Mzee Yusuph: Walio na nyimbo zangu kwenye simu zao wafute

Ngoja na sisi tuchume mali za dhambi kama alizochuma Mzee Yusuph kisha ndipo tutatubu.
Kama anataka fair kwa Mungu basi agawe bure kwa yatima mali alizochuma kwa dhambi, hapo ndipo atapata toba ya haki.
 
Atoe nyumba na gari zote alizozipata kupitia taarabu kwa yatima..nitamuona wa maana...
Mbona jahazi bado iko..si aifunge band
 
Mliokuwa mnasema ati Shetwani akizeeka hawi malaika mnahitaji kujichunguza sana. Mbona hawa wanabadilika??
 
Kweli man,nyimbo zilizopo kwenye simu watu wametoa pesa ambazo kwa namna moja au nyingine ndo kajengea nyumba and so far,kama dhambi arudishe vitu vyote vilivo tokana na mziki dhambi,sasa natambua inawezekana nyimbo zake zina dhambi kubwa ya kitafsiri tofauti na tunavoziskia
Aliyekuwa mfalme wa muziki wa taarab nchini, Mzee Yusuph amefunguka na kueleza kuwa watu wote walio na nyimbo zake kwenye simu zao wafute na kuacha kusikiliza ili kuepuka dhambi.

Katika mahojihano na kipindi cha Mitikisiko ya Pwani cha Times Fm, Mzee Yusuph ameelezea maisha yake ya ndoa, kidini na kiuchmi yalivyo kwa sasa ukilinganisha na hapo awali.

“Mimi nikikubali watu wacheze nyimbo zangu ina maana nimeruhusu dhambi tena ni bora nirudi kuimba muziki tena hivyo, watu wote waliokuwa na nyimbo zangu kwenye simu zao wafute na kuacha kusikiliza kuepuka dhambi,” amesema Mzee Yussufu.

Mzee Yussufu amesema yeye hayupo kwenye kundi lake la ‘Jahazi Modern Taarab’ kama baadhi ya watu wanavyodhani na wala hafuatilii kabisa kundi hilo.

“Nilitaka kulivunja Kundi la Jahazi lakini sheria za nchi haziruhusu nikaliacha na haya niliambiwa na Basata wenyewe. Vyombo vya bendi ya Jahazi havikuwa vya kwangu tulikuwa tunasaidiana na mabosi,” amesema.

Katika hatua nyingine Mzee Yusuph amesema maisha ya kiuchumi kwa sasa ni toufauti na kipindi alichokuwa anafanya muziki kwani hapo awali kwa wiki alikuwa anaweza kutengeneza milioni moja na nusu mpaka mbili ila sasa kushika laki tano au milioni inaweza kumchukua miezi miwili.

Ameongeza kuwa wake zake wanne bado anaendelea kuishi nao kama kawaida, na kuwa na wake ni jambo ambalo amehimizwa na sio amri, na kwa sasa wanamjua ni mtu wa namna gani na mambo yote yanaenda sawa hakuna hata mmoja anayefanya sivyo.

d28c79aae0e581a8717129ee818cf03a.jpg
 
Inasemekana 5star aliusika sanaaa kweny kuwatoa kafara ni vizur alivo ungama mapema ila sjuo km Mungu atamsamehe
 
Mtaji wote aliopata wa kuuza simenti na matofali apeleke msikitini, asituzingu muhuni tu huyu.
 
Aliyekuwa mfalme wa muziki wa taarab nchini, Mzee Yusuph amefunguka na kueleza kuwa watu wote walio na nyimbo zake kwenye simu zao wafute na kuacha kusikiliza ili kuepuka dhambi.

Katika mahojihano na kipindi cha Mitikisiko ya Pwani cha Times Fm, Mzee Yusuph ameelezea maisha yake ya ndoa, kidini na kiuchmi yalivyo kwa sasa ukilinganisha na hapo awali.

“Mimi nikikubali watu wacheze nyimbo zangu ina maana nimeruhusu dhambi tena ni bora nirudi kuimba muziki tena hivyo, watu wote waliokuwa na nyimbo zangu kwenye simu zao wafute na kuacha kusikiliza kuepuka dhambi,” amesema Mzee Yussufu.

Mzee Yussufu amesema yeye hayupo kwenye kundi lake la ‘Jahazi Modern Taarab’ kama baadhi ya watu wanavyodhani na wala hafuatilii kabisa kundi hilo.

“Nilitaka kulivunja Kundi la Jahazi lakini sheria za nchi haziruhusu nikaliacha na haya niliambiwa na Basata wenyewe. Vyombo vya bendi ya Jahazi havikuwa vya kwangu tulikuwa tunasaidiana na mabosi,” amesema.

Katika hatua nyingine Mzee Yusuph amesema maisha ya kiuchumi kwa sasa ni toufauti na kipindi alichokuwa anafanya muziki kwani hapo awali kwa wiki alikuwa anaweza kutengeneza milioni moja na nusu mpaka mbili ila sasa kushika laki tano au milioni inaweza kumchukua miezi miwili.

Ameongeza kuwa wake zake wanne bado anaendelea kuishi nao kama kawaida, na kuwa na wake ni jambo ambalo amehimizwa na sio amri, na kwa sasa wanamjua ni mtu wa namna gani na mambo yote yanaenda sawa hakuna hata mmoja anayefanya sivyo.

d28c79aae0e581a8717129ee818cf03a.jpg
Mungu azidi kumsaidia katika toba yake na ss tujifunze na kutubu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom