Madame S
JF-Expert Member
- Mar 4, 2015
- 17,177
- 34,444
- Thread starter
- #201
MZIMU UNAOTABASAMU-24
Davis alikuwa jijini Kampala nchini Uganda akiendelea na masomo yake, moyo wake haukuwa na amani, tangu siku ambayo alijua kwamba pacha wake aliuawa msituni walipokuwa wamekwenda, hakupata raha hata kidogo.
Hakujua kitu gani kilimfanya baba yake kuchukua uamuzi wa kuwapeleka msituni kule, kila alipotaka kumuuliza moyo wake ulisita na hivyo kubaki kimya, ukimya ambao aliamini kwamba ungedumu milele ndani ya moyo wake.
Maisha jiji Kampala nchini Uganda yalikuwa mazuri, aliishi shuleni alipokuwa akisoma, akili yake akaiweka katika masomo na kuachana na mambo ya kufikiria mambo mengine. Shuleni hapo alipokuwa akisoma, alikuwa muongeaji sana, alijenga urafiki na watu wengi kiasi kwamba Waganda wakaamini kwamba hakukuwa na watu waliokuwa wakiongea sana kama Watanzania.
Siku zikakatika, baada ya miaka sita akamaliza masomo yake na hivyo kuamua kwenda kusoma katika Chuo Kikuu cha Nairobi na kuchukua masomo ya biashara.
Ucheshi wake uliendelea kuwa vilevile, akajijengea marafiki wengi huku wengine wakitamani kuona wanakuwa naye karibu kila siku. Darasani alikuwa na uwezo mkubwa, alitoka katika familia yenye pesa hivyo kila kitu alichokuwa akikihitaji alikipata kwa haraka sana.
Japokuwa Davis alikuwa mcheshi, aliyezungumza na kila mtu chuoni hapo lakini hakuwa mtu wa wanawake kabisa. Alipendwa, kila mwanamke alitamani sana kulala naye lakini hilo lilishindikana kabisa.
Wanaume wengi wakamkejeli, walimtania na kumpa jina la Papa kwa kitendo chake cha kutotaka kuwa na mwanamke yeyote yule. Jina hilo likampa umaarufu mkubwa, mbali na kujulikana ndani ya chuo hicho pia akaanza kujulikana mpaka nje ya chuo hicho.
“Eti chalii, kwa nini hupendi manzi ya Nairobee?” aliuliza jamaa mmoja kwa lafudhi ya Kikenya.
“Sijaamua kuwa na mwanamke Oliatuu. Nikiamua, hata dada yako Arafa muweke mbali,” alisema Davis na kuanza kucheka.
Japokuwa kulikuwa na wanawake wengi waliokuwa wakimpenda, lakini msichana aliyekuwa amekufa na kuoza kwa Davis alikuwa Evelina. Huyu alikuwa msichana mrembo wa kimasai aliyekuwa akiishi Mombasa hapohapo nchini Kenya.
Alikuwa msichana mrembo, mwenye macho makubwa na vishimo katika mashavu yake. Umbo lake lilikuwa machachari, alipenda kusuka kichwani, miguu yake ilikuwa minene na kila alipotembea aliringa kama twiga.
Wanaume wengi walimpenda Eveline, wengi walimfuata na kumtongoza lakini hakukuwa na mtu aliyefanikiwa kulionja penzi lake. Alifuatwa na wanaume wengi lakini moyo wake ulikuwa kwa Davis tu.
Mwanaume huyo alimpagawisha, alimpenda kupita kawaida. Kila alipokuwa akimuona, moyo wake ulikufa na kuoza, hakuajiamini, kwake, mtu aliyekuwa ameuteka moyo wake alikuwa mwanaume huyo tu na hakutaka kusikia jambo lolote lile zaidi ya kuona akiuteka moyo wa mwanaume huyo na kuwa naye.
Aliogopa kumwambia, alijisikia aibu kubwa. Kwa sababu Davis alikuwa mchangamfu sana, kila alipokuwa, alihakikisha na yeye anakuwa mahali hapo na kuanza kumsikiliza kila neno alilokuwa akiliongea.
Alivumilia kwa siku nyingi lakini mwisho wa siku akaamua kumwambia ukweli. Hakutaka kuogopa tena, hakutaka kuona akiendelea kuumia moyoni mwake, alichokiamua ni kumfuata na kumwambia kuhusu hisiia zake, jinsi mapenzi yalivyokuwa yakimtesa usiku na mchana.
“Unanipenda mimi?” aliuliza Davis, kwa kuwa alikuwa mtu wa utani sana, hata uulizaji wake ulikuwa wa masihara sana.
“Ndiyo!”
“Jamaniiii! Kwa hiyo nakutesa sana!”
“Ndiyo! Nahitaji uwe mpenzi wangu, ninakupenda mno David,” alisema Eveline huku akimwangalia David.
Hilo lilikuwa gumu kwake, aliyaogopa mapenzi, hakutaka kabisa kuona akiyapa nafasi mapenzi hayo, alitaka kubaki hivyohivyo, hakutaka msichana yeyote aingie ndani ya moyo wake kwa kuwa tu aliogopa kuumizwa.
Hakukubaliana na Eveline, mpaka chuo kinafungwa na kurudi jijini Dar huku msichana huyo akirudi Mombasa wakawa hawajakubaliana kuwa wapenzi.
Jijini Dar es Salaam waliendelea kuwasiliana, walizungumza sana kwenye simu, msichana huyo aliendelea kumsisitiza Davis awe naye lakini mwanaume huyo hakutaka kabisa kukubaliana naye, alimwambia kuhusu msimamo wake kwamba muda wa kuwa na mwanamke haukuwa umefika, kama kweli alimpenda alitakiwa kusubiri.
“Utatakiwa kusubiri,” alisema Davis.
“Mpaka lini?”
“Hapo nitakapoamua. Vuta subira Eveline,” alisema Davis, na maneno hayohayo ndiyo aliyokuwa akimwambia kila siku.
“Sawa. Haina shida! Nitakusubiri.”
***
David alikuwa ndani ya daladala iliyoanza kuondoka kuelekea Bagamoyo, alikaa dirishani, aliiwaona wanaume waliokuwa wakizungumza kwa mbali huku wakimwangalia yeye.
Moyo wake ukaogopa na kuhisi kwamba ile karatasi waliokuwa wameishika watu wale ilikuwa na picha yake. Alichokifanya, akainama, kuivua sura yake ya bandia halikuwa jambo gumu, ilikuwa imepachikwa tu. Kitendo cha kuinama huku akiwa ameuegemea mkono wake katika kiti cha mbele, akaanza kuivua pasipo mtu yeyote kugundua. Alipoona imetoka, akaitupa chini ya kiti cha gari na kutulia.
Ndani ya dakika moja tu, wanaume wale wakasimamisha daladala ile kwa lengo la kuingia ndani. Walimwambia dereva kwamba walimuona mwanaume yule aliyekuwa akitafutwa akiwa ndani ya gari lile.
“Jamani! Yaani nyie mmuone halafu abiria wote humu ndani wasimuone! Kweli?” aliuliza dereva lakini kwa kuwa vijana hao waling’ang’ania kuingia ndani ya gari, akawaruhusu.
Wakaingia, kitu cha kwanza kilikuwa ni kuangalia katika kiti alichokalia David, ni kweli walimuona mwanaume yule akiwa katika kiti kile lakini walipoangalia tena, kulionekana kuwa mtu mwingine kabisa.
“Yupo wapi?’ aliuliza mwanaume mmoja.
“Alikuwa hapa. Eeh! Mbona kuna mwingine?” aliuliza jamaa mwingine.
Walichanganyikiwa, hawakujua ni kitu gani kilikuwa kimetokea. Mwanaume aliyekuwa amekaa katika kiti kile alikuwa mwingine kabisa lakini nguo zake zilikuwa zilezile. Hawakujua kama wao walichanganya au la. Ilikuwaje aonekane mtuhumiwa lakini baada ya dakika kadhaa kuonekana mwanaume mwingine.
“Oya braza! Jamaa aliyekuwa hapo yupo wapi?” aliuliza jamaa mmoja huku akimwangalia David.
“Hakukuwa na mwingine zaidi yangu!”
“Hapana! Kulikuwa na huyu mwanaume!” alisema huku akimuonyeshea picha.
“Hapana! Nimekaa mimi tangu mwanzo,” alisema David.
Hawakutaka kuridhika, waliendelea kumwangalia kila abiria aliyekuwa ndani ya daladala hiyo lakini hawakufanikiwa kumuona mtu waliyekuwa wakimtafuta. Wakateremka na kuondoka huku wakiwa hawajui ni kitu gani kilikuwa kimetokea kwani mwanaume aliyekuwa katika picha ile walimuona akiwa ndani ya gari lile, ghafla baada ya kuingia, hakuonekana tena.
Kidogo David akashusha pumzi, akatulia na kujipa uhakika kwamba ilikuwa ni lazima kufika nchini Kenya kwa kuwa tu sura aliyokuwanayo ilikuwa nyingine kabisa, sura aliyozaliwa nayo ambayo hakukuwa na mtuu aliyekuwa akiifahamu.
Walichukua saa moja wakaingia Bagamoyo, hakutaka kupoteza muda, akawatafuta wavuvi na kuwaulizia kama kulikuwa na ngalawa yoyote ya kuelekea Mombasa.
“Siku hizi hakuna ngalawa kaka! Watu wanasafiri kwa jahazi!” alisema jamaa mmoja.
“Sawa. Mimi nataka kufika Mombasa, inakuwaje sasa?” aliuliza David.
Hilo halikuwa tatizo, alichokifanya mwanaume huyo ni kumwambia kuhusu jahazi ambalo lilitaka kusafiri kuelekea Mombasa kwa siri huku likiwa na watu waliokuwa na biashara zao za magendo.
Akatakiwa kulipa kiasi cha shilingi laki moja, hilo halikuwa tatizo, akalipia ana usiku wa siku hiyo akaunganishwa na watu wa jahazi na kuanza safari ya kuelekea Mombasa.
Bahari ilikuwa imetulia, hawakupata shida, walitumia saa kumi na nne mpaka kufika Mombasa huku wakiwa wamepitia Tanga. David akateremka na kuanza kuelekea katika hoteli ya Lion Kingi iliyokuwa hapohapo Mombasa pembezoni mwa bahari.
Akachukua chumba humo. Kitu cha kwanza kabisa alichokifanya ni kuwasiliana na mzee Armando na kumpa taarifa kwamba alikamilisha kazi aliyokuwa amepewa, alimuua Msuya pasipo kugundulika.
“Unasemaje?” alisikika mzee huyo huku akionekana kutokuamini.
“Nimekamilisha kazi yako mzee. Hakuna mtu atakayegundua. Ingia katika mitandao ya Kitanzania uangalie, utakutana na taarifa hiyo,” alisema David kwa sauti ya kujiamini.
Upande wa pili mzee huyo akafanya kama alivyoambiwa, alichokutana nacho humo kilikuwa kilekile, kulikuwa na habari iliyoripotiwa sana na vyombo vya habari kwamba bilionea huyo alikutwa amekuffa ufukweni.
Moyo wa Armando ukaridhika, akajikuta akitoa tabasamu pana na kuanza kurukaruka chumbani kwake. Mtu ambaye alimuhangaikia sana kwa kipindi kirefu amuue na kushindwa leo hii aliuawa na kijana aliyeamini kwamba angemsaidia huko mbele. Kwake, akamuona David kufaa kufanya kazi.
Katika daftari lake alikuwa na watu wengi waliotakiwa kuuawa kwa kuwa tu aligombana nao. Ukiachana na Msuya, kulikuwa na mtu mwingine aliyetaka sana auawe, huyo aliitwa Fabian Petrescu, mwanaume aliyekuwa raia wa Romania aliyekuwa akiishi nchini Ufaransa.
“Huyu ndiye anayefuata. Nitahakikisha nawamaliza wabaya wangu wote kupitia huyu David, naamini atafanikisha mipango yangu yote ya mauaji,” alisema mzee Armando.
Wakati akiwaza hayo bado David alikuwa hotelini, kichwa chake kilikuwa na mawazo tele, bado picha aliyokuwa msituni na baba yake ilikuwa ikizunguka kichwanai mwake, moyo wake ulimuuma, hakuacha kuwa na hasira dhidi ya baba yake huyo. Hakutaka kumuua, kila siku alipanga kumfanyia kitu kimoja ambacho kingemfanya kujutia kile alichokuwa amemfanyia.
Ilipofika majira ya saa kumi na mbili jioni, David akatoka kwa lengo la kutembea hapo Mombasa, alitaka kuzunguka mji huo baadhi ya sehemu kwa kuwa alijua kuwa alikuwa salama kabisa. Hakutaka kuchukua teksi, aliamua kutembea kwa miguu ili auone mji huo vizuri kabla ya kwenda Nairobi ambapo angechukua ndege na kuelekea Ujerumani.
“Davie...Davie...Davie...” alisikia akiitwa kwa nyuma.
Akashtuka, hakuamini kama kulikuwa na mtu aliyekuwa akimfahamu. Akageuka, macho yake yakatua kwa msichana aliyekuwa akija kwa kasi huku akiwa na tabasamu pana, alipomfikia, akamkumbatia kwa furaha.
“Why didn’t you tell me that you are coming?” (kwa nini hukuniambia kwamba unakuja?) aliuliza msichana huyo huku akiwa amemkumbatia. David alibaki akishangaa, msichana huyo alikuwa mgeni kabisa, hakumfahamu, sasa ilikuwaje amfuate na kumkumbatia kiasi kile kana kwamba alikuwa akimfahamu.
Hakutaka kumwambia kwamba alimfananisha, ili kwenda naye sawa naye akajifanya kumchangamkia na kumkumbatia, alichokitaka ni kujuua mwanamke huyo alimfananisha na nani.
“Why?” (kwa nini?)
“I am sorry! I was very busy!” (samahani! Nilikuwa bize sana) alisema David.
Msichana huyo akamwangalia David kwa macho yaliyoonyesha mapenzi yote aliyokuwa nayo, akamshika mkono na kumwambia waende sehemu fulani kwani kulikuwa na kitu alitaka kumuonyesha. David akakubali, akaanza kwenda naye huku huku kichwa chake kikiwa na mawazo lukuki kwamba msichana huyo alikuwa nani.
Akampeleka mpaka katika hoteli moja iliyoitwa Giraffe na kumwambia kwamba hiyo hoteli ilikuwa ya baba yake. David akafurahi tu lakini bado kichwa chake kilikuwa na maswali lukuki juu ya msichana huyo, alikuwa nani na alijuaje vipi kama aliitwa David?