo tuangalie historia ya USA - Amerika iliacha kuwa koloni la Uingereza in late 1770s sasa ni takribani miaka 400 (mia nne) tangu wajitawale - unaweza kutupatia ushahindi wowote wa kuonyesha Taifa lolote lililo wahi kuvamia Amerika, kuondoa utawala wao madarakani au kulazimisha utawala wao ufuate siasa za mlengo fulani? Historia inaonyesha Amerika imewahi kupigana vita vya kuvamivi Mataifa mengine zaidi ya mara mia tatu , sasa hizi athi za kusema eti alitaki Mataifa mengine yamiliki silaha kali eti kwa ajili ya usalama wa Taifa lao - Taifa gani liliwahi kutamka kwamba lina mpango wa kuivamia na kukialia Taifa la Marekani - hakuna.

Matatizo ya kiusalama yanayo kabiri Taifa lao yanatokana na wao kijitia kimbelembele kuvamia Matifa ya watu wengine, kuwauua viongozi wa Mataifa mengine bila sababu, kupiga mabom mashule, hospitali, misikiti na makazi ya raia wasio na hatia, kuwafanya raia kuwa wakimbizi - hivi Amerika inategemea ndugu na jamaa walio uwawa na uvamizi/majeshi ya Marekani watafanya nini kama siyo kulipiza kisasi kwa njia ya kutumia ugaidi - ugaidi umeshamiri Duniani kutokana na matendo ya kishenzi/kikatiri ya Taifa hilo ambalo alina hofu ya Mungu.

Jaribu kufatilia nini kilijiri baada ya Amerika kufanikiwa kuhunda Bomb ya Nuclear kwa msaada wa wanasayansi kutoka Ulaya, je kulikuwa na sababu zozote za msingi za kulitumia bom hilo kuua Wajapan wakati vita ilisha fikia tamati - unaweza kuamini kwamba Wamerika walitaka kutumia bom hilo kutishia Mataifa mengine specifically Urusi ambayo walikuwa wana ogopa nguvu zake za kijeshi baada ya kutoa mchango mkubwa wa kushinda jeshi la Hitler ambalo lilikuwa imara na hatari, Wajapan wakapigwa bom la Nuclear na Marekani kwa lengo la kuitisha Urusi!!! Nilisha wahi kusema humu kwamba Churchil alimshauri Truman watumie mabom ya nuclear kupiga miji muhimu ya Urusi ili waisambaratishe kabisa Taifa hilo na kulikalia wakati likiwa bado linaombeleza raia wake millioni ishirini walio poteza maisha kukomboa Taifa lao na Mataifa mengine mengi ya Ulaya Mashariki na kati,Waingereza walipoteza watu laki nne tu na Amerika laki saba - ndiyo maana walikuwa na jeuri ya kutaka kuivamia Urusi.

Kilicho wafanya Waingereza na Wamerika wasitishe mpango wao wa kuivamia Urusi kilitokana na Amerika kutokuwa na mabom ya Nuclear ya kutosha kushambulia Urusi ambayo eneo lake la mraba ni robo ya Dunia, actually walibakiwa na bom moja tu baada ya kudondosha mabom mawili Japan na moja lilifanyiwa majaribio huko Los Almos Nevada Desert ,mabom walio kuwa wamehunda yalikuwa manne tu ndiyo maana walilazimika kuhairisha mpango wa kuishambulia Urusi mpaka watakapo hunda mabom ya kutosha, kwa bahati nzuri wanasayansi walio saidia Amerika kuhunda bom wakaona Amerika ikiendelea kuwa Taifa pekee linalo miliki Mabom ya nuclear basi Dunia haitakuwa salama, hivyo wakahamua kuwapatia majasusi wa Urusi siri za kuhunda Bom la Nuclear, baada ya miaka 3/4 Urusi nayo ikafanikiwa kulipuwa bomb la Nuclear - Serikali ya Amerika ilishikwa kiwewe akianza kumtafuta mchawi, jamaa mmoja na mkewe wakatiwa mbaroni na kuhukumiwa kifo kwa ujasusi wa kuwapatia siri Warusi, cha kushangaza mwanasayansi aliye kuwa kiungo muhimu wa ujasusi alifungwa tu na baade kubadirishwa na jasusi wa Kimerikani aliye kuwa anashikiliwa na Warusi.

Sasa hii inatufundisha nini kuhusu hulka za USA - ni kwamba walitaka wao ndiyo wawe wamiliki pekee wa mabom ya Nuclear, walitaka kuyatumia kutishia na blackmail mataifa mengine, Taifa lao ndilo pekee ambalo liliwahi kutumia mambom hayo hatari kwa binadamu wenzao consequently hawana moral Authority ya kukemea Mataifa mengine wasiwe nayo, kama wao wanafikiri mambom hayo yana wahakikishia Usalama wao kwanini hawataki Mataifa mengine kuyamiliki - they have a choice aidha waache Mataifa yenye uwezo wa kuyahunda na kuyamiliki wabaki nayo au wamiliki wa mabom hayo wakubaliane wote kuyahabiru including ya Wamerika wenyewe 4 the benefit/amani ya wakazi wote Dunani - atuwezi kuendelea kui-entertain double standard.
Mkuu nakupata vizuri, wala sitetei uhuni wa US kwa mataifa mengine.
Ninavaa viatu vya US au uongozi wao na sera zao yaani Marekani na Maslahi yake kwanza, mtu mwingine, Taifa lingine ni kipaumbele namba mbili kwa wazi au kificho.
Bill clinton alikili kabisa kuhusu Rwanda genocide wangeenda mapema wangeokoa watu zaidi ya 300, 000 lakini kwa sababu walikuwa na uzoefu wa kuuliwa kule somalia kwa wanajeshi wake walipotaka kumuambushi mbabe wa kivita Mohamed Farah Aideed, waliamua kukaa kimya maana maslahi yao pale hayakuwa makubwa.
"If we'd gone in sooner, I believe we could have saved at least a third of the lives that were lost...it had an enduring impact on me."Bill Clinton.

Huko kwingine kote, Hasa kwenye vita vingi America imekuwa na vision ya kuwa superpower na hasimu wake mkubwa amekuwa Russia hasa baada ya WW2. Ndio msingi wa Operation Paperclip na ile nyingine lakni ambacho hakujua Rais wao wakati huo wakati wao wanatafuta wanasayansi wa Hitler hiyo kazi ilikuwa inafanywa pia kwa siri Na red Army chini ya General Stalin na KGB. Huku Uingeleza nao wakiwa na kazi hiyohiyo. Proof ni pale mwaka 1953 walipojipa jukumu la UN kumrudisha nyuma N/Korea wakashangaa Ndege ambazo Technology yake wao waliitoa Kwa wanasayansi wa Hitler Babu yake Kim nae alikuwa nayo yenye sifa ileile na alipewa na warusi waliokuwa wanampa backup. Hapo ndio ingekuwa mwisho wa dunia maana Russia angeamua nae kuingilia moja kwa moja maana yake Kungekuwa na vita uso kwa us Russia na US hapo korea ambayo maana yake ni NUCLEAR WAR.

Kwa kutumia KGB russia nao walijaribu kuihujumu US lakini walizidiwa ujanja na CIA. kwa hiyo kwenye ulimwengu wa Fitna hapo hakuna common Friendship bali Common Interest. Hivyo basi anayofanya US hata nchi nyingine zinatamani kufanya sema uwezo hazina ikiwepo na Russia. Ndio maana sitashangaa kuona siku moja North Korea anakombola la kufika US kwa kupenyezewa na Russia ndio maana US 24/7 wanamonitor hapo wasione movement yoyote maana huyo jamaa bado wanaushirika wa karibu na russia. Ukitaka kujua nenda Siberia ujionee mamia ya Wanorth korea wakikata magogo huko kwa ajili ya nchi yao.

Kwa kuhujimu maslahi ya China na Russia, walichonganisha USSR ikasambaratika, waliwatumia mujahideen afganstan kusambaratisha maslahi ya urusi huko, Vietnam Russia iliwapa back up nao walifanikisha kuwachonganisha huko hadi ucommunist ukafeli, nicaragua na nchi nyingi za south amErika hivyohivyo etc.

Japan Walitakiwa kusuureender kwa gharama yoyote vinginevyo hadi leo ww2 isingeisha, njia pekee ya kuwatisha maadui na kuwadiscourage hao wajapani ilikuwa ni kufanya walichofanya. Libya waliua biashara ya mafuta china, Syria na Iraq anaua balance of power middle east ili mtu mwenye interest sawa na yeye Israel awe ndio pekee mwenye nguvu napo amefanikiwa kwa kiasi kikubwa, Pia wanauza silaha, private millitary contractors wao wanapata ajira, wanapata mafuta, wanapunguza nguvu za wale ambao wako kinyume nae, Ndio maana kupitia UN pia anawahujumu maadui wake wengi tu huku akipata nguvu kutoka kwa UK maana wengi wa walioko US walitokea huko na baadhi ya nchi za ulaya kwa hiyo ni kama ndugu pia.

Kwa hiyo ninachojua Yote US anafanya for their own Interests.
 
We ndo muongo
Dar to Musoma ni takribani km 1400...
Kutoka Tabora mpaka Musoma unavuka mikoa miwili ambayo average distance inaweza kua km 500 inamaana 1400-500 jibu lake ndio distance ya Dar to Tabora
Hivi kwa akili yako huwa unadhani Km za kombora zinazihesabiwa ni za Barbara? Kwamba linaanzia Posta, jangwani, magomeni Kimara, mbezi, kibamba, chalinze msamvu, gairo, kongwa, Dodoma, manyoni, itigi, tura, kigwa then Tabora? Nakushauri use unafuatilia mijadala kimya kimya ili upate kujifunza
 
Back
Top Bottom