error term
JF-Expert Member
- Jan 29, 2017
- 388
- 624
Mkuu nakupata vizuri, wala sitetei uhuni wa US kwa mataifa mengine.
Ninavaa viatu vya US au uongozi wao na sera zao yaani Marekani na Maslahi yake kwanza, mtu mwingine, Taifa lingine ni kipaumbele namba mbili kwa wazi au kificho.
Bill clinton alikili kabisa kuhusu Rwanda genocide wangeenda mapema wangeokoa watu zaidi ya 300, 000 lakini kwa sababu walikuwa na uzoefu wa kuuliwa kule somalia kwa wanajeshi wake walipotaka kumuambushi mbabe wa kivita Mohamed Farah Aideed, waliamua kukaa kimya maana maslahi yao pale hayakuwa makubwa.
"If we'd gone in sooner, I believe we could have saved at least a third of the lives that were lost...it had an enduring impact on me."Bill Clinton.
Huko kwingine kote, Hasa kwenye vita vingi America imekuwa na vision ya kuwa superpower na hasimu wake mkubwa amekuwa Russia hasa baada ya WW2. Ndio msingi wa Operation Paperclip na ile nyingine lakni ambacho hakujua Rais wao wakati huo wakati wao wanatafuta wanasayansi wa Hitler hiyo kazi ilikuwa inafanywa pia kwa siri Na red Army chini ya General Stalin na KGB. Huku Uingeleza nao wakiwa na kazi hiyohiyo. Proof ni pale mwaka 1953 walipojipa jukumu la UN kumrudisha nyuma N/Korea wakashangaa Ndege ambazo Technology yake wao waliitoa Kwa wanasayansi wa Hitler Babu yake Kim nae alikuwa nayo yenye sifa ileile na alipewa na warusi waliokuwa wanampa backup. Hapo ndio ingekuwa mwisho wa dunia maana Russia angeamua nae kuingilia moja kwa moja maana yake Kungekuwa na vita uso kwa us Russia na US hapo korea ambayo maana yake ni NUCLEAR WAR.
Kwa kutumia KGB russia nao walijaribu kuihujumu US lakini walizidiwa ujanja na CIA. kwa hiyo kwenye ulimwengu wa Fitna hapo hakuna common Friendship bali Common Interest. Hivyo basi anayofanya US hata nchi nyingine zinatamani kufanya sema uwezo hazina ikiwepo na Russia. Ndio maana sitashangaa kuona siku moja North Korea anakombola la kufika US kwa kupenyezewa na Russia ndio maana US 24/7 wanamonitor hapo wasione movement yoyote maana huyo jamaa bado wanaushirika wa karibu na russia. Ukitaka kujua nenda Siberia ujionee mamia ya Wanorth korea wakikata magogo huko kwa ajili ya nchi yao.
Kwa kuhujimu maslahi ya China na Russia, walichonganisha USSR ikasambaratika, waliwatumia mujahideen afganstan kusambaratisha maslahi ya urusi huko, Vietnam Russia iliwapa back up nao walifanikisha kuwachonganisha huko hadi ucommunist ukafeli, nicaragua na nchi nyingi za south amErika hivyohivyo etc.
Japan Walitakiwa kusuureender kwa gharama yoyote vinginevyo hadi leo ww2 isingeisha, njia pekee ya kuwatisha maadui na kuwadiscourage hao wajapani ilikuwa ni kufanya walichofanya. Libya waliua biashara ya mafuta china, Syria na Iraq anaua balance of power middle east ili mtu mwenye interest sawa na yeye Israel awe ndio pekee mwenye nguvu napo amefanikiwa kwa kiasi kikubwa, Pia wanauza silaha, private millitary contractors wao wanapata ajira, wanapata mafuta, wanapunguza nguvu za wale ambao wako kinyume nae, Ndio maana kupitia UN pia anawahujumu maadui wake wengi tu huku akipata nguvu kutoka kwa UK maana wengi wa walioko US walitokea huko na baadhi ya nchi za ulaya kwa hiyo ni kama ndugu pia.
Kwa hiyo ninachojua Yote US anafanya for their own Interests.
Nimependa umechambua vizur sana kwa pande zote, Asante mkuu