N/korea Watest Kombora lililosafiri kilometer 700

Walikuwepo watu hapa wakasema north kama mwanaume arushe tena haya karusha wamekuja na mlango wa nyuma sasa mara masikini mara marekani hajaamua mara third world basi tabu tupu lakini ukweli wametest na wamefanikiwa
haya kanunue kret la soda ufanye sherehe kwenu wakikuuliza wajibu n.k katest n, nafanikiwa Na hajapigwa.
 
Hao Japan na Skorea wanyamaze tu, wao si ndo walikua kimbelembele kulialia Marekani alipotaka kumdhibiti Nkorea. Wacha waendelee kunyooshwa
Marekani alisema hamsikilizi yeyote hao wengine wakizingua! Katika kumshuguhlikia Kim (rekodi za maelezo hayo zipo)
 
Kaka inabidi ufanye utafiti kidogo, nguvu ya keshi la korea kusini inatokana na mkono wa marekani hivyo korea kusini wanajeshi la anga la recent technology kuliko north korea mfano korea kusini wana ndege (war drones) nyingi za teknolojia ya kisasa kuliko north korea japo wana idadi ndogo ya wanajeshi kuliko n.korea lakini teknolojia yao ya kivita ni kubwa kuliko n.korea kwa ufadhilia wa USA kushinda vita ya kisasa unahitaji kuwa na technology kubwa ya kijeshi sio kuwa na wanajesh waliojipanga kama siafu, kim ni mpiga kelele tu.
Lazima u'define' hiyo technolojia kubwa nini! Baada ya hapo ueleze nani ana miliki nini!
 
Marekani alisema hamsikilizi yeyote hao wengine wakizingua! Katika kumshuguhlikia Kim (rekodi za maelezo hayo zipo)
Emb fatilia vzuri hzo rekodi zako uone kati ya Marekani na hao kina Japan nani alikua anabembeleza vikwazo zaidi na si kutumia nguvu za kijeshi.
 
HABARI

Silaha ya balistika ya Korea Kaskazini yadaiwa kufika kwenye sayari

Mei 14, 2017

Watu wanaangalia habari za Korea Kaskazini kurusha silaha ya balistika wakiwa katika kituo cha treni Korea Kusini.

Shirikisha

Korea Kaskazini imerusha kombora Jumapili katika anga za juu zaidi zisizo za kawaida katika njia inayopita silaha za balistika.

Hiyo ni dalili kuwa kunauwezekano kwamba Korea Kaskazini tayari iko katika uwezo mpya wa teknolojia ya balistika inayoendeshwa na nguvu ya nishati na mafuta yenye uwezo wa kupaisha kombora hilo mpaka kilometa 4,500.

Jaribio hilo kwa mujibu wa tamko la ikulu ya White House, “inalazimu kuwa ni ilani kwa mataifa yote kutekeleza vikwazo vikali zaidi dhidi ya Korea Kaskazini.”

Mapema, Japan na Korea Kusini mara moja zililaani kitendo cha Korea Kaskazini na kusema kuwa ni tishio kubwa kwa eneo hilo na ukiukaji wa azimio la Umoja wa Mataifa kuhusiana programu ya silaha ya Korea Kaskazini..

Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe, aliagiza serikali yake “kuandaa hali zote za tahadhari,” kwa mujibu wa taarifa ya ofisi yake.

“Urushaji wa kombora hili la ballistika ni tishio kubwa kwa nchi zetu. Wizara ya Ulinzi na majeshi yetu ya ulinzi yanaendelea kufanya kazi kwa karibu na Marekani na Korea Kusini katika kukusanya na kuchambua taarifa mbalimbali,” Waziri wa Ulinzi wa Japan Tomomi Inada amewaambia waandishi mjini Tokyo.

“Tutafanya juhudi zote tunazoweza kuhakikisha kuwa amani na usalama unakuwepo nchini kwetu.”

Waziri huyo amesema inawezekana kuwa aina mpya ya silaha ya balistika ambayo imerushwa katika pembe ya sayari ya juu kabisa, ambayo imekwenda umbali wa kilometa 2,000 na kuruka kwa dakika 30, kabla ya kurejea katika pwani ya Japan baada ya safari yake ya kilometa 700.

Hata hivyo China imetaka pande zote kujizuilia ili kuepusha hatari inayoongezeka katika eneo hilo wakati Wizara ya Mambo ya nje ikitoa kauli ya kupinga kitendo cha Pyongyang kukaidi azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Beijing ni mshirika mkuu pekee wa Korea Kaskazini na ni nchi kuu inayofanya biashara na Pyongyang.

Rais wa Russia Vladimir Putin, ambaye hivi sasa yuko Beijing kwa ajili ya mkutano wa kimataifa, ameeleza wasiwasi wake kuhusu jaribio la kombora na kuongezeka kwa hatari, kwa mujibu wa msemaji wa Ikulu ya Kremlin.

Mahali lilipoangukiwa kombora hilo ni kilometa 400 kutoka pwani ya mashariki ya Korea Kaskazini kwa mujibu wa serikali ya Japan.

Source . voice of America
 
Safi sana NK. Ni lazima wababe wajue wewe ni nani chini ya jua.
 
North korea wana kelele nyingi maonyesho mengi lakini vita hawawezi
Dogo kumbuka hawa hawanunui vifaa bali wanatengeneza wenyewe. Hivyo siri wanayo wenyewe. Kwa hiyo huu mtanange siyo wa haueleweki nani zaid.
 
Tatzo ni kwamba km 700 halifiki tabora,,waambie korea waongeze uref wa kombora lao ila km 700 bado sana
Hajasema linaishia km 700 wamesema 4500 ila kwenye test ndio wameishia 700 ssa ulitaka wafikishe 4500 kwani wapo vitani?
 
Hebu na wewe usitudanganye hapa. Source aliyo quote haijazungumzia hilo kilometre mnazozitaja.

Sasa sijajua kama ni akili yangu tu au ni kweli hayo yameandikwa hapo.
 
Attachments

  • IMG_2991.PNG
    IMG_2991.PNG
    134.3 KB · Views: 41
Tumwombe Mungu vita ya 3 isitokee kwani madhara yake yanatupata sisi moja kwa moja
Kwani ww unataka uishi duniani milele? Usiwe unataka kusikia tu historia ambazo hujazishuhudia omba angalau historia mojakubwa ya dunia uwe sehemu ya aliye shuhudia
 
Marekani ana makombora yanayofika popote duniani korea anatest km 700, marekani wana ndege za kivita za kisasa zenye gharama na zisizomilikiwa na nchi yeyote duniani, marekani huwez kumpiga kwa nuclear wala kwa mtutu tena bora korea kusini na china wanaweza kujaribu kumpiga marekani lakini sio N.korea
Sasa Trump analia nini?
 
Back
Top Bottom