Mzimu unaotabasamu

Mzimu unaotabasamu

hadithi nyingine ulizopost zenye maadhi kama haya ni zipi???
 
mmh...leo lini vile waungwana??
nimepost juu hapo mkiona kkmya mjue haijapostiwa huko naloitoa na kwa hiki kknachoendelea sitapost simulizi ambayo haijaisha ntasubiri iishe nipost
 
nimepost juu hapo mkiona kkmya mjue haijapostiwa huko naloitoa na kwa hiki kknachoendelea sitapost simulizi ambayo haijaisha ntasubiri iishe nipost
Mmh...Madame S uwe na kifua nawe...

Hizi kelele chukulia kama mziki tu..

Ningekubembeleza ununuke...tatizo sina hakina kama ni ke au me ..maana humu..kuna ...vice verser..
 
MZIMU UNAOTABASAMU-20

Hakukuwa na mtu aliyekata tamaa, kila mmoja alikuwa akipambana kuhakikisha wanaiba kiasi cha naila bilioni tano kutoka katika Benki Kuu nchini Nigeria. Wiki nzima walikuwa wakifanya kazi hiyo kwa nguvu, waliingiza kila aina ya ‘codes’ kwa lengo la kuingia kwa urahisi ndani kabisa ya database lakini ilishindikana.
Hawakujua tatizo lilikuwa nini, kwa kipindi cha wiki nzima walichokuwa wamepambana pasipo na mafanikio haikuonekana kuwakatisha tamaa zaidi ya kuwahamasisha kwamba walitakiwa kufanya zaidi na zaidi. Walitumia ujuzi wao wa kila aina ili kufanikiwa katika hilo lakini ilishindikana kabisa.
“Tatizo nini? Kuna kitu tumekisahau?” aliuliza Mike huku akionekana kuchanganyikiwa.
“Hakuna ila nahisi kuna kitu hakipo sawa,” alisema Joshua.
“Kitu gani sasa?” aliuliza David.
Hakukuwa na mtu aliyejua sababu ya kutokuweza kuingia ndani kabisa ya database ya kompyuta hiyo. Kuna kipindi walitamani kuachana nayo lakini kila walipokumbuka jinsi walivyopambana mpaka kuhakikisha wanazipata namba, muda waliopoteza, wakaona kabisa kuachana nalo jambo hilo kilikuwa kitu kisichowezekana kabisa.
Mpaka kuingia ndani kabisa ya database kulikuwa na ulinzi mkubwa, kitu cha kwanza kabisa ambacho walitakiwa kukifanya ni kuvunja ulinzi huo na hakukuwa na kitu ambacho kingewezekana kuuvunja tofauti na kutengeneza virusi.
Lilikuwa jambo jepesi kuchukua virusi kama Autorun, Storm Worm, Trojan na wengine lakini wakahisi kabisa kwamba wasingeweza kuvunja ulinzi huo kwa kuwa tayari virusi hivy vilitafutiwa dawa, ilikuwa ni lazima watengeneze virusi vyao ambavyo vingekuwa hatari zaidi ya vile vilivyokuwa kipindi hicho.
“Nipeni nafasi hiyo. Nitatengeneza virusi ambavyo havijawahi kutokea katika uso wa dunia,” alisema David ambaye katika suala la kutengeneza virusi alikuwa mtu hatari.
Hiyo ndiyo kazi aliyoifanya. Akaanza kutengeneza virusi hivyo, alitaka kuhakikisha vinakuwa hatari ambavyo vingekuwa na uwezo wa kufungua mafaili yote. Haikuwa kazi kubwa, alihangaika kwani kila virusi alivyokuwa akivitengeneza alipojaribu kuchukua anti-virus ziliweza kuviangamiza virusi hivyo.
Alichukua wiki mbili ndipo akafanikiwa kutengeneza virusi alivyoviona hatari ambavyo alivipa jina la Davy Blaster Worm. Vilikuwa virusi hatari vilivyokuwa na uwezo wa kuharibu mafaili na hata wakati mwingine kuyaficha kabisa. Kila mtu akavipenda virusi hivyo kwani kwa jinsi vilivyokuwa na uwezo wa kuficha mafaili na hata kuharibu mafaili wakahisi kabisa vingeweza kuharibu ulinzi mkubwa uliokuwa katika database ya benki hiyo.
“Ila haviwezi kuharibu kabisa?” aliuliza Mike, alionekana kuingiwa na wasiwasi.
“Hakuna kitu kama hicho. Ninaingiza virusi kwenye database yao, baada ya hapo, kutafunguka, tunachukua pesa na kusepa zetu. Au mnaogopa?” alisema David na kuuliza.
“Kwenye suala la utajiri hakuna kuogopa, fanya mambo!” alisema Tim na hivyo kuanza kufanya mambo yake.
Hakukuwa na ugumu tena, kwa kutumia virusi hivyo akaingia ndani ya database, akaharibu mfumo mzima wa kuhifadhia mafaili na kisha kuingia katika akaunti mbalimbali za mabenki madogomadogo na kuanza kuchukua.
Walikubaliana kabla kuchukua kiasi cha naila bilioni tano lakini walipoona kwamba kuna uwezekano wa kuchukua hata zaidi ya naila bilioni mia tano, wakafanya hivyo na hivyo kila mtu kuingiziwa kiasi cha naila bilioni mia moja katika akaunti yake.
“One hundred bilion naila!” (Naila bilioni mia moja!) alisema Joshua huku akionekana kutokuamini alichokiona.
“Yes sir! We are bilionaires now!” (ndiyo mkuu! Sisi ni mabilionea sasa)
Kilichokuwa kimetokea ni kama kilikuwa ndoto moja kubwa ambayo hawakuwahi kuiota maisha yao yote. Walikuwa mabilionea, ni kama walilala wakiwa masikini lakini mwisho wa siku wakawa mabilionea wakubwa mno.
Kila mmoja akaingiziwa pesa hizo katika akaunti yake. Mfumo mzima wa kutambua kiasi cha pesa kilichokuwa kimeingizwa katika akaunti fulani ukaharibiwa na hivyo kuonyesha kwamba pesa ziliibiwa lakini hakukuwa na akaunti yoyote ambayo iliingizwa kiasi hicho cha pesa.
Hakutaka kuishia hapo, akawaambia wenzake kwamba walitakiwa kuzifuta picha zao katika mitandao ya kijamii, kwenye simu zao na kwenye kompyuta zao.
“Kwa nini?” aliuliza Tim.
“Wanaweza kutugundua.”
“Hakuna kitu kama hicho!”
David hakutaka kupuuzia hilo, alichokifanya ni kuchukua simu ya kila mmoja na kuanza kufuta picha zake. Hakutaka mtu yeyote abaki na picha zake kwani alihisi kabisa kwamba hapo baadaye watu wangeweza kuwatafuta kutokana na uhalifu walioufanya kuwa mkubwa mno.
Ni yeye tu ndiye aliyefuta picha zake lakini wengine wote wakapuuzia kwa kuona hakukuwa na ubaya wowote ambao ungetokea kwa kuwa tu wizi huo ulifanyika katika database ambapo hakukuwa na picha zao.
Alipomaliza, akawaambia kwamba huo ulikuwa muda wa kuondoka, kila mtu alitakiwa kusahau kila kitu kilichotokea na walitakiwa kuanza maisha mapya nje ya Nigeria.
“Mimi nitakwenda Ghana, nitafungua biashara na kufanya mambo yangu,” alisema Joshua.
“Mimi nitakwenda Senegal,” alisema Tim.
Kila mtu akachagua mahali pa kwenda. Hawakutakiwa kubaki nchini humo kwani kwa kiasi kikubwa cha pesa ambacho waliingiza ilikuwa ni lazima kutafutwa kwa nguvu zote. Wakati kila mtu akiwa ameamua kuondoka nchini Nigeria, David akampigia simu bilionea Armando na kumwambia kwamba alitaka kuelekea nchini Ujerumani kwani ule wizi aliokuwa amemtaarifu kabla ulifanikiwa.
“Kwa hiyo mmefanikiwa?” aliuliza mzee huyo.
“Ndiyo! Asilimia mia moja!”
Hicho ndicho kiichompa furaha mzee huyo, hakutaka kuchelewa, haraka sana akamtafutia hati za kusafiria kuelekea nchini Ujerumani. Hakukuwa na tatizo, alikuwa bilionea aliyeheshimika sana nchini humo, suala la kupata hati za kusafiria halikuwa tatizo hata kidogo.
Baada ya siku mbili, David alikuwa ndani ya ndege akielekea nchini Ujerumani. Moyo wake ukaridhika, kwa kile alichokifanya nchini Nigeria kilionyesha kabisa kuwa na hatari kubwa huko mbele, piga ua ilikuwa ni lazima kuondoka kwenda nchini huko kukaa kwa kujificha.
Wakati yeye akifikiria kwenda kujificha, kwa Mzee Armando alikuwa akifikiria kitu kingine kabisa. Alitaka kujihakikishia ulinzi, kwa jinsi alivyomuona David alijua kabisa kwamba kama angemtumia itakavyo basi kijana huyo angeweza kupambana kwa ajili yake na kuhakikisha anampa ulinzi mkubwa kama anaotaka kuwa nao maishani mwake.
Baada ya David kufika nchini Ujerumani, akachukuliwa na kupelekwa katika hoteli kubwa iliyokuwa katika Jiji la Berlin ambapo alitakiwa kukaa hapo mpaka siku inayofuatia ambapo angepelekwa nyumbani kwa mzee Armando.
***
Vijana wa IT walikuwa wakitetemeka, mashati mazuri waliyovaa yalilowanishwa na jasho zilizokuwa zikiwatoka. Hawakuamini kilewalichokuwa wakikiangalia kwenye kompyuta zao, kiasi kikubwa cha pesa kilikuwa kimeibiwa katika Benki Kuu nchini Nigeria.
Wao ndiyo walikuwa walinzi, ndiyo waliohakikisha kwamba hakukuwa na watu wabaya ambao wangeweza kuingia na kufanya uhalifu wowote ule. Pamoja na kuweka ulinzi mkubwa huku wakisaidiwa na watu wengine wa IT kutoka nchini Ufaransa na Afrika Kusini, bado kulikuwa na watu waliokuwa wameingia katika database ya benki hiyo na kuiba kiasi cha naila bilioni mia tano.
Hawakujua ni kitu gani walitakiwa kwenda kumwambia mkurugenzi wa benki hiyo, Bwana Daniel Ife. Waliamini kwamba ingekuwa moja ya taarifa mbaya ambayo hakuwahi kuipata tangu alipoanza kufanya kazi katika benki hiyo.
Wakatoka ndani ya chumba chao na kuanza kuelekea katika ofisi ya mkurugenzi huyo. Walipofika, wakahitaji kuzungumza naye. Kitendo cha kuwaona vijana hao, jinsi walivyokuwa akahisi kabisa kwamba kulikuwa na tatizo kubwa lililokuwa limetokea. Haraka sana akasimama.
“Network imeshuka tena?” aliuliza Bwana Daniel huku akiwaangalia vijana watatu waliosimama mbele yake.
“Hapana bosi.”
“Tatizo?”
“Pesa zimeibwa!” alijibu kijana mmoja.
“Unasemaje?”
Kijana huyo akarudia na kumwambia kiasi kilichokuwa kimeibwa ndani ya benki hiyo. Akahisi miguu yake ikikosa nguvu na kukaa chini. Kiasi kilichokuwa kimeibwa kilikuwa kikubwa mno, ni pesa za serikali na benki ndogo zilizokuwa zikihifadhi pesa humo. Alichanganyikiwa, akahisi mapigo ya moyo wake yakidunda kwa nguvu, kila alipowaangalia vijana wale akahisi kabisa moyo wake ungechomoka kwa jinsi ulivyokuwa ukidunda kwa nguvu.
Hapohapo akawapigia simu mabosi wenzake ndani ya benki hiyo na kuomba kuonana nao. Ni ndani ya dakika moja tu, mabosi wote wanne akiwemo Cecilia wakafika chumbani humo. Wakabaki wakimwangalia Bwana Daniel, kwa jinsi alivyoonekana tu walijua kulikuwa na tatizo kubwa lililokuwa limetokea.
“Kuna nini bosi?” aliuliza Sebastian.
“Naila bilioni mia tano zimeibwa kwenye benki hii,” alijibu Daniel kwa sauti ndogo. Kila mtu aliyesikia akashtuka.
Huo ndiyo ulikuwa ukweli, walichanganyikiwa, hawakujua pesa hizo ziliibwa vipi. Wakawauliza vijana wa IT ambao waliwaambia ukweli kwamba wizi huo ulifanyika baada ya wezi hao kuingia ndani ya database na kuharibu mafaili kisha kufanya uhalifu huo.
Hilo halikuwaingia akilini mwao, walijua kwamba kuingia kwenye database ilikuwa ni lazima kupata namba za kuingilia humo, sasa kama wezi hao waliingia na kuiba pesa, namba za kuingilia walizitoa wapi?
“Mlituambia kwamba hakuna mtu anayeweza kuingia pasipokuwa na namba za kuingilia ambazo ni sisi tu ndiyo tunazo, si ndiyo?” aliuliza Bwana Daniel.
“Ndiyo bosi!”
“Sasa wameingiaje pasipokuwa na hizi namba?” aliuliza Bwana Daniel.
“Hata sisi hatujui. Bila shaka walizipata namba hizi,”alijibu kijana mmoja.
“Walizipata namba hizi? Walizipataje? Nani aliwapa?” aliuliza maswali mfululizo, maswali ambayo hayakuwa na majibu yoyote yale.
Kitu cha kwanza kabisa kilichofanyika ni kutoa taarifa polisi na vijana wote wa IT kukamatwa kwa lengo la kuanzia upelelezi na kuwabaini watu waliokuwa wamefanya uhalifu huo mkubwa.
Taarifa hizo zilianza kuchuja baada ya kufika katika kituo hicho, taarifa zikaanza kusambaa kila kona kwamba kiasi cha naila bilioni mia moja kilikuwa kimeibwa kutoka katika Benki Kuu nchini humo. Kila mtu aliyesikia taarifa hizo alishtuka, hakukuwa na mtu aliyeamini kama kweli kiasi hicho cha pesa kiliibwa katika benki hiyo kirahisi namna hiyo.
Kila mmoja akakosa imani na benki hiyo kwa kuona kwamba hakukuwa na ulinzi wowote ule. Kama mwizi aliweza kuingia ndani ya benki hiyo na kufanya uhalifu namna hiyo, ilikuwaje kwa benki nyingine ndogo?
“Jamani hii ni hatari, watu wameiba benki!” alisema kijana mmoja.
“Ni hatari kweli. Ila benki inaibiwaje? Tena kubwa kama ile? Nahisi kuna kitu, kuna mchezo utakuwa umechezeka hapa. Hiki ni kitu kisichowezekana,” alisema kijana mwingine.
Rais Richard Ogunagu wa nchini humo alipopata taarifa alichanganyikiwa, hakuamini alichokisikia. Haraka sana kwa kupitia waziri wa ulinzi akamuagiza kuleta wapelelezi wa kimataifa kutoka Afrika Kusini kwa lengo la kwenda Nigeria na kufanya upelelezi juu ya kile kilichokuwa kimetokea.
Lisingekuwa jambo linalowezekana kwa kiasi hicho kuibwa huku kukiwa hakuna hata akaunti moja iliyoingizwa kiasi hicho cha pesa. Baada ya siku moja tu, wapelelezi kutoka Afrika Kusini wakafika nchini Nigeria tayari kwa kuanza kazi hiyo. Kitu cha kwanza kabisa wakataka kuonana na mabosi wanne waliokuwa na namba za kuingilia kwenye database kwa kuamini hapo ndipo mzizi wa wizi huo ulipofanyika.
***
Kuibwa kwa pesa katika Benki Kuu nchini Nigeria ikawa gumzo dunia nzima. Kila mtu alishangaa, lilionekana kuwa jambo gumu kuwezekana kwani kila mmoja alijua kwamba benki kubwa kama hiyo ilikuwa na ulinzi mkubwa hivyo kusingekuwa na uwezekano wa kuibwa kwa kiasi kikubwa namna hiyo.
Watu wakatoa maoni yao lakini suala kubwa ambalo lilizungumzwa kila kona ni juu ya kuhusika kwa viongozi kadhaa katika benki hiyo katika upoteaji wa pesa hizo. Hakukuwa na mtu aliyekubaliana na taarifa kwamba mwizi aliyekuwa amefanya uhalifu huo alitoka nje ya benki hiyo, kila mtu alikuwa na uhakika kwamba muhusika alikuwa ndani ya benki hiyo na ndiye aliyechora ramani nzima ya tukio hilo kufanyika.
Rais Richard hakutaka kusubiri, akaagiza viongozi wote wa benki hiyo kuwekwa ndani kwani aliamini kwamba kama wangebaki nje ingekuwa rahisi sana kuvuruga upelelezi uliokuwa umeanza kufanyika.
Benki haikuvamiwa, pesa ziliibwa kiteknolojia, watu waliokuwa wamefanya tukio hilo ilionyesha kabisa kwamba walikuwa wataalamu wa kutumia kompyuta kiasi kwamba mpaka watu wa IT kutoka katika benki hiyo walishindwa kutambua mpaka pesa hizo zilipoibwa.
Muda wote aliokuwa sero Cecilia alikuwa akilia. Moyo wake ulimuuma, hakuelewa ni kitu gani kilikuwa kimetokea mpaka wizi huo kutokea. Alichanganyikiwa, hakujua ni kitu gani alitakiwa kufanya, mbali na yeye, pia alikuwa na Bi Pamela ambaye naye alishikiliwa huku wakipisha upelelezi uliokuwa ukiendelea.
Kila siku ilikuwa ni lazima wapelelezi kutoka kituo kikuu cha polisi wafike mahali hapo na kuwahoji maswali kadhaa. Wapelelezi hao walijua kabisa kwamba watu hao wanne walikuwa wamehusika katika wizi huo kwani pesa zilihamishwa baada ya database kuvurugwa na hakukuwa na mtu yeyote aliyekuwa na uwezo wa kuingia ndani ya database zaidi yao.
Wao ndiyo walikuwa na namba za siri, kama kuna mtu mwingine aliingia humo, aliingiaje na wakati hakuwa na namba? Hilo likawapa uhakika kwamba watu hao walikuwa wamehusika katika uhalifu huo hivyo ilikuwa ni lazima wawaweke ndani huku wakiendelea kupeleleza ni kitu gani kilikuwa kimetokea.
Vijana ambao ni wataalamu wa masuala ya kompyuta, IT nao walikuwa ndani. Walishikiliwa kwa kuwa kulikuwa na uwezekano mkubwa wa kuhusika katika wizi huo kwa kuwa wao ndiyo walipewa jukumu la kuilinda database hiyo. Kama waliambiwa walinde kwa nguvu zote lakini mwisho wa siku pesa kuibwa, nani alikuwa amehusika zaidi yao?
“Watu wa IT na wale mabosi watakuwa wamehusika, ni lazima tuwahoji zaidi mpaka watuambie ukweli,” alisema Kamanda Mkuu wa Jeshi la Polisi, Nigeria, Bwana Agu.
Walichokuwa wakikihitaji wapelelezi ni ukweli wa kile kilichokuwa kimetokea. Hakukuwa na mtu aliyejua chochote kile, ni kweli hawakuhusika hata kidogo hivyo walishindwa kabisa kutoa ushirikiano kwa wapelelezi waliokuwa wakiwahoji kila siku.
Japokuwa alikuwa kwenye matatizo makubwa lakini Cecilia hakuacha kumfikiria mpenzi wake, David. Alimkumbuka mno, alihitaji kumuona lakini mpaka kipindi hicho hakujua mwanaume huyo alikuwa wapi. Alihisi kwamba kuna kitu kilikuwa kimetokea kwani kwa jinsi walivyokuwa wakipendana ilikuwa ni vigumu kwa wawili hao kutokuonana kwa siku tatu mfululizo na wakati alikuwa kwenye matatizo makubwa.
“David! Kwa nini hutaki kuja kuniona na kunijulia hali?” aliuliza Cecilia huku akilia peke yake.
Kwa wiki nzima walifanyiwa mahojiano lakini waliendelea kusema kwamba hawakumjua mtu aliyekuwa amehusika katika wizi wa pesa uliokuwa umetokea. Wale wapelelezi kutoka nchini Afrika Kusinina Ufaransa wakawa wanafanya kazi yao, walihakikisha wanafuatilia kila kitu kilichokuwa kimetokea.
Walikwenda katika ofisi za watu hao na kuanza kuangalia kama kulikuwa na kitu kilichokuwa kimetokea. Kila walipokuwa wakifika katika ofisi zao hawakuambulia kitu, hata ushahidi wa kile kilichokuwa kimetokea hawakuwanacho kabisa hali iliyoonyesha kwamba mabosi wale hawakuhusika na kulikuwa na ukweli kwamba hawakufahamu kitu chochote kile.
“Na simu zao?”
“Hazina dalili zozote zile. Labda tufuatilie kwenye makampuni ya simu,” alisema mpelelezi mmoja aliyeitwa kwa jina la Thierry kutoka nchini Ufaransa.
Wakaelekea huko na kuhitaji kuonana na watu wa kitengo cha mawasiliano, walitaka kuangalia simu zilizokuwa zimepigwa na hata meseji za simu zilizokuwa zimeingia katika simu hizo siku chache kabla ya kutokea kwa tukio hilo.
Hakukuwa na tatizo wakapewa kila kitu walichokihitaji, kilichowashangaza ni kwamba hakukuwa na simu yoyote mbaya au hata ujumbe ambao uliwafanya kuwa na wasiwasi nao. Wakachoka, wakakaa kwenye viti, mbele yao kulikuwa na mtihani mzito, hawakujua ni kitu gani walitakiwa kufanya ili kupata kile walichokuwa wakikipata.
Hawakutaka kubaki huko, wakarudi mpaka kituoni na kupeleka ripoti juu ya kile kilichotokea kwamba hawakufanikiwa na mbaya zaidi hata dalili za kuonyesha kwamba watu hao walikuwa wameshiriki katika wizi hawakuweza kugundua hilo.
“Kwa hiyo upelelezi unaonyesha kwamba hakuna kitu kama hicho?” aliuliza Agu.
“Hakuna kabisa. Ila kuna jambo tunatakiwa kufanya!” alisema Thierry.
“Lipi?”
“Bila shaka kulikuwa na watu waliokuwa wakiwafuatilia watu hawa, au walikuwa wakienda ofisini kwao, hivi hatuwezi kuanzia huko?” aliuliza Thierry.
Likaonekana kuwa wazo zuri, hawakutaka kuchelewa, wakaelekea ofisini huko kwa lengo la kuangalia kile walichokuwa wamehisi. Walipofika, wakawauliza wafanyakazi kuhusu uhusiano wa watu wale na watu wengine wa karibu lakini hawakupata kitu chochote cha kuwasaidia.
“Ofisi zao zipo wapi?” aliuliza Thierry.
Hilo halikuwa tatizo, wakapelekwa katika ofisi ya kila mmoja na kuangalia ndani ili kuona kama kulikuwa na kitu chochote kile. Walipofika, wakaanza kuangalia huku na kule lakini hawakubaini kitu chochote ila walipofika katika ofisi ya Cecilia, wakakutana na kitu ambacho kiliwapa maswali.
Juu ya meza yake kulikuwa na ua jekundu lililokuwa kwenye mfuko wake wa kuonekana. Lilikuwa kubwa, ilionyesha kabisa kwamba alitumiwa na mtu aliyekuwa akimpenda sana. Thierry akalichukua ua lile na kuliangalia, kwenye kikaratasi chake kulikuwa na manen machache sana sana yaliyosomeka ‘I love you’ yaani Nakupenda huku kwa chini kukiwa na namba zilizosomeka 2/5/18/12/9/14.
“Nani ameweka hili ua humu?” aliuliza Thierry.
Harakaharaka sekretari wa Cecilia akanyoosha mkono na kusema kwamba yeye ndiye aliyeliweka, alipoulizwa kuhusu mtu aliyemtumia msichana huyo akamwambia kwamba alikuwa mpenzi wake ambaye alifika ofisini hapo na kumwambia ua ampelekee Cecilia.
“Hakujua kama amekamatwa?” aliuliza Thierry.
“Sijajua! Nilishindwa kumwambia hivyo!”
“Unamjua?”
“Kila mtu humu ndani anamjua!”
“Anaishi wapi?”
“Sijui! Ila alikuwa akija ofisini na kuondoka tu.”
“Anaitwa nani?”
“David.”
Majibu hayo yakamtia hofu Thierry na kuhisi kwamba kulikuwa na kitu kilichokuwa kimetokea. Kwanza kitendo cha mpenzi huyo kutokwenda kituoni kumuona mpenzi wake na mwisho wa siku kuelekea kazini kwake kumpeleka ua kilionyesha kabisa kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea.
Wakaondoka mpaka kituoni ambapo moja kwa moja wakahitaji kuzungumza na Cecilia, hilo halikuwa tatizo, msichana huyo akapelekwa sehemu ya mahojiano na kuanza kuhojiwa juu ya kile kilichokuwa kimetokea.
Alikiri kwamba alikuwa mpenzi wake, alimpenda lakini tangu alipopata tatizo hakuwa amefika kituoni hapo kumuona kitu kilichomfanya kuwa na hofu kwamba inawezekana ndiyo ukawa mwisho wao.
“Na hizi namba ni nini?” aliuliza Thierry.
“Mmh! Sijui!”
“Itakuwaje akuandikie namba usizozifahamu! Hebu tuambie namba hizi ni za nini,” alisema Thierry.
Cecilia hakujua kitu chochote kile, yeye mwenyewe alibaki akizishangaa namba zile. Zilionekana kuwa kama tarehe lakini zilionekana kuzidi. Alihisi kabisa kulikuwa na sababu ya David kuandika namba zile, zilimaanisha nini? Na kwa nini zilikuwepo katika kikaratasi kidogo? Yeye mwenyewe akabaki na wasiwasi.
“Alikuwa anaishi mtaa gani?” aliuliza Thierry.
Cecilia akawaelekeza mtaa aliokuwa akiishi na Thierry huku akiongozana na polisi kumi na mbili kuanza kwenda huko. Walipofika katika jumba hilo wakagonga hodi na mwanaume mmoja kufungua mlango.
Wakajitambulisha na kuingia ndani. Kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kutaka kuzungumza na mtu aliyekuwa akiishi humo, walitaka kumtambua alikuwa nani na alikuwa na mahusiano gani na msichana Cecilia.
“Hakuna mtu humu!” alijibu mwanaume huyo.
“Hakuna mtu? Unamaanisha nini?”
“Walihama!”
“Walihama? Wangapi?”
“Wanne. Kwani kuna nini jamani?” aliuliza mwanaume huyo.
“Wewe ndiye mwenye nyumba?”
“Hapana! Mimi mlinzi!”
Wakataka kumuona mwenye nyumba. Hilo halikuwa tatizo kwani baada ya kupigiwa simu na kuambiwa kwamba alikuwa akihitajika na polisi akafika nyumbani hapo na kuonana nao, kitu walichokuwa wakihitaji ni kujua ni wakina nani walikuwa wakiishi humo.
“Wapangaji ila wamehama!”
“Ni wakina nani?”
“Vijana fulani hivi. Ukiniuliza wamehamia wapi, sifahamu chochote kile,” alisema baba mwenye nyumba.
Walichokifanya ni kumwambia ukweli wa kile kilichokuwa kimetokea, baba mwenye nyumba alikuwa kimya, alisikiliza kwa makini. Kwa jinsi polisi alivyokuwa akielezea ikawa kama naye akawa anakumbuka mambo fulani. Baada ya dakika chache, akaulizwa kama alikuwa na lolote la kusema.
“Kumbe ndiyo maanaaaa...” alisema baba mwenye nyumba huku akitingisha kichwa chini na juu.
“Ndiyo maana nini? Unafahamu nini kuhusu watu hawa?” aliuliza Thierry huku akimwangalia baba mwenye nyumba ambaye alikuwa na jambo alilotaka kuwaambia kuhusu watu waliokuwa wakiishi humo kwani hata naye maisha yao yalimshangaza sana.
“Hebu tuambie ulichokuwa ukikiona,” alisema Thierry na baba mwenye nyumba kujiandaa kusimulia kila kitu.
 
Back
Top Bottom