Madame S
JF-Expert Member
- Mar 4, 2015
- 17,177
- 34,444
- Thread starter
- #21
ERIC SHIGONGO
MZIMU UNAOTABASAMU-12
David na Davis walikuwa wakitetemeka, kila mmoja aliogopa, ni kweli waliwahi kumuona baba yao akiwa kwenye hasira kali lakini si kama alivyokuwa siku hiyo.
David alijua kile ambacho kingekwenda kutokea, baba yake alitaka kuwamaliza msituni hapo kwa kuwa alihitaji mkumridhisha mwanamke aliyekuwa akiishi naye.
David alibaki akimwangalia baba yake kwa hasira kali, hakuamini kama mwanaume huyo alikuwa radhi kuiangamiza familia yake kwa kuwa tu alimpenda mwanamke mwingine. Moyo wake ukajaa chuki na kumchukia mno baba yake kwani mbali na kutaka kuwamaliza, pia alimuua mama yao na kusingizia kwamba ni kansa ndiyo iliyommaliza mwanamke huyo.
“Ninakuchukia baba! Ninakuchukia kama shetani,” alisema David, hakutaka kubaki kimya, alijua kuwa huo ndiyo ulikuwa mwisho wake, akaona ni bora kumwambia baba yake kwamba alikuwa akimchukia.
Davis alishangaa, hakujua kaka yake alimaanisha nini, kwake, bado baba yake alionekana kuwa mtu mwema, alimpenda mno na kuona kuwa huyo ndiye mtu aliyebaki ambaye alitakiwa kuwa pamoja nao hasa baada ya mama yao kufa.
Gideon akatoa bastola yake, akaishika kwa nyuma, hakutaka watoto hao waione kwanza. Alidhamiria kufanya mauaji hayo msituni hapo lakini alipowaangalia tena watoto wake, kidogo huruma ikaanza kumuingia.
Davis alikuwa akilia lakini kwa David alikunja ndita huku akionekana kuwa na hasira kali kiasi kwamba akaanza kutetemeka, yaani kwa hasira alizokuwa nazo mahali hapo, kama angekabidhiwa bastola, asingejiuliza kumuacha baba yake, ilikuwa ni lazima amuue.
“Sina jinsi, naomba mnisamehe wanangu,” alisema Gideon huku akijiandaa kuwanyooshea bastola aliyoishika katika mkono wake aliouweka kwa nyuma.
“Paaa! Paaa! Paaa!” milio ya risasi ikasikika mahali hapo.
“Aauugghh...” ulisikika uyowe mkubwa pale walipokuwa wamesimama watatu hao. Damu ikatapakaa mahali hapo.
***
Mzee Msuya alichanganyikiwa, hakuamini kilichokuwa kimetokea, kitendo cha kupigiwa simu na kimada wake na kumwambia kwamba kulikuwa na watu waliokuwa wamemteka aliona kabisa kuna mtu alimshika sharubu na alitaka kuona makali yake.
Kwake, ilikuwa ni afadhali umuumize yeye lakini si msichana Juliet. Huyo alikuwa msichana pekee aliyekuwa akimpenda kwa moyo wa dhati, kitendo cha kumuumiza au kumfanya kitu chochote kile kilimaanisha kwamba mtu huyo alitaka vita.
Alijiangalia kiunoni mwake, kulikuwa na bastola yake iliyokuwa na risasi kumi, alijua fika kwamba alikuwa akienda kuitumia huko kwani asingeweza kutulia kuona Juliet akinyanyaswa na mwanaume mwingine na wakati alikuwepo.
Baada ya dakika ishirini akafika nyumbani hapo. Akateremka na kuanza kuelekea ndani ya jumba hilo. Kwanza mlinzi hakumkuta, akahisi kwamba kile alichokuwa ameambiwa kilikuwa kweli kabisa, akachukua bastola yake kutoka kiunoni na kuanza kuelekea ndani huku akiwa makini kabisa, alijiandaa kwa jambo lolote lile ambalo lingetokea.
Akafika mpaka sebuleni, hakukuwa na mtu, hakutaka kuita, akawa anaangalia sehemu nyingine kwa kujibanza, alipoona amekwenda mpaka jikoni hayupo akaanza kuita, akasikia miguno kutoka chumbani kwa Juliet.
Haraka sana akaanza kuelekea huko, alipoufikia mlango, akaufungua, hakuanza kuingia kwanza, aliogopa kufanya hivyo kwa kuhisi kwamba ndani kulikuwa na maadui na kama angeingia kwa fujo basi angeweza kupigwa risasi mfululizo, akasimama pembeni ya mlango na baada ya dakika tano, akaingia kwa kujibinua sarakasi pasipo kujali kitambi alichokuwanacho.
“Mmmh...mmmh...mmmh...” alisikia miguno kutoka kitandani.
Akayapeleka macho yake hapo, yakatua kwa mpenzi wake, Juliet aliyekuwa na mlinzi, wote wawili walikuwa wamelazwa huko mikono na miguu yao ikiwa imefungwa kamba ngumu ambazo zilifungwa mpaka katika kitanda hicho cha chuma na midomoni mwao walifungwa vitambaa.
Haraka sana Mzee Msuya akawasogelea, akavitoa vitambaa walivyokuwa navyo midomoni na kisha kuwafungua kamba. Kitu cha kwanza kabisa alichokifanya Juliet ni kumkumbatia Mzee Msuya.
“Walitaka kuniua...walitaka kuniua bebi,” alisema msichana huyo huku akianza kulia.
“Hawajakuumiza popote?”
“Hapana! Ila walitaka kuni...” alisema Juliet lakini hata kabla hajamaliza sentensi yake, akaanza kulia.
Wakakumbatiana lakini kidogo Mzee Msuya alionekana kuwa na maswali mengi kichwani mwake. Hakujua lengo kubwa la watu hao waliovamia nyumbani kwa mchepuko wake lilikuwa nini. Hawakuiba wala hawakumfanya kitu chochote kibaya, alijiuliza kama sababu ya watu hao ilikuwa ni kumtaka kumsumbua au ilikuwa nini.
Wakati akijiuliza maswali hayo, simu yake ya mkononi ambazo zilikuwa kwa watu wenye pesa tu kwa kipindi hicho. Haraka sana akaitoa kutoka mfukoni mwake, ilikuwa simu kubwa iliyofanana na redio call, akaipeleka sikioni, sauti ikaanza kusikia kutoka upande wa pili, ilikuwa ni ya mtu aliyekuwa akimfahamu kabisa.
“I have your family, I am going to kill them,” (nina familia yako, nitaiua) alisikia sauti kutoka upande wa pili.
“My family?” (familia yangu?) aliuliza huku akionekana kushtuka.
“This is just a message for you,” (huu ni ujumbe kwa ajili yako) aliisikia sauti hiyo na simu kukatwa.
“Halo...halo...halo...” aliita lakini tayari simu haikuwa hewani.
Hapo ndipo akapata jibu ya kile kilichokuwa kimetokea, aligundua kwamba alitolewa kanisani ili familia yake itekwe, akajaribu kumpigia simu mke wake, simu haikuwa ikipokelewa, hakukata tamaa, aliendelea kupiga zaidi na zaidi na mwisho wa siku simu haikuwa ikipatikana, ilionyesha kabisa kwamba ilikuwa imezimwa.
Alichanganyikiwa, hapo ndipo alipogundua kwamba familia ilikuwa ni muhimu kuliko hata Juliet. Hakutaka kubaki chumbani hapo, akasimama na kuondoka kwa mwendo wa kasi kwenda nje, akachukua gari lake na kuondoka bila hata kuaga.
Safari ilikuwa ni kwenda kanisani tu, aliamini kwamba huko angeweza kuikuta familia yake, alitumia dakika chache tu, akafika, akateremka, akaelekea kanisani, akakutana na mchungaji wake, kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kumuuliza ilipo familia yake.
“Sijui! Ila waliondoka hapa,” alisema mchungaji huku akimwangalia mzee huyo.
Akaona kabisa hapo hakukuwa na msaada, akalifuata gari lake na kuondoka kanisani hapo. Njiani alikuwa akiangalia huku na kule, alihisi kwamba angeweza kuiona familia yake sehemu, mpaka anafika nyumbani hakufanikiwa kuiona, akaingia ndani, napo dada wa kazi akamwambia kwamba familia yake haikurudi tangu walipokwenda kanisani asubuhi ya siku hiyo.
“Armando....!!” alijikuta akilitaja jina hilo.
Hakutaka kubaki nyumbani hapo, alichokifanya ni kuondoka na kuelekea kituo cha polisi ambapo akatoa taarifa kwamba familia yake ilitekwa na mtu aliyejulikana kwa jina la Armando. Polisi walipolisikia jina hilo, wakashtuka, hawakumwamini kwani mtu aliyekuwa amemtaja alikuwa mtu hatari aliyekuwa akitafutwa dunia nzima na Wamarekani wenyewe walishindwa hata kumpata.
“Armando huyu tunayemjua sisi?” aliuliza polisi mmoja.
“Huyohuyo! Amekuja Tanzania na kuiteka familia yangu, sijui walipo, naomba mnisaidie,” alisema Mzee Msuya huku machozi yakianza kumtoka.
Polisi wakapigiana simu za mezani na kupeana taarifa kwa kile kilichokuwa kimetokea, polisi wakajipanga kuanza kuisaka familia ya bilionea huyo. Kila mmoja alijiahidi kujitoa kwa nguvu kwani kama familia hiyo isingepatikana salama basi lawama za bilionea huyo zingekuwa juu yao.
***
Mzee Armando akapewa taarifa kwamba familia aliyokuwa akiihitaji ilikuwa mikononi mwa vijana aliokuwa amewatuma. Akawaambia kwamba waiweke sehemu na usiku wa siku hiyo wangekwenda sehemu kuimaliza na kuondoka nchini Tanzania.
Hilo halikuwa tatizo, familia hiyo ikapelekwa Kimara na kuhifadhiwa huko. Moyo wa Armando ukafarijika, hakuamini kama alifanikiwa kuiteka familia hiyo aliyokuwa akiihitaji kwa nguvu zote.
Mzigo wa madawa yake uliotapeliwa ulimchanganya, hakutaka kuiacha familia hiyo hai, alitaka kuimaliza, arudi nchini Ujerumani na kisha kupanga mikakati ya kummaliza Msuya mwenyewe.
Alikaa kitandani hotelini huku macho yake yakiwa kwenye saa yake, alikuwa akiangalia muda, alitaka itakapofika usiku wa saa moja aondoke kwenda kuonana na Theofil ambapo huko angemchukua na kumpeleka mahali familia ilipokuwa na kisha kuimaliza msituni.
Muda ulipofika, akakutana na Theofil ambaye alimchukua na kumpeleka huko. Alipofika, akaiangalia familia hiyo ya mke mmoja na watoto wawili. Akatoa tabasamu pana na kujiona kwamba alikuwa mshindi, akamwambia Theofil aichukue na wenzake na kuondoka nayo kwenda msituni kwani ilikuwa ni lazima kuimaliza haraka sana.
“Fanyeni haraka,” alisema mzee huyo.
Hilo halikuwa tatizo, kila kitu kilifanyika kwa haraka sana, familia hiyo ikachukuliwa, ikapakizwa ndani ya gari na kuelekea msituni. Hawakuchukua muda mrefu sana wakafika katika msitu wa Pande, wakaiteremsha na kuwataka kupiga magoti, Iddi akachukua bastola yake, alikuwa akisubiri amri ya bosi wake tu kwamba aimalize, basi afanye hivyo bila kuuliza lolote lile.
“Kill them,” (waue) alisema Armando.
Wakati Iddi akiwa amekoki bastola yake kwa lengo la kuwamaliza watu hao, ghafla wakaanza kuona mwanga wa gari, kwanza wakashtuka, haraka sana wakawawahi mateka wao na kuwafumba midomo.
Baada ya sekunde kadhaa wakasikia muungurumo wa gari ambalo lilitembea na kwenda kusimama sehemu. Wakabaki wakiliangalia, akili yao iliwaambia kwamba hilo lilikuwa gari la polisi ambao walikuwa na taarifa za kutekwa kwa familia hiyo.
Wakamuona mwanaume mmoja akiteremka kutoka ndani ya gari, akazungumza kidogo kisha kuwaagiza watu fulani wateremke. Macho yao yakawaona watoto wawili wakiteremka na kusimama mbele ya mwanaume huyo ambaye akaanza kuongea nao huku wakiwa hawasikii hasa kile kilichokuwa kinaongelewa.
“Who are they?” (ni wakina nani hao?) aliuliza Armando.
“We don’t know sir,” (hatujui mkuu)
Wakati wakiwa hapo, ghafla wakaanza kusikia milio ya risasi, mwanaume yule, Gideon aliyekuwa amesimama na watoto wale akapigwa risasi ya mkono na begani, akaanguka chini, bastola aliyokuwa nayo ikadondoka. Watoto wale walipoona hivyo, Davis akakimbilia ndani ya gari na David kuanza kwenda kule walipokuwa wao kwani hakuwa akijua kama kulikuwa na watu wengine.
“Who shot them?” (nani amewapiga risasi?) aliuliza Armando.
“Wasn’t me sir,” (siyo mimi mkuu)
Ghafla wakawaona wanaume watatu wakielekea kule walipokuwa watu wale huku wakiwa na bastola mikononi mwao. Wakajua kwamba watu hao walikuwa hatari hivyo walichokifanya ni kuanza kuwashambulia kwa risasi mfululizo.
“Paaa...paaa...paaa...” milio ya risasi ikasikika mahali hapo, wanaume wale waliokuwa wametumwa na Lucy wakaanguka chini na damu kutoka miilini mwao.
“Kill them! Do this fast man,” (waue! Fanya haraka) alisema Armando kwani tayari walijua kuwa eneo hilo halikuwa salama hata kidogo.
Hawakutaka kuchelewa, haraka sana wakaanza kuipiga risasi za vichwa familia ya Mzee Msuya, ilikuwa ni lazima kuimaliza kwani hawakwenda nayo mahali hapo kupanga mikakati, kilichokuwa kimewapeleka kilikuwa ni kufanya mauaji tu.
Wakati wakiwa wamekwishawapiga risasi za vichwa mfululizo kiasi kwamba ilikuwa hata shida kuwatambua, wakakumbuka kwamba kulikuwa na mtoto mmoja alikuwa amekimbia kutoka kule lilipokuwa lile gari, walipoangalia, kwa mbali walimuona akiwa amelala chini kwani milio ya risasi ilimuogopesha na kuhisi kwamba kama angekimbia basi angeweza kupigwa risasi mfululizo, hivyo kulala kwake ikaonekana kuwa kama nafuu.
Iddi akachomoka kwa kasi, akamfuata David pale alipokuwa amelala, alipomfikia, akambeba juujuu na kurudi naye kule walipokuwa wenzake.
David alikuwa akilia, aliuona mwisho wake, alikuwa mikononi mwa watu hao walioonekana kuwa na hasira mno na ndiyo watu waliokuwa wamewapiga watu wengine risasi mfululizo. Alijaribu kuwaomba msamaha wamuache aondoke lakini hakukuwa na mtu aliyejali.
“Tukimuacha, kuna siku atasema kilichotokea, huyu amekwishakuwa shahidi wa kila kitu kilichotokea. Kwa usalama wetu lazima tumuue,” alisema Theofil huku akiwaangalia wenzake, wakati huo David alikuwa chini akilia.
“Sawasawa. Mpige risasi za kichwa kama hiyo familia,” alisema Armando na hapohapo Iddi kuikoki bastola yake tayari kwa kumpiga risasi David