Mzungu ana nini cha ziada?

Mzungu ana nini cha ziada?

.Daaah kwa hiyo unataka kuniambia haya yote ninayoyaona ni kwamba hayapo ila tu nimefanywa kuyaona hivyo? Hapana! Waafrika tupo nyuma kwenye kila kitu. Najaribu kutazama juhudi zilizotumika wakati wa kudai uhuru na yake yaliyofanywa na viongozi mara baada ya kupata uhuru. Natazama rasilimali tulizo nazo na umasikini tulio nao. WAAFRIKA ni tatizo hapa duniani

Siyo kweli. Tunaaminishwa tujione ni tatizo. Nenda nchi za watu ujionee, kuna wafrica wengi sana ni mabingwa wa fani mbali mbali. Lakini tayari washapewa uraia wa huko ili wasikumbuke wala kurudi makwao na kuendeleza. Angalia vitu kama Facebook, instagtam,whastsapp, ni za kawaida sana lakini, zinavyopewa promo na kuwa habari ya dunia mzima. Lakini angalia app zilizotengenezwa Africa/na waafric nikikuambia unitajia hata kumi hufikishi. Lakini zipo nyingi na nzuri sana. Africa tunaweza na tunafanya makubwa sana. Tatizo mfumo. Huo mfumo umefanya hadi sisi kwa sisi tujione wajinga hatuwezi na kurudishana nyuma.
 
kwa hiyo tumegundua nini cha maana wao wakaficha ?
magari ?
ndege ?
au nini ?

Acha ujinga wa kuamini kwamba kuna historia imefichwa

wazungu wanakimbia sisi waafrika tunatambaa

Na kama ni kweli tumegundua na wazungu wameficha ugunduzi wetu napo bado inaongeza kwamba wapo juu yetu, kwanini mtu mwingine afiche ugunduzi wako? Sisi tunaweza kuficha ugunduzi wao?
 
Amezaliwa kwenye baridi kama watu wa kasikazini na kagera
acha kujipa moyo,mbona huyo huyo ndo amekuvumbulia wewe air conditioner ili uweze kukabiliana na joto lako licha ya kuwa yeye kazaliwa kwenye baridi?kubali tu kuna vitu waafrika tumenyimwa...
 
Sayansi inakua kuendana na muda naamini kwa sayansi tuliyokua nayo na tusingeingiliwa leo hii tungekua mbali kwa namna yetu....

Wazungu waliharibu sayansi yetu.
Labda sayansi ya uchawi kwa kuuuwa na kuleta dini. Hapo ntakuelewa.
 
wamarekani weusi wamebobea kwenye fani kama hizi, basketball, soccer, boxing, american football, kuigiza , kuimba, rap, madawa ya kulevya na kuuana..
kwenye fani za teknolojia na sayansi wapo sana wakorea, wachina na wazungu, japo kuna weusi wachache pia, hii inaonyesha uwezo wa weusi wa kufikiria ni mdogo ukilinganisha na hao wengine
 
Huko nchini Ghana kulikua na usemi usemao hivi , ukiwa unaenda kwenye nyumba ya ibada, ukakutana na mzungu njiani basi rudi nyumbani kwa kuwa umekutana na Mungu
Hahaaa hata shetani tunaminishiwa ni MWEUSI Yaani uweusi ni ushetani jaribu kuangalia matendo yetu. Kitu cheusi ni kitu kisichofaa

Mfano blacklist, balckmails etc..
 
tutaishia kusema hivyo na kulalamika. Hebu tazama Marekani ilitawaliwa na UK, India ilitawaliwa na UK ila leo inauchumi mkubwa, China ilitawaliwa na Japan lakini leo Japan imepitwa mbali Sana, Korea ilitawaliwa na Japan lakini leo ina uchumi mkubwa.

Afrika Ina nchi sisizoonja makucha ya ukoloni lakini bado hali zao ni mbaya mf Ethiopia.
Very true but hopefully we will also get there one day
 
acha kujipa moyo,mbona huyo huyo ndo amekuvumbulia wewe air conditioner ili uweze kukabiliana na joto lako licha ya kuwa yeye kazaliwa kwenye baridi?kubali tu kuna vitu waafrika tumenyimwa...
Hahaha
 
Sisi weusi ni mashetani angalia hata viongozi wetu ni mashetani kweli we fikiria tu tuna rasimali kibao lakin hazitunufaishi,tunategemea misaada kuna liraisi lililopita liliulizwa kwanini nchi yako maskini na ina rasilimali nyingi likasema halijui
Bora tungewaacha wakoloni wakatutengenezea miji,sie hovyo sana hata akili zetu zinaweza kufanya mambo mepesi mepesi tu aaarghhhhhhhhhhhh

...ni kukesha makanisani kwa kwenda mbele sambamba na kuendeana kwa waganga wa kienyeji, chuki za ajabu ajabu, kufanyiana fitina, kuoneana wivu wa kijinga, majungu, unafiki, uongo, na kufanyiana ukatili wa ajabu ajabu wenyewe kwa wenyewe... alafu utakuta watu wanasema Mungu kawapendelea wazungu...
 
Salaam..

Wadau naomba kuuliza hivi mtu mweupe ususani mzungu, ananini cha zaida mpaka sisi ma Negro tunafikia kuleta misemo ya ajabu ajabu.

1. Bora kuzaliwa mbwa ulaya.
2. mzungu hazoei njaa.
3. mzungu ukitoa 'z' unapata Mungu.
4. Ulaya hakuna masikini.
5. Ahadi ya kizungu.

Na wengine inafika kipindi mpaka wanasema mzungu akija Afrika hapimi ukimwi lakini waafrika hupimwa maradhi yote, hili mimi siliafiki.
mimi naamini kuwa ni swala la muda tu, Africa tutapiga hatua na kukaribia maendeleo sawa na ya Ulaya, issue kubwa ni kuwa wao walitangulia kupata elimu,maendeleo, kustarabika etc ndio mana vijana wetu wengi wanatamani wawe kama wazungu, naamini na nitaendelea kuhamini kuwa Africa tutaifikia Ulaya katika nyanja kuu zote za uchumi..lakini si Africa hii ya kina Nkurunzinza, Shain, Mugabe etc
 
Kabla ya Hawa makatili (wazungu) kuja afrika, sayansi ya afrika ilikua juu sana gunduzi mbalimbali ziliendelea, fikiria pyramids zilivyojengwa, uhunzi mbalimbali, ugunduzi wa kalenda, Viwanda vya chuma..... Kuna mambo mengi yanafichwa kwenye historia... Kama mnavyomficha joh okello...

OPEN YOUR MIND.
Kuna wakat huwa inabid tuishi kwa fact kuliko hadithi za historia ambazo zina ujanja ujanja mwingi sababu tunatakiwa kukubali tu kuwa tumezidiwa sababu huo upeo wa kuboresha na kuendeleza huo uhunzi na ugunduzi wa kalenda uliishia wapi hadi mtu mweupe akapata upenyo wa kutufikisha hapa tulipo? Huko ndio kuzidiwa kwenyewe katika maarifa ni lazima tuukubali ukweli,

Wakati huyo mwafrica akigundua kalenda na hivyo vingine huyo mzungu alikuwa kagundua nini kwa wakati huo? Maana huenda tukabaki kujisifu kwa kalenda na hizo piramid kumbe wakat huo mzungu ana uvumnuzi mara 8 ya huo wa mwafrica

Tuukubali ukweli mzungu katuzid maarifa na alituzia tangia enzi na enzi wala tusifarijiane kwa vihistoria vya hapa na pale ndugu yangu.

Sisi waafrica tukazane kushindana kung'ang'ania madarakani tu maana ndio tulicho wazid wenzetu wazungu.
 
Last edited:
.

Nakumbuka jirani yetu (very poor people) waliiba mbwa ili wamuuze. Mbwa kakaa hapo kakondeana kaisha na kupata kupe. Wakaona wamtupe. Lakin alikuwa anarudi. Mwishowe wakaamua wamuue. Imagine anambeba mmbwa juu na kumpigiza kwenye sakafu. Nilitoka ndani nikawafwata nikawaambie nipeni huyu mbwa. Nikampigia rafiki yangu ana hobby ya mbwa amchukue. Tukachanga Vet akaenda kumtibu maskini. Kambwa kakaanza na kucheza. Kumbe alikuwa kavunjika uti wa mgongo akafa.
Baadae napewa umbea na housegirl, jirani ananisema nitatoaje 20,000 kumpandisha mbwa Bajaj badala ya kuwapa wao wale. Eti me ni mchawi!!

Unajua kadri muda unavyoenda binadamu anaendelea kukua kifikra. Tukubali tu ukweli kuwa wazungu wametuacha.

Tena hii ya kutreat wanyama ndo wametuacha mbali kabisaa.
Not only wana sheria kali dhidi ya ukatili kwa wanyama, but also wanathamini uhai na uwezo wa wanyama.

Wanaishi na wanyama nyumbani na kuwatunza.

Wana hospitali na foster homes za wanyama.

Imagine kuna madaktari wa upasuaji kwa ajili ya wanyama jamani!
Wakipata mnyama alieumia porini wanamchukua, wanamtibu, wanamrudisha. Sio huku bongo ukiokota kipaka kimeumia unaambiwa "subiri akuongeleshe, embu tupa huo uchawi".
Wana sheria za kutunza species za wanyama.
Wanajifunza tabia za wanyama hadi wanyama tuliowaogopa sasa wanaweza ishi nao peacefully (mf. simba)

Bora kuzaliwa mbwa ulaya kuliko maskini Africa

alafu watu wanakesha makanisani na misikitini, kumtaja Mungu kwenye kila jambo hadi kumsingizia mambo ya ajabu tunayoyasabisha wenyewe... ukatili watu wanaofanyiana haviendani...
Hivi tunaanzaje jamani kusema Mungu kawapendelea wazungu?
 
They do not look down on women.
They are good lovers. *wink * sio wanaume wa jf eti siridhishi tena mwanamke kumbe hajui game maskini

hahahahaha... wakisema wanajua game ujue wanamaanisha kutumia manguvu kama vile wako kwenye karakana/garage ya kutengenezea magari....Hivi inahitaji elimu gani kujua kuwa ile game inahitaji attention zaidi kuliko nguvu?
...housegirl ref: ule uzi wa jana, eti kumuwekea mwenzako madawa ya kulevya na kum-rape ndio kumpenda... Hivi mwanaume wa kizungu yeye angesemaje kwenye hilo?
 
hahahahaha... wakisema wanajua game ujue wanamaanisha kutumia manguvu kama vile wako kwenye karakana/garage ya kutengenezea magari....Hivi inahitaji elimu gani kujua kuwa ile game inahitaji attention zaidi kuliko nguvu?
...housegirl ref: ule uzi wa jana, eti kumuwekea mwenzako madawa ya kulevya na kum-rape ndio kumpenda... Hivi mwanaume wa kizungu yeye angesemaje kwenye hilo?
Nilishangaa idadi ya watu waliomtetea huyo mwanaume kuwa ni domo zege!!! Ndo uone jinsi mapenzi yalivyo huku. Kuridhishwa kutoke wapi mtu anachowaza ni atapiga kwa muda gani, doesn't matter at all mwanamke ana fikiria nini.

Ingekuwa imepostiwa uzunguni sidhani kungekuwa na hata comment moja inayotetea shetani lile. Labda religious fanatics
 
haribu kufuatia uvumbuzi wa vitu muhimu ulaya utakuja waamegundua vingi sana hata bulb unayotumia ya taa amegundua mwafirika tungekaa Gianni.madaktari wazuri ulaya ni mablack
 
mimi naamini kuwa ni swala la muda tu, Africa tutapiga hatua na kukaribia maendeleo sawa na ya Ulaya, issue kubwa ni kuwa wao walitangulia kupata elimu,maendeleo, kustarabika etc ndio mana vijana wetu wengi wanatamani wawe kama wazungu, naamini na nitaendelea kuhamini kuwa Africa tutaifikia Ulaya katika nyanja kuu zote za uchumi..lakini si Africa hii ya kina Nkurunzinza, Shain, Mugabe etc

Usijidanganye mkuu hakuna siku tutamfikia mzungu...mwal.nyerre kama sijakosea alisema ili kumfikia aliye mbele zaidi yako,yakupasa ukimbie wakati yeye anapotembea,badala yake wakati wenzetu wanakimbia sisi tunatembea,wenzetu wakitembea tunaKaa chini tunapumzika,the same to wanapotumia mamilion na sisi tumatumia bilions zaidi yao kwenye bajeti ya chai wizarani badala ya kuzitumia kujenga shule...wenzetu wanapotumia milion sisi tunatumia billions kufanya sherehe za uhuru
 
Back
Top Bottom