Poise
JF-Expert Member
- May 31, 2016
- 7,660
- 7,948
Mbona hampigi sasa? Marekani sio muoga tumeona kwa Saddam, Osama na Gaddafi lakini kwa Kim amekua na maneno meengi
Marekani, ni muoga sana, asikundanganye mtu.
USA ni muoga Kwa sababu hizi
Kwanza, hataki kupigana vita ambayo ardhi yake itaguswa au watu wake kupata madhara ya moja Kwa moja.
Kitu ambacho Kim Un, amesema yeye ataifumua ardhi ya USA moja Kwa moja akiwa Pyongyang ataizamisha New York City, Washington DC hadi Pentagon .
Pili, Historia inamkataa Marekani hajawahi shinda vita akiwa peke yake uwanjani na game yenyewe ni tough sana hii ya Kim Un na NK Kwa sababu kuna nukes.
Tatu, washirika wa (USA ) wote sasa hivi wanamajanga aidha ya kiuchumi, kisiasa, au kiusalama mifano ni UK, Ujerumani, Ufaransa.
Kwa hiyo, katika matatizo yote hayo ya washirika wa USA wakifanya hesabu za haraka wanona Hakuna return watakayoipata kutoka aidha NK ama USA maana, hiyo vita itakuwa wao wanatumia pesa na nguvu kazi yao bila kupata faida . Kwani , NK hana maliasili yoyote mfano, mafuta ama madini. Kwa hiyo ni vita ambayo mikono haitapokea fadhila za mafuta au madini.
Nne, NK, naye anamsaada wa kijeshi, kisilaha, fedha kutoka China, Russia na Iran (hao ni washirika wa Karibu sana wa NK, tangia walipowekewa vikwazo hao ndiyo wamemsaidia hadi katika hizo nukes) Kwa mfano, NK, ina wanasayansi wake wanasaidia Iran kutengeneza nukes arsenals Kwa hiyo NK.
Tano, Nukes arsenals kutumika na Kim Un, kasema yeye hata risasi moja kutoka Kwa USA ikigusa ardhi ya NK itajibiwa Kwa vita kamili na siyo vinginevyo.
Ukumbuke, kiduku amepinda siyo wa mzaha kabisa.
USA hana inteligensia ya kutosha juu ya NK na Kim Un. Hilo nalo ni kikwazo, maana NK akimkamata mtu anayefanya aina yoyote ile ya udukuzi, ujasusi hukumu yake ni kifo na hukumu inatekelezwa ndani ya dakika chache sana baada ya hukumu.
Sababu, ni nyingi Sana, naomba nishie hapa japo niko na data nyingi.
Kwa hiyo, USA labda wampoteze Kim Un pekee na ni kitu ambacho bado ni kigumu kutekelezwa maana NK inteligensia na UwT wao uko vizuri Yaani mtu akifanya mawasiliano au mienendo yake ikitiliwa Shaka tu na NK hata kama ni Mwananchi majibu yake utayakuta makaburini.
Mfano, wiki jana jamaa mmoja raia wa NK amepewa dollar laki tatu ($ 300,000) na CIA agents wakishirikiana na South Korea agents ili amuue Kim Un, kwa sumu ya biochemical lakini alidakwa na intelligence agents wa NK.
Huyo jamaa , alikamatwa hadi muda huu tunavyoongea ameishapatiwa ile kitu watu wanaogopa sana hapo Tanzania inaitwa "Napenization"
Nitarudi tena. ... ... ...